- Thread starter
- #41
MkandaraMkuu maneno sawa kabisa kwa mtazamo wako na ndio maana mimi sikuwa Mkristu kwa sababu sikubaliani na imani hiyo..
Kwa hiyo maadam mimi sikubaliani sintopenda kumsikia Pengo akizungumzia swala linalonihusu mimi hali sikubaliani na imani yake. Nitakupa Mfano mdogo sana.. Ktk Ukristu jitu linaweza kuua hadharani likakimbilia kanisani na likapewa hifadhi tena Askofu alitoe hata ushahidi dhidi ya hilo jambazi kwa sababu limeungama.. Hii ni imani yenu na naiheshimu lakini sikubaliani nayo kabisa na ndio maana sikuwa mkristu kwa sababu naamini jambazi ni jambazi lilikimbilia kanisani litolewe na kutupwa ndani hakuna kinga kama tunavyodai JK awaondolee kinga hawa Mafisadi na huyo Pengo mwenyewe analikubali hilo.. sasa iweje yeye atake kuwapa kinga hawa jamaa hali alichosema Nape ni kwamba hawa Mafisadi wanataka kukimbilia makanisani ili wasafishwe?
Sasa basi maadam hii ni ibada ya dini yenu, sisi tutaiheshimu na mnaitumia sana kuwalinda hata wahalifu maana wamekuja kutubu lakini usiiweke hii ibada yako kuwa ya kila Mtanzania na kinga kwa hata Mafisadi ambao hawatakiwi ktk uongozi wa jamii.
Mkitaka wasafisheni na wabakie raia wa kawaida tu lakini mnapotaka kuwasafisha ili warudi kisiasa hapo mtakuwa mnaniingilia hata mimi ktk imani yangu kwamba jambazi linastahili jela tu hata kama likikimbilia msikitini litolewe na kukabidhiowa vyombo vya serikali..
Ya Kaizali aachiwe Kaizali, dini zinapoingilia ya Kaizali nina haki ya kuyapiga vita kwani hata Biblia imetukanya.. Kardinal Pengo anatakiwa kufahamu hilo
Nafikiri umejijibu mwenyewe kuwa ndiyo maana hukuwa mkristo kwa hiyo waache wakristo wawapokee wenye dhambi kama dini yao inavyoelekeza, hata kiongozi wa wakristo (Yesu) alikuja kwa kondoo waliopotea si kwa waliokundini. Halafu usitake kupotosha kuwa Pengo anataka kuwakinga mafisadi (Mkandara JF ni waelewa) anachotaka Pengo ni kuwapa toba ya dhambi kiroho si kusafisha ufisadi, kama wewe una ushahidi bado unaruhusiwa kuwafikisha mahakamani hata baada ya toba.