Askofu Mwigira hii 10,000 ya Ubatizo ni ya Nini??

.
Siku moja jioni nilikuwa naangalia trinity Tv na familia, kwa macho yangu na kwa masikio yangu nikamwona na kumsikia mwingira akiwaambia waumini wake wanawake wawe wanawasachi waume zao mifukoni wakati zimetundikwa na kuzikomba pesa zilizopo ndani, hakuishia hapo kwani aliendelea kwa kuwaambia kinamama hataki kusikia malalamishi ya mke kulalamika eti kachukuliwa mme na mfanyakazi wa ndani. Aliwashauri kama kuna mwenye mfanyakazi wa ndani mwenye mchezo wa kummendea mmewe, basi achukue kitu kizito na kumponda nacho mahali pakumuumiza.
Nikiwa katika hali hiyo ya mshangao mkuu huku yeye akiwatizama waumini wake, kwa kujigamba aliwaambia wasiogope kufanya hivyo kwani watakapofika mbinguni watamkuta yeye Mwingira na Yesu, hivyo atamwelekeza Yesu kwamba hawana shida hawa ni mimi niliwaagiza wafanye vile.
KWA HASIRA NILILAZIMISHA CHANEL IBADILISHWE KABLA YA MIMI KUTENDA DHAMBI ZA KUJITAKIA. Tukaendelea na futuhi star tv na ikatupa furaha kuliko ule upuuzi wa awali yake.
.

Mungu wangu! Yesu amaetuambia tuangalie mtu asitudanganye maana wengi watakuja kwa jina lake!
 
Back
Top Bottom