Askofu Mokiwa akataa rushwa ya Sh11 milioni

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,315
33,109
SIKU 16 kabla ya kufanyika wananchi kupiga kura, askofu mkuu wa Kanisa la Anglikana, Dk Valentino Mokiwa amedai kuwa hivi karibuni alipelekewa rushwa ya Sh11 milioni na mtu asiyemfahamu ili asizungumze masuala ya uchaguzi.

Dk Mokiwa alisema hayo kwenye tamasha la kuombea uchaguzi mkuu lililoandaliwa na Usharika wa Yombo wa Kanisa la Kiinjili la Kulutheri Tanzania (KKKT) Dar es Salaam jana.

Alisema tukio hilo lilitokea siku moja baada ya watu wawili mmoja akiwa anamjua kwenda nyumbani kwake kwa lengo la kumsalimia ambapo alizungumza nao kisha wakaondoka.

“Siku moja baadaye, mlinzi alinipigia simu akaniambia yule mgeni wa jana ameleta ….nikamwambia kwa nini ulichukua? sina ahadi na mtu yeyote kuniletea mzigo,” alisema Dk Mokiwa.

Alifafanua kuwa taarifa hizo zilimlazimu aende nyumbani kwake ili kujua nini kimeletwa... na alipofungua alikuta fedha taslimu Sh11 milioni ambazo zilimtia wasiwasi.

“Nikampigia yule ninayemfahamu nikamwambia njoo uchukue fedha za jamaa yake, akaniambia 'usiwe na wasiwasi', nikamwambia haiwezekani njoo akaja akachukua zile fedha,” alisema.

Aliongeza kuwa alikumbuka maneno ya mtu yule wakati walipokwenda nyumbani kwake kuwa nyinyi (viongozi wa dini) mkizungumza nchi inatikisika, akaona ile ilikuwa ni rushwa ili anyamaze kuzungumzia masuala ya uchaguzi mkuu ujao.

Alisema aliamua kukataa fedha hizo kwa sababu alikuwa na wasiwasi asije baadaye akaambiwa na yeye alipewa fedha za rushwa na kumalizia nyumba yake kwani ile kwake ilikuwa ni rushwa ili anyamaze.

Akizungumzia hoja yake iliyopingwa na taasisi za serikali zinazohusiana na rushwa na uchaguzi kwa madai kuwa anahamasisha watu kupokea rushwa, Dk Mokiwa alisema:

“Mimi sikuhamasisha rushwa ila nilikuwa nawapinga viongozi wabaya wanaotoa rushwa kwa wapiga kura. Sheria ya Gharama za Uchaguzi si mbaya, lakini wasimamizi wa sheria hiyo ndio wabaya,” alisema Dk Mokiwa.

Alidai kuwa atafanya awezalo kuhakikisha kuwa viongozi wala rushwa hawaiongozi nchi hii kwa sababu mwaka huu rushwa imeenea na wakati huu wa kampeni rushwa ndio inaliwa sana na viongozi wasiokubalika ndio watoa rushwa.

“Tunamuomba Mungu leo, tupate viongozi ambao hawajawahi kutuongoza nchi hii; viongozi watakaotuletea amani bila ya kuwepo polisi shirikishi kwa kuwa hapa tulipofika ni matokeo ya kuwapa ushirikiano viongozi wabovu,” alisema.

Akizungumzia kauli ya vyombo vya usalama juu ya amani kulekea kwenye uchaguzi, Dk Mokiwa alisema ili kulinda amani iliyopo hakuna budi vyombo hivyo vikatenda kazi yake bila ya upendeleo katika kusimamia uchaguzi.

“Nani alisema hakuna amani, tatizo ni vyombo hivi vinataka kuwalinda watu waendelee kuongoza wakati wananchi wamewachoka. Wanatakaiwa wawe fair katika usimamizi,” alisema.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi
 
Ni kwanini huyu Askofu asimpeleke huyu jamaa TAKUKURU?
Hayo si ndo makosa wanayoshughulikia? Naomba elekezo hapo.
 
Ni kwanini huyu Askofu asimpeleke huyu jamaa TAKUKURU?
Hayo si ndo makosa wanayoshughulikia? Naomba elekezo hapo.

Hukumu ya kukataa rushwa ni mbaya kuliko kwenda Takukuru, maana huenda kule angehonga na kuachiwa!
Kwa tendo hilo la kukataa kwake, then jumuia yote ya kitanzania imejua mpango huo.
Lakini inatakiwa mtu huyo atajwe ili ijulikane anamtumikia nani!
Huu sasa ni ushenzi wa ccm uliokithiri, kama wanataka kuwanyamazisha hadi wachungaji wa kondoo kwa Rushwa?
Tegemeo laolilikuwa kwamba kwa vile alisema watu wapokee rushwa na kuzila, then yeye mwenyewe angepokea rushwa hiyo...Maaskofu wana maono....fedha hizo zilikuwa na mkono uliofichama kwa nyuma, ambao ungetumika kumdhalilisha askofu huyo machachari, na kumwondolea uaminifu na heshima yake mbele ya KANISA na jamii!
Hongera MOKIWA!
 
Alipokea au hakupokea?
Tutathibitishaje?
Ila does it really matter now?
 
Aache kudanganya wajinga,yeye mwenyewe njaa tupu,halafu akatae 11miliion!
 
Wanajamvi,
Samahani nauliza hivi Askofu Mokiwa amefikwa na nini? Mbona amepotea/amepotezwa kama Askofu Kilaini?
Karibu kila kiongozi awe wa dini, siasa au Kijamii tayari amesema au kutoa tamko kuhusiana na tukio la Arusha, hali ya maisha na wimbo wa Taifa i.e BABU WA LOLIONDO. Lakini katika hayo yooote sijamsikia Askofu Mokiwa! Kulikoni? Mwenye taarifa na kilichomsibu Askofu Mokiwa, tafadhari anishirikishe.
 
. Lakini katika hayo yooote sijamsikia Askofu Mokiwa! Kulikoni? Mwenye taarifa na kilichomsibu Askofu Mokiwa, tafadhari anishirikishe.

Mbwe mbwe zao na matusi waliyo watukana viongozi na CCM wakitegemea padre Slaa angekuwa rais ndio zinazo mtesa. Wenzake wamenuna yeye amesusa kaaz kweli kweli.
 
Back
Top Bottom