Atakaye kujua.......

Tausi Mzalendo

JF-Expert Member
May 23, 2010
1,471
722
wabongo ni watu gani? Ukisoma mada kadhaa humu JF utaona watu wanasema "nyie wabongo"....ina maana gani? Nilikuwa nafikiri wabongo ni watanzania huenda siko sahihi? Na je watanzania wanaoishi nje ya Tanzania wao siyo watanzania?...nimetoka kusoma mada moja imeandikwa na "Ndevu mbili" na humo kumejaa msemo huu wa "nyie wabongo" nikaona nitafute tafsri sahihi isije ikawa niko nyuma kiufahamu.

Nijuzeni nipate kufahamu.
 
Mimi navyo jua jina la bongo lilitokana,tz maisha ni ya tabu kwa hiyo ili uweze kumudu inabidi
utumie ubongo(bongo)
Kwa hiyo badala ya kuita tz,tunaita bongo.
Ukiwa nje ya nchi unakuja tz unasema naenda bongo.
Hivyo wabongo ni wa tz
 
mi nijuavyo bongo ni jiji la dar,maana hapa dar bila kichwa kufanya kazi utalala njaa,kuibiwa,kutapeliwa ilimradi ni vurugu tu,
 
Ukiwa kule kwetu Umasaini, Bongo ni DSM tu,
Na ukiwa nje ya Tanzania Bongo pia ni Dsm, ndo maana huwezi kua kwenu kishumundu halafu mtu alieko USA, UK, n.k akakupigia na kukuliza ''habari za bongo''.
Tukija kwenye watu ukiwa nje ya nchi, so long umetokea DSM we ni m'bongo tu, labda ubadilishe uraia,
ila kwa kua kule abroad tunatambuana kwa nchi, ndo ukikaa na wa-nchi nyingine unajiita M-Tz.
 
Back
Top Bottom