Atakayeshika dola egypt ikiwa mubarak ataachia ngazi leo

Ng'wamagigisi

Member
Jan 3, 2011
35
1
Wa-Egypt wanaita siku ya leo kuwa ni "Mubarak Departure Day". Lakini sielewi kama kuna mtu ambaye amekubalika na wananchi, wapinzani wote au bunge (kama lipo na lina uwezo) kushika dola!! Ikiwa hayo makubaliano hayapo ni nani atakayeshika dola?!!

Nafahamu kuwa Mohamed ElBaradei anapendelewa na vyombo vya habari vingi hasa vya magharibi, lakini pia yaelekea jeshi linapewa nafasi kubwa na kuonekana ndio lifaalo kushika dola mpaka hapo utakapofanyika uchaguzi.

Wanajeshi kama Lietenant General Omar Suleiman (current VP), Air Marshal Ahmed Shafiq (current PM), Lieutenant General Sami Annan na Field Marshal Mohamed Hussein Tantawi ni wanajeshi wenyenguvu sana na wanaweza kuamua kuwa kwa sababu jeshi, ambalo lasemekana ndio taasisi pekee ambayo haijaharibiwa na rushwa na ufisadi, likashika dola mpaka hapo utakapofanyika uchaguzi. Kwa upande mwingine iwapo jeshi likishika dola kunaweza kuwa na tatizo kwani mahusiano kati ya jeshi la Egypt na Muslim Brotherhood si mazuri.

Lakini pia kuna tetesi ya kamati ya wazee (inayosemeka kuwa na mkono mkubwa wa Marekani) inaandaliwa kushika dola mpaka baada ya uchaguzi.

Hapo ndipo kazi ilipo iwapo Mubarak ataachia ngazi leo au siku za karibuni bila makubaliano rasmi na wawakilishi wa makundi yote hapo Egypt. Wana-jf mnamawazo gani kuhusu utawala wa Egypt iwapo Mubarak ataachia ngazi leo au kesho??!!!
 
hilo nalo ni neno la kutazama, ngoja tusubiri wapevu wa midle east affairs
 
Back
Top Bottom