Askofu Valentine Mokiwa wa Anglican

Stuxnet

JF-Expert Member
Feb 12, 2011
10,337
17,860
Wadau naomba munijuze CV ya huyu askofu mkuu wa kanisa la Kianglikana nchini kwani namuona kama anaeitst religious dictator. Ukienda Dodoma kuna fukuto Kati ya pande mbili zinazotofautiana kiitikadi. Huko Ukonga analazimisha waumini waongozwe na mchungaji waliyemkataa. Juzi kule Arusha amemsimika Askofu Stanley Hotay ambaye licha ya waumini kumkataa lakini vilevile Mahakama kuu imeweka pingamizi.

Ingawa Mimi si muanglikana lakini kama mkristu naguswa na utendaji wa kibabe wa huyu mtu anayeitwa Dr Valentine Mokiwa. Wadau naomba michango yenu
 
Huna CV yake (which means humfahamu) tayari umeshamhukumu kuwa ni "mbabe"? Japo kunawezekana kukawa na hoja ukonga -and I am not sure on that- lakini kwa Arusha umepotosha ukweli. Unataka kutuambia waumini WATATU waliofungua kesi ndio wanakufanya uamini askofu hatakiwi na waumini? Hao ni percent ngapi ya waumini wote?
 
Naomba mtoboasiri unijibu tu kwa upole kwa vile mimi si mwelewa wa mazingira ya kanisa la anglikana Ila nimeguswa tu na vuguvugu hili ambalo sikuliona kwa watangulizi wake Kama Askofu John Ramadhani au Mtetemela kakukuwa na tensions kama hizi. Kanisa la kianglikana Tanzania linaweza kupotea katika ramani ya imani za kikiristo kama hatua madhubuti za dialogue na reconcilition hazitafanyika
 
Sijawa mkali ndugu yangu! Nimetoa tu maoni yangu juu ya conclusion yako kuwa Dr Mokiwa ni mbabe. Binafsi namfahamu kiasi tangu akiwa chaplain wa UDSM, ni Msomi mwenye msimamo na hayumbishwi kirahisi. Mgogoro wa Dodoma kaukuta. Ila migogoro iliyopo si Anglican tu Bali na makanisa mengine chanzo ni fedha tu.
 
Asante Bwana Mtoboasiri kwa kuliweka sawa
 
Wakati nipo mlimani (udsm) miaka ya 95 alikuwa Pastor pale kanisani mlimani karibu na Hall 4. Wakati huo alikuwa anahubiri kwa uchangamfu sana na niliona anapendwa zaidi na vijana zaidi kutokana na maneno yake. Thats what i remember about him. Nilipomsikia baadae nilliona kama alipanda haraka sana kuwa Askofu na hatimaye Askofu Mkuu. Japo sijui background yake ya elimu, lakini kwa kumsikiliza akihubiri nilikuwa na judgement kwamba huyu mtu ana 'akili'.
 
Napenda kusema askofu Mokiwa kwa hili kakosea la kuamua kumsimika askofu ambae mahakama imezuia,na leo katumiwa hati ya kukamatwa kwa kuingilia amri ya mahakama. Cha kujiuliza ni kwa nn kanisa la Anglican kuna migogro kila kukicha hasa linapokuja suala la madaraka. Tuangalie kanisa katoliki,hakujawahi na haitokaa itokee askofu akataliwe kusimikwa kwa vile utaratibu wao ni mzuri,askofu ana teuliwa na papa na kusimikwa na Cardinali akisaidiwa na maaskofu wenzie,(askofu mahalia andie anatuma majina kwa papa kwa mtu anaemwona anafa kuwa askofu papa ndie huteuwa.Sasa kwa angilcan naona kuna maslahi ya watu wachache na ndio hao waliofungua shtaka la zuio mahakamani. Sii kazi yangu kuingilia kazi ya mahakama ila kwa sasa ifike wakati masuala ya kanisa yaamuliwe na kanisa lenyewe.Wana askofu mkuu wao cantebury kwa nn asitumike kutuewa ikawa ndio mwisho kuliko kuwaachia watu wapige kura huku wakiangalia maslahi yao wenyewe? Nawashauri kanisa la Anglican wainge mfano wa kanisa mama Katoliki na ndiko walikoanzia.
 
Tatizo hili na yote haya ni Dr Mbena anayetaka kuongoza watu ambao hawajamchagua! Mokiwa, Hotay wote wako sawa, halafu jaribu kuchukua picha za watu watatu walioweka pingamizi, hakika utajionea maajabu na utajua tu kuna watu wako nyuma yao,wanatia huruma
 
Napenda kusema askofu Mokiwa kwa hili kakosea la kuamua kumsimika. Nawashauri kanisa la Anglican wainge mfano wa kanisa mama Katoliki na ndiko walikoanzia.
Mkuu na mimi nakuunga mkono kwa kuwa katika elimu ya bureaucracy inaaminika kuwa kuna bureaucracy mbili tu duniani zilizofanikiwa. Ya kwanza ni ya Kanisa Katoliki kwa kuwa mfumo unatoka kwa muumini unakwenda kwa Paroko, baada ya hapo unakwenda kwa Askofu na juu kabisa kuna Papa,Bureaucracy ya pili kwa ubora ni ya Jeshi kwani amri inapotoka juu inapokwenda chini ni kwa ajili ya utekelezaji tu na hakuna kudadisi.
 
Uwe na amani juu ya Askofu Dr. Mokiwa. Ni shetani tu anavuruga kazi ya Mungu. Mbona migogoro iko madhehebu karibu yote siku hizi? Injili ya Kristo inahubiriwa sana siku hizi na shetani hataki hili. Anataka watu wahangaike na kesi waache mambo ya msingi ya kuhubiri injili. Dr. hana tatizo lolote. Ila kazi ya Mungu lazima isonge mbele.
Naomba mtoboasiri unijibu tu kwa upole kwa vile mimi si mwelewa wa mazingira ya kanisa la anglikana Ila nimeguswa tu na vuguvugu hili ambalo sikuliona kwa watangulizi wake Kama Askofu John Ramadhani au Mtetemela kakukuwa na tensions kama hizi. Kanisa la kianglikana Tanzania linaweza kupotea katika ramani ya imani za kikiristo kama hatua madhubuti za dialogue na reconcilition hazitafanyika
 
Napenda kusema askofu Mokiwa kwa hili kakosea la kuamua kumsimika askofu ambae mahakama imezuia,na leo katumiwa hati ya kukamatwa kwa kuingilia amri ya mahakama. Cha kujiuliza ni kwa nn kanisa la Anglican kuna migogro kila kukicha hasa linapokuja suala la madaraka. Tuangalie kanisa katoliki,hakujawahi na haitokaa itokee askofu akataliwe kusimikwa kwa vile utaratibu wao ni mzuri,askofu ana teuliwa na papa na kusimikwa na Cardinali akisaidiwa na maaskofu wenzie,(askofu mahalia andie anatuma majina kwa papa kwa mtu anaemwona anafa kuwa askofu papa ndie huteuwa.Sasa kwa angilcan naona kuna maslahi ya watu wachache na ndio hao waliofungua shtaka la zuio mahakamani. Sii kazi yangu kuingilia kazi ya mahakama ila kwa sasa ifike wakati masuala ya kanisa yaamuliwe na kanisa lenyewe.Wana askofu mkuu wao cantebury kwa nn asitumike kutuewa ikawa ndio mwisho kuliko kuwaachia watu wapige kura huku wakiangalia maslahi yao wenyewe? Nawashauri kanisa la Anglican wainge mfano wa kanisa mama Katoliki na ndiko walikoanzia.

Mfumo wa uchaguzi wa post za Katoliki ni wa kimafia zaidi kuna usiri mkubwa sana. I ma Catholic n will die like that n proud to be one ila siamini katika papa mzungu huko Roma kutuchagulia askofu wetu, I am nt mjuzi wa masuala kanisa so kurekebeshwa I am ready, maana nasikia ni maombi sijui yanafunua or ni ujasusi unatumika. Better mm kama mlei niitwe kwenye mkutano wa kupiga kura ya kumchagua askofu wangu! coz tunaishi naye twamuona na akili zetu zitatusaidia.
 
Huna CV yake (which means humfahamu) tayari umeshamhukumu kuwa ni "mbabe"? Japo kunawezekana kukawa na hoja ukonga -and I am not sure on that- lakini kwa Arusha umepotosha ukweli. Unataka kutuambia waumini WATATU waliofungua kesi ndio wanakufanya uamini askofu hatakiwi na waumini? Hao ni percent ngapi ya waumini wote?
Yuko wapi Askofu king'ang'anizi Mokiwa ?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom