Elections 2010 Askofu Mokiwa: UCHAGUZI 2010 UTAKUWA MGUMU

Mfalme Daudi alimpofanya dhambi ya kumchukua Mke wa Uria, Mungu alimtuma Nabii Nathan akamwonye na Kumkemea, alipotoza kodi na wakusanya kodi wakawa wanakula hizo pesa za walalahoi (ufisadi) watumishi wa Mungu walimkemea kwa nguvu na kodi ikafutwa

Ujumbe mzito sana huu! Mkuu tunaomba ile avatar yako ya awali...asante!
 
Mstari unaotenganisha siasa na dini ni upi? sehemu anapoongelea mtu? cheo chake? maneno yake? kuwa kwenye chama cha siasa? au ni nini? Kama yeye ni mdau wa maendelea ya Tanzania, na anajua tatizo liko sehemu fulani, je akiongea tayari amekuwa mwanasiasa? Mbona Makamba alipokuwa na-quote quran na Biblia hatukumwita askofu au sheikh? Au ndi yale ya kusema bila kujua mtu unasema nini?
 
Ujumbe mzito sana huu! Mkuu tunaomba ile avatar yako ya awali...asante!

Hata Masheikh walipompa support J.K. Nyerere kudai uhuru walikuwa wanapiga siasa, na kwa mujibu wa serikali ya Kikoloni nao walikuwa wanakiuka sheria halali (ya serikali iliyokuwepo madarakani ya mkoloni) ya kuchanganya dini na siasa. leo Pia maaskofu (wanaosema sema habari za kura na ufisadi) na Masheikh (wanaonong'ona nong'ona OIC na mahakama Kadhi) ya kadhi kwa mujibu wa CCM wanachanganya Dini na Siasa. Sasa jiulize wadau wa CCM kwenye Mtakabari wa nchi hii watakuwa nani sasa? inaamna tuwachie akina Mbowe, Mrema, Lipumba, maalim Seif ndio wazungumzie habari za sisi watanzania wote?

Mkuu Avatar ipi hiyo?? Ile passport size yangu nina nywele ndefu? niliyopiga wakati nipo BBA 3?
 
Mkuu Avatar ipi hiyo?? Ile passport size yangu nina nywele ndefu? niliyopiga wakati nipo BBA 3?
Yeah ....Ile mzee picha ya mrembo BBA hasikiki tena sijui mafisadi wa Ngono wamemficha tayari!Wengi tulivutiwa nayo si Mkuu Masa pekeee!
 
Yeah ....Ile mzee picha ya mrembo BBA hasikiki tena sijui mafisadi wa Ngono wamemficha tayari!Wengi tulivutiwa nayo si Mkuu Masa pekeee!

Mumepewa bure Toeni bure ha ha ha kila aombaye hupewa. Umeshaipata!
 
Back
Top Bottom