Assist difficulties with web browser.

Loloo

JF-Expert Member
Apr 9, 2011
214
54
Wakuu habari zenu; Jamani naombeni msaada for the past two month napata shida sana kufungua official mail yangu ya yahoo.Ilikuwa ivi,niliwazima mtu laptop katia kufanya kazi zake akaremove firefox,nilivyokuja kuinstall upya hapo ndo matatizo yalipoanza ,maisl nashinwa kuacess ila other activies kwenye website nyingine zinafanyika nikawa nafungua through access mode,for two weeks imekubali sasa ndo imegoma kabisa,IE ndo kabisa nikanza tu kutype mail off it goes,natumaini nimeeleweka kiasi flanni naombeni saada please!
 
tatizo ni geni ila jaribu mambo haya

1. Clear cookies na cache

2. Maybe kuna ads on zinazoblock mail yako jaribu kutumia opera browser (ina less ads on) na uangalie tatizo litaendelea? Kama opera hapatwi na hilo tatizo then nenda kwenye ads on (plugins) jaribu kuangalia zisizo na maana zi disable zote.
 
Itabidi nijaribu manake frankly speaking nimezoea IE na FF
 
Itabidi nijaribu manake frankly speaking nimezoea IE na FF

Hilo tatizo lipo sana, sasa cha kufanya ni kuingia kwa kupitia client nyingine. Pakua 'yahoo Messenger', kisha isanikishe kwenye dadavuzi mpakato yako. Kwa hiyo utakuwa una ingia yahoo kupitia hii Messenger, utakapo kuwa hapo utabofya kitufe cha 'mail' ambacho kitafungua kivinjari chaguo msingi chako (IE au MF). Njia hii nimeithibitisha na naamini hautakuwa na tatizo tena.

lete mlisho-nyuma kama utajaribu.
 
Nashukuru sana ila nakuomba kama hutajali unieleweshe kwa kutumia IT terms au kingereza cha kawaida samahani sana lakini
 
Nashukuru sana ila nakuomba kama hutajali unieleweshe kwa kutumia IT terms au kingereza cha kawaida samahani sana lakini

kuingia = sign in
dadavuzi mpakato = laptop
kitufe = button
sanikisha = install
kivinjari = browser
chaguo msingi = default
mlisho-nyuma = feedback
pakua = download
bofya = click

Kiswahili ni kitamu kama ziwa la mama, alisema Shaaban Robert! Karibu
 
Back
Top Bottom