Assume we ndo nahodha!

Jaguar

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
3,438
1,026
Jamaa mmoja akiwa na mizigo mingi bandarini dar,alikodi boti zima kuelekea Zanzibar.Safari ilianza vizuri tu,lakini walipofika katikati ya bahari,jamaa akaamuru boti isimame kidogo.Kwa mshangao wa nahodha,yule jamaa akaanza kutupa kitu kimoja baada ya kingine(magunia ya mchele,sukari,mafuta ya kupikia n.k) baharini akidai ndo kafika mwisho wa safari.Wakati nahodha akiwa mdomo wazi,yule jamaa akamwambia;'nisubiri nikakuchukulie pesa yako ya nauli nyumbani kwangu,nitarudi baada ya dakika 3,kisha akajitosa na kuzama baharini.Ungekuwa wewe ndo nahodha ungefanyaje?ungesubiri pesa yako au ndo spidi 240 kurudi bara?
 
He he he bora usubiri uchukue chako.hawa ndo wale,ukikimbiza boti unashangaa gafla anatokea pembeni yako kimiujiza
 
hapo ni spidi anaweza kurudi na wenzake wanakwambia 'aise tuna njaa hatujala hata breakfast' ikala kwako!
 
Maaaweeeee!!!!?? Yani hapo kama ni mimi spidi ntakayotoka nayo hapo hata yeye atacheka lazima.
 
Mi ntamwambia ckuamini nshawah kuibiwa hvyohvyo so twende wote (sijui mguu kwa mguu au mbizi kwa mbizi)
 
Kwa sisi manahodha tunafundishwa kutumia logic na kutopanic unapokutwa na lolote usilolitegemea,liwe la kawaida au la kutisha. Sasa kwa hapo jiulize swali moja, kama ameweza kudumbukia baharini anakodai ni kwao,atashindwa nini kukuunganishia ukimkimbia kama ana shida na wewe? Hapo ni kumsubiri tu, sijui atatoka na hela ya nchi gani teh teh teh teh toh toh.
 
mie hata boti ntaona itanichelewesha, ntakimbia kwa miguu yangu mwenyeweeee...hahahaaa
 
Kwa sisi manahodha tunafundishwa kutumia logic na kutopanic unapokutwa na lolote usilolitegemea,liwe la kawaida au la kutisha. Sasa kwa hapo jiulize swali moja, kama ameweza kudumbukia baharini anakodai ni kwao,atashindwa nini kukuunganishia ukimkimbia kama ana shida na wewe? Hapo ni kumsubiri tu, sijui atatoka na hela ya nchi gani teh teh teh teh toh toh.
Nimeipenda hii mkuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom