Atakayevaa Vazi la Jeshi Jela Miaka 20

Babuji

Senior Member
Nov 27, 2008
197
3
RAIA yeyote atakayepatikana amevaa vazi la jeshi au linalofanana na vazi hilo atatumikia kwenda jela miaka 20.

Rai hiyo imetolewa mjini Dodoma Bungeni na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Hussein Mwinyi wakati alipokuwa anafafanua juu ya kufuata sheria ya mavazi hayo kwa wananchi.

Mwinyi alisema kuwa kuanzia sasa mtu yeyote ambaye ni raia wa Tanzania atakayeonekana amevaa vazi la Jeshi la Wananchi wa Tanzania [JWTZ] kiholela ambaye hausiki kwa namna moja ama nyingine na vazi hilo atatumikia kifungo cha kwenda jela miaka 20.

Source: http://www.nifahamishe.com
 
Lini sheria hii imepitishwa bungeni au ndio kuropoka kwa viongozi wetu wenyedhamana na hii wizara
 
Hawa wanaacha kazi za kulinda mipaka wanafuatilia nguo za Jeshi hawatembei nchi za wengine na kuona nguo au vazi linalofanana na jeshi ni vazi la kawaida,au wanataka mavazi ya yale Miss dunia tu,hivi mtu yuko shamba huko anapiga jembe na amevalia kaptula la kijeshi ndio wataenda kumfunga miaka 20, basi wawafunge hao mafisadi tuone kama kweli wamezamiria kuongoza Taifa hili kisheria na hakuna kulia mtu.
 
No wonder... Miafrika Ndivyo Tulivyo.... Nyani Ngabu
Mambo ya maana hatusemi miaka mingapi jela, nani kavaa nini miaka 20 haya...
 
Hiyo adhabu ya miaka 20 ni kwa faida ya nani hasa? Je, ni watu wa aina gani ni likely kukutwa na minguo hiyo, kama si akina kajamba nani na kina kanumba huko mitaani ambao minguo hiyo wanaipata pengine kama msaada au mitumba (low cost clothes)? Huyu waziri anajua fika kuwa hatokutwa Chenge au Rashidi na minguo hiyo bali mlalahoi fulani, ambaye kwao ni rahisi kumkandamiza...........!

Je, kuvaa minguo hiyo kunakera zaidi ya kujichotea mibilioni ya fedha like wht bw. Chenge & Rashid did? kipi kinakera zaidi? kipi chenye athari kubwa kwenye uchumi na maendeleo ya watz..............!! mbona haya hawayatolei matamko rasmi bungeni, say yeyote atakayekutwa na hatia ya kujichotea mihela ya public atakula shaba in public?

Sheeeeeeeeeeet........! Very tired with the current regime!!
 
Hivi vazi la jeshi la Tanzania likoje? Mimi ninafahamu lile la kijani kilichoiva kwa Army, light blue kwa Air Force, na jeupe kwa Navy. Hata hivyo nguo za rangi hiyo siyo mavazi ya kijeshi mpaka yawe na nembo ya JWTZ na bendera ya Tanzania pamoja na jina na cheo cha askari anayelivaa. Vivyo hivyo ndivyo ilivyo kwa majeshi ya nchi nyingine pia.

Vazi la kijeshi la kivita ni lile la mabakamabaka likiwa na nembo ya jeshi, pamoja na bendera ya nchi na jina na cheo cha askari aliyelivaa; kwa mfano vazi la kivita la jeshi la Marekani ni kama ifuatavyo:
Army_Combat_Uniform.jpg

Nguo ya mabakamabaka bila kuwa na nembo ya jeshi, na bendera ya Taifa hata bila kuwa na jina wala cheo cha askari siyo uniform ya jeshi. Ni nguo inayoweza kutumika na mtu yeyote yule anayefanya shughuli za porini kama vile uwindaji na camping.

Angalia yanavyoweza kutumika:

3A.-John-Kerry-proves-his-Crockett-in-Chief-creds-during-the-2004-reelection.-739205.jpg

Mgombea Urais wa Marekani kwa tiketi ya Democrat mwaka 2004 akiwinda ndege​

42-18969229.jpg

Babu anamfundisha mtoto wake kuwinda swala​

ks1001.gif

Watoto wakiwa Camping​

Huyu waziri anaweza kuwa karopoka, au kama ninavyolifahamu jeshi letu huenda linataka kuhodhi aina fulani ya mavazi ikiwa ni pamoja na zile safety boots (MABUTI). Ngoja tuone shria hiyo itakuwaje​
 
Fulana ya kijani nayo imo? Wanajeshi wanavaa fulana za kijani, sasa hiyo nayo inahusika au?

Watuambie kabisa ikibidi hata zile tulizowatumia kina mamie kwani Msola baada ya kupewa zawadi misheni tuzirudishe kwa wenyewe wamisheni.

Wengine hatutaki tabu na wanajeshi, pande za Mjimwema tushapata dhahma tosha!
 
Hivi vazi la jeshi la Tanzania likoje? Mimi ninafahamu lile la kijani kilichoiva kwa Army, light blue kwa Air Force, na jeupe kwa Navy. Hata hivyo nguo za rangi hiyo siyo vazi la kijeshi mpaka ziwe na nembo ya JWTZ na bendera ya Tanzania pamoja na jina na cheo cha askari anayelivaa. Vivyo hivyo ndivyo ilivyo kwa majeshi ya nchi nyingine pia.

Vazi le kijeshi kivita ni lile la mabakamabaka likiwa na nembo ya jeshi, pamoja na bendera ya nchi na jina na cheo cha askari aliyelivaa; kwa mfano vazi la kivita la jeshi la Marekani ni kama ifuatavyo:
Army_Combat_Uniform.jpg

Nguo ya mabakamabaka bila kuwa na nembo ya jeshi, na bendera ya Taifa hata bila kuwa na jina wala cheo cha askari siyo uniform ya jeshi. Ni nguo inayoweza kutumika na mtu yeyote yule anayefanya shughuli za porini kama vile uwindaji na camping.

Angalia yanavyoweza kutumika:

3A.-John-Kerry-proves-his-Crockett-in-Chief-creds-during-the-2004-reelection.-739205.jpg

Mgombea Urais wa Marekani kwa tiketi ya Democrat mwaka 2004 akiwinda ndege​

42-18969229.jpg

Babu anamfundisha mtoto wake kuwinda swala​

ks1001.gif

Watoto wakiwa Camping
Huyu waziri anaweza kuwa karopoka, au kama ninavyolifahamu jeshi letu huenda linataka kuhodhi aina fulani ya mavazi ikiwa ni pamoja na zile safety boots (MABUTI). Ngoja tuone shria hiyo itakuwaje​

Huyu Mwinyi anayajua anazijua tofauti hizo?
 
Kweli Tanzania bado kuna sheria za mwaka 47!!! Hivi huyu hajui kama nchi za nje watu wanaruhusiwa kuvaa nguo hizo bila matatizo yeyote!!? Kwanini tunataka kujifanya sisi kama kisiwa katika dunia hii na kuwa na sheria za ajabu ajabu!? Hii ni sheria ya uonevu ambayo imepitwa na wakati. Mafisadi wanaokupua mabilioni ya walipa kodi mnashindwa kuwafunga na kuwaacha waendelee kupeta bungeni na mtaani na wengine ni bado vingunge kwenye mashirika ya umma (Idrisa Rashid wa TANESCO, Edward Hosea wa PCCB na Mwanasheria Mkuu) lakini mlalahoi akijivalia hizo nguo za jeshi basi atafungwa miaka 20!!!! Aibu tupu!!!! :(
 
Hivi huko uraiani mtu atapataje vazi la jeshi bila mwanajeshi kuhusika kwa namna moja au nyingine? Au anamaanisha vazi lolote lenye mabakamabaka!
 
Hili suala limekuwepo kwa muda mrefu, idadi ya walalahoi wanaonyang'anywa mabuti, mabegi, mashati, pensi na suruali zao ni mitaani na wajeshi ni kubwa! Hawa jamaa kitu chochote chenye mabakabaka ni chakwao! hata kiwe na nembo ya jeshi la nchi nyingine au maandishi ya kichina ambayo hawajui hata maana yake. Dingi yangu alishatembezwa kifua wazi mitaa ya Kigamboni kwa sababu tu alikuwa kavaa kishati chake cha mtumba kinachofanana na vile vya navy! Mi binafsi nshang'ang'aniwa na mjeshi pale Ubungo kwa kuwa nilikuwa na begi linalofanana na la jeshi lakini nikamtoka kiaina!
Cha kushangaza ni kwamba hivi vitu vinauzwa madukani na vinaingizwa nchini kihalali, kama serekali haitaki wananchi wa kawaida wavitumie kwanini wasiwabane wanaoviingiza nchini? Badala yake wanasubiri walalahoi wakishavinunua ndo wanawabugudhi huko mitaani? Tena wajeshi wakishamnyang'anya mtu chochote wanakitumia wao binafsi, wala hawatoi taarifa popote! Ni vyema tukawekana wazi haswa ili kila mtu ajue 'vazi la jeshi' ni lipi na mimi kwa maoni yangu binafsi- cha muhimu kabisa na distinquishing feature ni NEMBO.
 
Mimi nionavyo ni kwamba bado sisi watu weusi tuna matatizo.

Kama ikiwezekana mavazi hayo yapigwe marufuku kuingizwa TZ. Ni juzijuzi nilikuwa nakifikiria kununua moja ya koti la baridi liuzwalo paundi za bibi karibu 60 na ni koti zuru kwelikweli.

Sasa sijui itakuwaje na hizi sheria za ajabuajabu!
 
Na wewe koti la baridi la nini Tanzania?
 
RAIA yeyote atakayepatikana amevaa vazi la jeshi au linalofanana na vazi hilo atatumikia kwenda jela miaka 20.

Rai hiyo imetolewa mjini Dodoma Bungeni na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Hussein Mwinyi wakati alipokuwa anafafanua juu ya kufuata sheria ya mavazi hayo kwa wananchi.

Mwinyi alisema kuwa kuanzia sasa mtu yeyote ambaye ni raia wa Tanzania atakayeonekana amevaa vazi la Jeshi la Wananchi wa Tanzania [JWTZ] kiholela ambaye hausiki kwa namna moja ama nyingine na vazi hilo atatumikia kifungo cha kwenda jela miaka 20.

Source: http://www.nifahamishe.com

...Pheeeewwww! ..."Raia" mtakoma!!! ...kama alivyovaa mjapani huyu, heri yao wenye "nondo" za Obama na Malkia...

.........kwi kwi kwi yaani Nyani akiingia bongo na mavazi yake ya mabaka mabaka mswano tu...........

Hahahahahaaaa......oh yeah...yaani ni full kujiachia na ma-camouflage....

Nilikwambia utafute bi kizee wa kizungu lakini hadi leo bado unauweka usiku...shauri lako
 
Kujifanya mwanajeshi wa JWTZ wakati sio kweli ni kosa la jinai. Sheria kama hiyo iko kila nchi.

Kuvaa nguo zinazofanana na za mwanajeshi wa JWTZ haitakiwi itoshe kuwa kosa. Huku ni kukaliana vichwani. Kwanza ni "mfanano kiasi gani" ndio utatosheleza sheria ya "kufanana"? What sort of a country would send its citizens to jail for 20 years on such a subjective thing?

Waziri anayetaka kusisitiza sheria kama hii ya kuwafunga raia kwa miaka 20 kwa sababu ndogo kama za fashion ni waziri wa namna gani? Huyo Mwinyi ana akili ya kutosha kuwa waziri kweli au ameteuliwa tu kwa vile ni mtoto wa Rais aliyepita?

Tuache ujinga wa kutaka kupita mitaani tukiangalia kama wananchi wamevaa kama wanajeshi au hapana. Badala yake, tupite tukiangalia ni kiongozi wepi wanauza nchi kwa vipande 30 vya shaba.
 
Back
Top Bottom