Ataka ndoa ivunjwe baada ya kubaini mkewe ni kikongwe

ndoa yake ivunjwe kwa madai kuwa amebaini mkewe ni kikongwe

halafu

baada ya miaka minane aligundua kuwa mkewe hakuwa kigori na kwamba alishazaa na tayari ana wajukuu watano

Haya maneno mawili yanawakilisha nini katika habari hii "Kikongwe" na "Kigori"?
 
Jamaa ana pointi mazee hata kama ni ndoa ya Kanisani, kama kulikuwa na Mambo ambayo (kama yangewekwa wazi yangepelekea pande moja kukataa ndoa) hayakuwekwa wazi basi hiyo ndoa ni void yaani haikuwahi kufungwa ( kwa maana ndoa hufungwa na Mungu na si padre wala mchungaji na huwezi kumdanganya Mungu)
 
Na hiki ndicho kinachowafunga wengi. Hivi waliokitengeneza hawakuweza kuforesee jamani? Mbon awengi wanaumia na haya maneno 3 tu? ah

we wacha tu, mie hayo maneno ma3 ukichanganya na wale wapiga vigelegele wa cku ile, nikikumbuka mie hoi.
 
Nyoni aliiambia mahakama hiyo kuwa mwanamke huyo, ambaye alimuoa mwaka 2002, alimweleza wakati wanakutana kwa mara ya kwanza kuwa yeye bado ni mbichi na hakuwahi kuzaa. Mume huyo alidai kuwa baada ya miaka minane aligundua kuwa mkewe hakuwa kigori na kwamba alishazaa na tayari ana wajukuu watano na hivyo akaamua kuachana naye.

Duh hii kali! Haya ndio matatizo ya kuwa na papara katika kutafuta mwenza.
 
Jamani mkataba wa Richmond na Tenesco ulivunjwa kwasababu kubwa kuwa Richmond walikiuka sheria za mikataba kwa kudangaya kuwa wana uwezo wa kuzalisha umeme jambo ambalo halikuwa kweli. Na hapa mi naona hakimu atumie uzoefu wa Richmond, kwani sheria za mahakama zinaruhusu kutumia uzoefu au hukumu ya kesi inayofanana hii inayoamuliwa.
 
Hodi hodi wanajamiiforums. Mimi ni mgeni jamani, naomba kuwa nanyi...

kwanza nampa pole huyo kaka kwa kujikuta akiingia mkenge kwa kikongwe na kuamua kufunga ndoa.

Pamoja na hayo inaonyesha kuwa huyo kaka alikuwa akimtegemea huyo kikongwe kiuchumi sasa ameimalika kiuchumi anatafuta yule ampendaye na kikongwe kaamua kumbana ndo maana analazimika kukimbilia mahakamani.

kutokana na hali hiyo vijana wengi wa kiume wanaopenda kulelewa na wamama wenye mipesa yao wawe makini na hilo wasijikute nao wanatangaza ndoa na hatimaye kuzifunga kwa kushawishiwa na pesa.

mwanamke mwenye watoto hadi wajukuu anajulikana tu hata kwa sura jamani .

kaka oleeeeeeeeeee
 
Huyu Nyoni ni kwamba alikuwa hawajui wakina dada wa kichagga mmachame au? wengi wana katabia ka kudanganya umri hata kama amekuzidi miaka 20 hawaoni shida kwani target yao ni wewe kumweka ndani. Huyu mwanammke naye ajifunze hasara za udanganyifu.
 
Hodi hodi wanajamiiforums. Mimi ni mgeni jamani, naomba kuwa nanyi...

kwanza nampa pole huyo kaka kwa kujikuta akiingia mkenge kwa kikongwe na kuamua kufunga ndoa.

Pamoja na hayo inaonyesha kuwa huyo kaka alikuwa akimtegemea huyo kikongwe kiuchumi sasa ameimalika kiuchumi anatafuta yule ampendaye na kikongwe kaamua kumbana ndo maana analazimika kukimbilia mahakamani.

kutokana na hali hiyo vijana wengi wa kiume wanaopenda kulelewa na wamama wenye mipesa yao wawe makini na hilo wasijikute nao wanatangaza ndoa na hatimaye kuzifunga kwa kushawishiwa na pesa.

mwanamke mwenye watoto hadi wajukuu anajulikana tu hata kwa sura jamani .

kaka oleeeeeeeeeee
karibu JF naomba jinsia yako tafadhali:hug:
 
Back
Top Bottom