Askofu Tibanenason aunga mkono Rais kusaini Muswada wa Marekebisha ya Katiba 2011

Nadhani bila kujali imani ya kila mmoja wetu,suala la kupata katiba bora ni la manufaa kwa Tanzania na vizazi vyetu. Hili litawezekana kama process yote ya kuitafuta haitakuwa ya 'kiujanja ujanja'. Baadhi ya Viongozi ni WATU HATARI.

Ni watu wenye uchu wa mali,umaarufu na madaraka. Wapo tayari kutokemea uovu ili wasiwaudhi wanaotoa hela nyingi za sadaka na michango mikubwa kwenye harambee....LORD JESUS ndivyo alivyofundisha hivi? Shame on them! ASKOFU TAPELI ATAWEZAJE KUKEMEA UTAPELI? Mwenye dhambi,shauri lenye dhambi hawezi kuliamua.

Tunaomba viongoz wa dini wafanye kaz zao za 'kuokoa roho za waovu' na si kujikomba kwa watawala na kujilimbikizia mali kutoka kwa waumini maskini wasio na hatia
 
Askofu Tibanenason wa Kanisa La Pentekoste Tanzania (KLPT) akiwa katika kutoa Tamko la Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara amesema "Sisi tunaunga mkono hatua ya Rais kusaini Muswada wa Marekebisha ya Katiba". " Rais ni kiongozi wa juu wa nchi, yeye ndiye anayeamua tufanye nini ..., ninyi mnasoma Biblia, hebu fikiri Mungu angekuja kuwaambia anataka kutunga amri 10 halafu akawaambia ataweka Usizini, Usiibe, Usiseme uongo,... Semeni, nani angekubali?

Source: Patapata ya Redio WAPO.

My take: Askofu Tibanenason, umekosea sana, umetufadhaisha wengi. Hamlielewi jambo hili, basi nyamazeni kimya kuliko kuja na kauli mbovu (siyo tata) kama hizi.

Kuipa nguvu hoja yake mfano aliotoa kwanza ni wa kiwango cha chini lakini pili hauhusiani na hoja ya msingi. Mungu ni Mungu, na wanadamu ni wanadamu. Utawala wa Mungu ni tofaut na utawala wa wanadamu. Utawala wa wanadamu unajaribu kucopy ule wa Mungu lakini bado gap ni kubwa mno. Askofu amesahau kuwa faida nyingine za Mungu kuweka amri hizo ni kurahisha utawala wa wanadamu miongoni mwao.
Pili, Askofu kasahau kuwa awali katika Biblia Mungu alitaka Israel watawaliwe na Yeye na kuongozwa Waamuzi aliowachagua Yeye. Israel baadaya miaka walitaka na wao wawe na wafalme kama mataifa mengine. Jambo hili halikumfurahisha Mwamuzi Samwel, hata alipokwenda kuomba kwa Mungu. Mungu alikubali waisraeli kuwa na mfalme wao lakini akimwambia Samwel, hawajakukataa wewe bali wamenikataa mimi, ili nisiwe mfalme juu yao. Ndipo Samwel alipomtawaza Sauli mwana wa Kishi akatawazwa kuwa mfalme wa kwanza.
Kikwete si Mungu, kama Mungu aliruhusu Israel wawe na mfalme wanayemtaka kwa kutawazwa na Samwel sembuse Kikwete, ili sisi tuwe na Rais wa haki kwa kutengeneza Katiba nzuri?

Nitarudi tena.

Hivi moses kulola anaumwa mbona this time amemtuma houseboy wake kuja kumbeba mkwrr
 
Askofu acha kumfananisha kikwete na Mungu,hayo ni mafundisho manyonge kiinjili,MUNGU HAKOSEI NA HAHITAJI USHAURI,RAIS NI BINADAMU,HUKOSEA,LAZIMA ASHAURIWE.
 
Nchi zingine watu wa dini ndio wanasukuma mabadiliko kutokea hasa wakristo lakn Tanzania ni tofauti. Asasi za kidini na dini zilizipo wanajikomba mno kwa serikali. Sasa wale wenzetu waliotoa tamko Igunga ndo usiseme wao hata wakipandishwa tu kwenye VX ya waziri mkuu utasikia kesho wanatoa tamko kuwa rais kafanya la maana kusaini muswada wa katiba.

Ikipita muda ndio tena wanaanza kusema muswada unalinda mfumo ukristo. yaani vurugu tupu. Makanisa ya kipentekoste yamekuwa chachu ya wakristo kukosa sauti ya kupigania haki kwa kuwa nyingi zao zimekuwa kama NGOs za viongozi waanzilishi. Mtu anaanzisha kanisa kwa kuanza mahubiri sokoni na magengeni, mwishowe anajenga kanisa la mabanzi na matete.

Waumini wanaongezeka kwa kuwa wametangaziwa miujiza na watu wanafikiri miujiza ndio utakatifu. Mwishowe anajenga kanisa kubwa anaanza kujitangaza. Anajipachika cheo cha askofu. Hana elimu yoyote ya dini. Hana elimu ya dunia hata diploma. Mwisho wa siku anaanza kutafuta umaarufu na nafasi ya kujulikana serikalini. Hajali wanaotoa sadaka na misaada mikubwa kanisani kwake wanazipata kwa ufisadi. Unategemea nini kwa watu kama hawa? Na ndio wanaojitangaza kwenye vyombo vya habari.

Wanatoa matamko yasiyokuwa hata na utu ya ubinadamu wala kanuni za Biblia za kutafuta haki. Wanatafuta huruma ya serikali ili mambo yao yaende kwa kuwa kanisa ni dogo na halina misuli ya kifedha na kimtandao. Sijawahi kusikia hata chuo kikuu kimejengwa na wapentekoste, wala shule ya sekondari au hospitali ya maana.

Ukiniambia Lwakatare ana St. marys hayo ni yake binafsina inawezekana hata ilikuwa ni msaada wa kujenga shule za kanisa ila kwa kuwa wako kimaslahi shule ni zake na zake daima. Unaona, wako kimaslahi zaidi ndio maana wengi wao wanashindwa kujua majukumu ya kutetea haki katika jamii ila wapo tu kuimba nyimbo za watawala ili mrija wao wa fedha utunishwe na wawe nafasi kwenye jamii.

Nawasilisha
 
Lipo tatizo la mfumo wa kiuongozi katika makanisa nalo ni wachungaji na maaskofu kuwa washauri lakini wao kukosa washauri. Kama vile ambavyo huwezi kuwa mwalimu mzuri kama hujawa mwanafunzi mzuri, ndivyo ambavyo huwezi kuwa mshauri mzuri kama hutaki kushauriwa.

Ukifiria wakati fulani unasema wangekuwa na washauri wazuri, wasingetoa matamko ya kukinza namna hii.

Wenye nafasi za kuwa karibu na hao watu washaurini japo ninyi si washauri wao.
 
Anamfananisha Mungu na JK, kweli dunia imekwisha,:A S embarassed:
 
Kwa hiyo ni Maaskofu tu kama Tibanenason ndiyo wenye tiba ya kuondokana na MfumoKristo. Hongera Askofu Tibanenason, naona hata Ritz na Njiwa leo wamekukubali, wafikishieni ujumbe Mohamed Said, FaizaFoxy, Topical na Mdondoaji - pole pole tutafika.

you've got it all wrong mate

 
Askofu Tibanenason wa Kanisa La Pentekoste Tanzania (KLPT) akiwa katika kutoa Tamko la Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara amesema "Sisi tunaunga mkono hatua ya Rais kusaini Muswada wa Marekebisha ya Katiba".

" Rais ni kiongozi wa juu wa nchi, yeye ndiye anayeamua tufanye nini ..., ninyi mnasoma Biblia, hebu fikiri Mungu angekuja kuwaambia anataka kutunga amri 10 halafu akawaambia ataweka Usizini, Usiibe, Usiseme uongo,... Semeni, nani angekubali?

Source: Patapata ya Redio WAPO.

My take: Askofu Tibanenason, umekosea sana, umetufadhaisha wengi. Hamlielewi jambo hili, basi nyamazeni kimya kuliko kuja na kauli mbovu (siyo tata) kama hizi.

Kuipa nguvu hoja yake mfano aliotoa kwanza ni wa kiwango cha chini lakini pili hauhusiani na hoja ya msingi. Mungu ni Mungu, na wanadamu ni wanadamu. Utawala wa Mungu ni tofaut na utawala wa wanadamu. Utawala wa wanadamu unajaribu kucopy ule wa Mungu lakini bado gap ni kubwa mno. Askofu amesahau kuwa faida nyingine za Mungu kuweka amri hizo ni kurahisha utawala wa wanadamu miongoni mwao.

Pili, Askofu kasahau kuwa awali katika Biblia Mungu alitaka Israel watawaliwe na Yeye na kuongozwa Waamuzi aliowachagua Yeye. Israel baadaya miaka walitaka na wao wawe na wafalme kama mataifa mengine.

Jambo hili halikumfurahisha Mwamuzi Samwel, hata alipokwenda kuomba kwa Mungu. Mungu alikubali waisraeli kuwa na mfalme wao lakini akimwambia Samwel, hawajakukataa wewe bali wamenikataa mimi, ili nisiwe mfalme juu yao. Ndipo Samwel alipomtawaza Sauli mwana wa Kishi akatawazwa kuwa mfalme wa kwanza.

Kikwete si Mungu, kama Mungu aliruhusu Israel wawe na mfalme wanayemtaka kwa kutawazwa na Samwel sembuse Kikwete, ili sisi tuwe na Rais wa haki kwa kutengeneza Katiba nzuri?

Nitarudi tena.

Tatizo nini? katumia haki yake ya msingi kueleza maoni yake wewe untoa mishipa kama vile ngili! KUMBUKA MAWAZO YAKO SIYO kwa upande mwingine. mtu asiyependa klukosolewa utamwona tu, na hata chama kisichopenda mawazo ya upande mwingine utaona tu misimamo yao huwa finally ni kuzila, kurayoti nk
 
Yani hapa JF askofu asipo support cdm anaitwa mwendawazimu, anakufuru, hakusoma, unazi umezidi na hatufiki ppte.
 
huyu askofu anadeal na madawa ya kulevya ndo maana anajikomba kwa jk ili asiumbuliwe
 
Yani hapa JF askofu asipo support cdm anaitwa mwendawazimu, anakufuru, hakusoma, unazi umezidi na hatufiki ppte.

Mkuu, usikurupuke namna hiyo. Suala la kudai katiba MPYA si la CHADEMA. Ni suala la kila mzalendo anayejua thamani ya kuwa na Katiba Mpya ya wananchi, na anajua uhusiano uliopo kati ya maisha mabovu na utawala kandamizi na Katiba ya 1977 iliyopigwa viraka 1992.
Ni hitaji lililopata sana nguvu baada ya Umma wa Watanzania kuporwa haki yao ya kujiöngoza/kujitawala nchi hii kwa kutumia Demokrasia ya Uwakilishi. Ni yule tu anayeishi nje ya nchi na hawawazii mema ndugu/jamaa zake aliowaacha Tz ndiye atakayeunga mkono yaliyotokea na yanayotokea Tanzania. Wa pili, atayeunga mkono ni yule anayefaidika na mfumo wa kidharimu na utawala kandamizi uliopo. Pia ukiwa mwoga hauishi kuusifia udharimu uliopo.

Ukiwa unaitakia mema Tanganyika na Tanzania kwa faida ya kizazi kilichopo na vijavyo, kuwa na Katiba Mpya Bora na ya wananchi si suala la kutania ama kulifanyia mzaha.

Kwenye bold, kuitwa mwendawazimu siwezi kulisemea kwanini kapewa jina hilo.

Kwamba anakufuru, kuna logic. KAMWE!! Huwezi kuufananisha utendaji kazi wa Jakaya Mrisho Kikwete na wa Mungu Mwenye enzi yote aliyeumba mbingu na nchi. Ndiyo maana hata alipotaka kulazimisha kupata msaada wa andiko kuipa nguvu hoja yake LIMEGOMA.

Kwamba hajasoma, sijui ni muktadha upi mchangiaji alomaanisha. LAKINI kama alimaanisha kusoma kwa maana ya kuangalia maandishi na kukielewa kilichoandikwa katika Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Katiba ya 2011, nasema mtumia neno hilo yuko sahihi.

Askofu Tibanenason ni muhubiri wa Injili ambayo ni Neno la Kristo iliyo KWELI. Tukimuuliza uliyoongea ndiyo Kweli, unafikiri jibu lake litakuwaje? Labda tubadilishe swali, Je! Alilofanya Kikwete, Yesu analiunga mkono? Akumbuke pia kuwa watu waliopo chini si wote wanakubaliana na madudu yaliyofanywa.
 
Back
Top Bottom