Askofu Mokiwa ashitakiwa kwa kumshika makalio Mtikila

Mchungaji Christopher Mtikila, amefungua kesi katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kumshitaki Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglican Tanzania Dk. Valentino Mokiwa.Msingi wa kesi ni kwamba Askofu Mokiwa alimshika makalio Mtikila na kwamba kitendo hicho kilichotokea Juni 25 mwaka jana walipokutana maeneo ya Ilala, kimemdhalilisha.Mtikila alikuwa ameitwa na Askofu kujadili tamko la la Mtikila kwamba Kanisa la Anglican linajihusisha na ufisadi, ukiwemo wizi wa vifaa vya Hospitali ya Mission ya Millo iliyoko Ludewa mkoani Njombe.Mtikila alisema kuwa alivyoitwa na Askofu Mokiwa ili kujadili hilo alifika na wenzake watatu wa taasisi ya Liberty International Foundation na wakakaribishwa kwenye moja ya jengo la dayosisi ya St. Nicholous, usiku wa saa 03:00.Muda mfupi baada ya kikao kuanza, Askofu Mokiwa ambaye alikuwa na wenzake saba, alisimama na kuwataka wajumbe wote wakaguliwe kama kuna mtu ana kinasa sauti.-Baadaye Askofu Mokiwa nae alisimama na kuungana na wenzie kuwakagua kina Mtikila baada ya kuhakikisha mlango umefungwa.Katika upekuzi huo ndipo tuhuma hizo zilipopatikana kutokana na madai kwamba operesheni hiyo ilienda mbali zaidi ya lengo la kawaida.Wakili wa Upande wa mashtska aliiambia mahakama kuwa, "Mlalamikiwa alitangaza kuwa, kila mtu aliyekuwemo kwenye mkutano lazima apekuliwe na kwamba atakayekataa angetumia nguvu, kwa kuwa alikuwa na bastola, hakuna aliyebisha."Alisema kisha akaendelea "Mshtakiwa (Mokiwa) alianza kupenyeza mikono yake kwenye shingo kuelekea chini kisha huko chini mikono ya mlalamikiwa ilionekana waziwazi ikipapasa makalio ya mlalamikaji".Mchungaji Mtikila ameiomba Mahakama imwamuru Askofu Mokiwa alipe fidia ya shs. bilioni moja kwa kumdhalilisha.Madhara zaidi ya kitendo hicho ni pamoja na mfadhaiko, masikitiko, wasiwasi, aibu katika jamii na kupata shinikizao la damu la mara kwa mara na matatizo ya moyo kila anapokumbuka kitendo hicho.Kesi inasikilizwa kwenye Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, chini ya Hakimu

Huyu mokiwa amedhihirisha uanglikana wake.
 
Malasusa,Mokiwa,Gwajima na Lusekelo ni watumishi wa Mungu au wa nani? Mbona visa haviwakwepi?
 
Mokiwa alitoa maelezo hayo huku akichukua bastola yake baada ya kufunga mlango na kuingiza risasi mbele yao huku akiwamuru wanyoshe mikono juu.
Mtikila anasema Mokiwa alifanya upekuzi mwili mzima kiasi cha kumushika makalio na sehemu za siri jambo lililomdhalilisha huku akijua kwamba kanisa lake limekubali Ushoga
RIP Mtikila
 
Back
Top Bottom