Askofu: Serikali ikaze uzi kwa mafisadi

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,721
21,778
Askofu: Serikali ikaze uzi kwa mafisadi
John Nditi, Morogoro
Daily News; Friday,December 26, 2008 @00:02



Kanisa Katoliki nchini limeitaka Serikali ya Awamu ya Nne kushika hatamu katika suala la kuongoza nchi kwa mujibu wa Katiba na mahakama kuhusika kikamilifu kusikiliza kesi za baadhi ya viongozi wanaotuhumiwa kuchota mamilioni ya fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) na waliotumia madaraka yao vibaya.

Mbali na kuitaka serikali na mahakama kusimamia wajibu wao, nao raia wametakiwa waheshimu uamuzi unaotolewa na mahakama katika masuala mbalimbali zikiwamo kesi nzito zinazoshughulikiwa kwa sasa.

Kauli hiyo ilitolewa na Mhashamu Askofu Teresphori Mkude wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, juzi wakati wa mahubiri ya ibada ya mkesha wa Sikukuu ya Krismasi iliyofanyika Kitaifa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Patris la mjini hapa.

Alisema vitendo vya ufisadi vilivyoshamiri vimewafanya Watanzania kusherehekea Sikukuu ya Krismasi wakiwa katika mawazo mazito kuhusu hatima ya taifa lao kwa kuwa neno fedha ndio msingi na ufunguo wa maisha ambapo baadhi ya watu huzitafuta bila kuzingatia maadili mazuri.

Alisema pamoja na mahakama kufanya kazi yake, serikali nayo inapaswa kushika hatamu katika suala la kuongoza nchi kwa mujibu wa Katiba na raia waheshimu uamuzi unaotolewa na mahakama katika masuala mbalimbali.

“Inasikitisha kusikia wapo baadhi ya viongozi wa serikali kujipatia fedha nyingi wakiwa watumishi wa umma na iwapo ni kweli, wahusika walijifikiria hivyo hawakuzingatia upendo wa ndugu zao Watanzania na wala hawakuwathamini,” alisema Askofu Mkude. Alisema kwa mantiki hiyo, hivi sasa fedha imekuwa ikitumika kuwaletea vyeo baadhi ya viongozi wakati wa uchaguzi kwa kutofuata njia ya maadili ya uongozi.

Alisema iwapo fedha hizo zilizochotwa na baadhi ya viongozi zingetumika kwa ajili ya kupunguza makali ya huduma za tiba katika hospitali na ujenzi wa zahanati, kuwalipia karo za shule wananchi masikini na zilizochakaa kukarabatiwa na kuboreshwa na kujengwa nyingine mpya vijijini. Kuhusu rushwa, alisema bado ni donda ndugu katika huduma nyingi kama za afya ambapo tiba ni ya kuchangia, lakini wananchi wanaendelea kudaiwa rushwa.
 
Hawa wezi wa EPA waunganishwe katika shitaka la kupanga kwa pamoja kuhujumu uchumi wa Nchi DPP chukua ushauri huu ili tukate kabisa mizizi ya wezi hawa wanaotamba na fedha za wizi.
 
Back
Top Bottom