Atakua mke wa nani ? Angalizo ichangiwe na Great Thinkers Only.

Judgement

JF-Expert Member
Nov 13, 2011
10,327
4,779
Nimetanguliza ANGALIZO kwamba ni Great Thinkers Membar, ndiyo ningeomba wanichangie katika agenda hii mezani.
Mizaha, Utani, Kubeza, Mas'khara, Uchakachuaji wa Thread ni vitu viendeleavyo kukua hapa Kijijini kwetu siku baada ya siku.
Ukishajiyakinisha sifa tajwa husika unazo karibu shuka na uzi, laa hujiamini chagua kona ya kukata.
____MADA____
wewe ni mfanyakazi mwenye fani aidha iwe ni Daktari, Fundi umeme, Muhasibu ilimradi una utaalamu flani.
Ukafika wakati nchi yako imetangaza state of emergency na siku chache badae nchi yako ikaingia vitani.
Kupitia amri ya mkuu wa nchi unateuliwe ufatane na briged za jeshi kufuatia utaalamu wako.
Kwa bahati mbaya vita inaisha uwepo wako kikosini unaleta utata, idadi kubwa ya wanajeshi uliokuanao wanatoa ushuhuda kwamba walikuona umeripukiwa na Bom na hivyo wewe ni RIP ! Idadi ndogo ya wanajeshi wana'declear kutokuwa na uhakika which is which.
Kumbe wewe ukweli wa mambo umetekwa nyara na majeshi pinzani.
Jeshi pinzani linaku'hold takriban kwa miaka 10. Huku nyuma umeacha mke na watoto wawili.
Wanajeshi wa nchi waliporejea pale vita imeisha walikuja na taarifa kwamba wewe ulikufa.
Ambapo baada ya mwaka 1 wa maombolezo mkeo alipitia taratibu zote za kisheria kuhusu kifo chako na akaolewa na mwanaume mwingine (Ndoa iliopitia taratibu zote za kisheria kama ulivyooa wewe).
Baada ya miaka 10 kupita wewe unaachiliwa, unafika kwako unakuta mkeo ameolewa na ana mtoto mmoja.
Haya yamekutokea wewe Great Thinker Unafanyaje ?
 
Namweleza mke wangu ukweli kuhusu kupotea kwangu,then nampa choice huku nikiwa tayari kwa maamuzi yoyote atakayoamua! Kwani hata kumkuta akiwa hai ni Mungu tu
 
Atakuwa mke wa jamaa aliyeoa kwa mara ya pili na kutokana na taarifa zilizokuja mwanzo kuwa mume wa kwanza ameRIP ni haki ya huyo mke kuwa na mme mpya!
 
mkuu kwa masharti pale juu ngoja nijitose!
Kushikiliwa kwangu kwa miaka 10 kutakuwa kumebadilisha maisha na fikra zangu'yule mke wangu ni halali kwa yule niliyemkuta naye'nitawaheshimu na nitachukua wale watoto na kuishi nao
 
Kisheria ni mke wa huyo mume wake mpya sababu wewe umesha andikiwa kama umefariki.
In fact katika database ya serikali wewe ni deceased tayari na umetolewa katika idadi ya population.
Kitu cha kwanza, anza upya registration, nenda kortini upewe tena identity mpya, na kama kuoa anza upya tena kuandikisha ndoa.
Kama utamtaka huyo huyo mke basi anza kumtongoza upya, vunja ndoa yake na huyo mume wake, wafanye divorce kortini, alafu na wewe umuoe mpya.
 
Naomba muongozo,kwani grita sinka yukoje? Maana naona jibu hata mie nalijua sasa nata kupata mwongozo.
 
Ukizingatia what you went through huko ulikotekwa nyara, sidhani kama hata ni sahihi kuanza kujirudisha kwa mkeo. Umeshakuwa mtu tofauti, na pengine it won't work anymore. Nadhani ni busara kujaribu kutengeneza bond na mwanao bila kuingilia ndoa ya mkeo na kuwaacha waendelee na maisha yao. Unaweza kulazimishia na mwisho mkeo asikupende kwa sababu ya psychological state uliyonayo (kwanza huo ukali hapo inaonekana umedata)
NOTE: this was the best novel ever, naskia movie yake ilitoka ila haijanipitia. Wish to get it...
 
kwenye hii movie, kwangu imefikia ndo wametangaza emejensi, so bado sijaenda vitani

ngoja waje walotekwa wajibu.

Mukubwa ! Mkuu wa kitengo cha "kuwa-bandua lebo" pole na kazi na lebo za chuma pia wabandua ? (naruhusiwa kuchakuchua mi kwa nafasi yangu kama thread creater na Kongosho kwa nafasi yake ya ukuu wa kitengo cha lebo )
 
Hili wala halina utata wowote kwani mtu keshakufa kila kitu chako kaondoka nacho. Kilichobaki kina wenyewe.

Kwani marehemu huwa ana nafasi ya kudai fidia??

Jamaa awalaumu waliotangaza kifo chaka na kutoa ushuhuda kwamba ame R.I.P!!
 
mkuu kwa masharti pale juu ngoja nijitose!
Kushikiliwa kwangu kwa miaka 10 kutakuwa kumebadilisha maisha na fikra zangu'yule mke wangu ni halali kwa yule niliyemkuta naye'nitawaheshimu na nitachukua wale watoto na kuishi nao

Like !
 
Umekuja na mkwara utafikiri ni mada inayoumiza kichwa....eti Great Thinkers tu ndio wachangie :lol: :lol:
 
Naomba muongozo,kwani grita sinka yukoje? Maana naona jibu hata mie nalijua sasa nata kupata mwongozo.

KK magreti sinka vigezo :
> Hawatukani
> Hawajibishani matusi.
> Wapandwapo jazba ikabidi watumie maneno makali, basi huyazimua kwa kuyaweka katika lugha ya stara.
> Hawana quick tempar
> Hoja zenye mashiko, weledi , busara na hekima ndiyo silka zao.
 
Nimetanguliza ANGALIZO kwamba ni Great Thinkers Membar, ndiyo ningeomba wanichangie katika agenda hii mezani.
Mizaha, Utani, Kubeza, Mas'khara, Uchakachuaji wa Thread ni vitu viendeleavyo kukua hapa Kijijini kwetu siku baada ya siku.
Ukishajiyakinisha sifa tajwa husika unazo karibu shuka na
uzi, laa hujiamini chagua kona ya kukata.
____MADA____
wewe ni mfanyakazi mwenye fani aidha iwe ni Daktari, Fundi umeme, Muhasibu ilimradi una utaalamu flani.
Ukafika wakati nchi yako imetangaza state of emergency na siku chache badae nchi yako ikaingia vitani.
Kupitia amri ya mkuu wa nchi unateuliwe ufatane na briged
za jeshi kufuatia utaalamu wako.
Kwa bahati mbaya vita inaisha uwepo wako kikosini unaleta utata, idadi kubwa ya wanajeshi uliokuanao wanatoa ushuhuda kwamba walikuona umeripukiwa na
Bom na hivyo wewe ni RIP ! Idadi ndogo ya wanajeshi wana'declear kutokuwa na uhakika which is which.
Kumbe wewe ukweli wa mambo umetekwa nyara na majeshi pinzani.
Jeshi pinzani linaku'hold takriban kwa miaka 10. Huku nyuma umeacha mke na watoto wawili.
Wanajeshi wa nchi waliporejea pale vita imeisha walikuja na taarifa kwamba wewe ulikufa.
Ambapo baada ya mwaka 1 wa maombolezo mkeo alipitia taratibu zote za kisheria kuhusu kifo chako na akaolewa na mwanaume mwingine (Ndoa iliopitia taratibu zote za kisheria kama ulivyooa wewe).
Baada ya miaka 10 kupita wewe unaachiliwa, unafika kwako unakuta mkeo ameolewa na ana mtoto mmoja.
Haya yamekutokea wewe Great Thinker Unafanyaje ?

1: No one to blaim if is true story, ila ikiwa umetunga sichangii
2: Nowadays no one atakaa mateka without serikali
kujua, just to remind you, kuwashika mateka is a biggest pride kwa wanajeshi wa serikali husika, so huwatangaza, publicly kwa serikali pinzani, na watademand a lot, why? simple, bcoz they will get most infos of war tacs ya mpinzani wako.
 
Back
Top Bottom