Askofu Mhogolo amshambulia Dr Slaa na CHADEMA; asema anawahadaa Watanzania na Siasa za Utapeli

Siyo wote ni maaskofu wa kweli kweli jamani. Dini zimeingiliwa siku hizi na ndiyo maana tunao wengine wanajiita manabii au mitume. Nishawahi kukutana na askofu ambaye alishawahi kuwa mkuu wa wilaya hapo awali. Tena enzi ya ruksa, mtu kama huyo kwa nini asitamke maneno kama hayo?

Waumini wake ndo wamhukumu. No more sadaka na fungu la kumi. Pia wapo wanachaguliwa kwa kura, sio kitu rahisi sana kumpata mtu mwaminifu kwa njia hiyo ndugu zangu japo ndo mifumo ya baadhi ya madhehebu yetu.
 
Mbona hajamsema Kikwete mwenye mamlaka ya nchi lakini amekuwa akiwaomba waalifu warudishe mali zetu. Aliwambelez wa EPA kuwa wakirudisha hatawashitaki, hivi sasa wanawaomba watuhumiwa wa ufisadi wajiondoe tu ndani ya CCM lakini sio kuwashitaki.

Huyu Askofu anatafuta kusifiwa na watawala wa dunia hii. Ole wake wake asemaya mwenye hakin hana haki na asiye haki kuwa na haki.

WAKO WACHUNGAJI WA KWELI NA WAKO AMBAO NI WA MSHAALA MUNGU WAO NI TUMBO.
 
problem ya wahubiri feki ni kutokuona ukweli.hawa wahubiri wengi kwa sasa ni wafanyabiashara wanaoiabudu ccm.huyu askofu yumo kwenye kundi la kuwanyonya watanzania kwa njia ya kukusanya sadaka na fungu la kumi.ni kipofu.mateso ya watanzania bila cdm hakuna kitu.ukombozi wa mali yetu umeanzishwa na cdm kama hana habari.kazi kubwa ya wahubiri hawa ni kuabudu watawala kwa kuogopa kuumbuliwa kwa maovu yao.hana kisomo cha kutosha kumzidi slaa kwani hata dr alikuwa huko na alikuwa mhubiri mzuri lakini akaona ukombozi hautapatikana kupitia kanisa.akatoka.si mnafiki.

brother, kidogo umepotoka. Dr. Slaa alikuwa padre wa kanisa katoliki na hajatokea huko huko kama unavyosema wewe. Wakatoliki wanayo system tight sana ya kuwapata hao viongozi wote. Na elimu si suala la kuuliza. Na tena unaipatia huko huko tangu ukingali sekondari. So, dr. Muweke mbali sana na hao jamaa zetu wanaojiita wachungaji au maaskofu wa madhehebu tofauti na la dr. Slaa ndugu yangu.
 
huyu bila shaka mafisadi wameshajua bei yake au alishikiwa bunduki kulazimishwa kuongea haya maneno?
naona kama anataka kutupoteza vijana , nadhani tusipokuwa makini na hawa viongozi wa dini watatuuza kama
wale wa burundi na Rwanda, watu walikwenda kujificha kanisani wakidhani wako salama kumbe hawakujua hata padri
alikua na ukabila, akaenda kuwachomea wakachinjiwa kanisani
ningekuwa mimi ni yeye ningejishungulisha na mambi zaidi kwa ajili ya nchi, vijana na viongozi wake kwa ujumla
Kuna wanasheria kama mabere marando na wengineo,kama wana ushahidi si wawapeleke mahakamani?....kuliko kuwatetea kina manji!
 
kwaiyo ukiingiliwa na mwizi nyumbani kwako na unaushahidi huendi mahakamani kwasababu wewe sio serikali.kabla ujaongea humu shauriana na mkeo

Naona mwinyi umeingia!! Mimi mwizi akiingia kwangu namkukata kata viungo bila kushauriana na yeyote.

Ila hawa mafisadi wameitapeli nchi kwa ujumla,na hapo ndio baraka na nguvu ya serikali inapohitajika. Ni hii serikali ndio inayowakumbatia hawa mafisadi.

Njaa mbaya,hata askofu Muhogo..Lol ni bin adam. Anaanzia mbali,ila cheap popularity ndio inayomsumbua yeye kutafuta attn ya watu,2015 sio mbali mtaona...
 
Anaishi Tanzania gani?Labda hajaskia kuwa miongoni mwa waliokuwa kwenye list of shame ya 2007 leo hii wako mahakamani kwa tuhuma za ufisadi na wengine wameporwa ulaji ndani ya CCM na kupachikwa jina la magamba.

Ama kweli si wote wasemao BwanA Bwana watauona ufalme wa mbingu.The so-called askofu ameona kelele za Dkt Slaa/Chadema dhidi ya ufisadi ni hatari zaidi kuliko ushetani unaofanywa na mafisadi kwa WALALAHOI!!!

HAlafu anasema Slaa apeleke majina ya mafisadi mahakamani!!!Anamaanisha mahakama hizi hizi zilizomhukumu Chenge faini ya laki 7 kwa kosa la kuu ,au mahakama ya kina Ocampo?Tatizo la baadhi ya hawa watmishi feki wa Bwana ni they are so out of touch with the reality wanajikuta wanaropoka tu ionce wakiwa kwenye mahubiri yao.

Huu ufisadi wote wakulaumiwa ni Maaskofu. Huo ndio ukweli maana ukisoma maandiko Mungu amewapa mamlaka kubwa hata ya kuwaondoa watawala madarakani, sema tu hawa wa sasa nao hawajui kumtafuta Mungu.

Waambie wasome habari za akina Musa, Elia, Elisha, Yehu, Daniel, Na wengine wengi! Sasa wao wamebaki wanapiga bla bla hadi nchi inafikia hapa tulipo!

Tukubali tusikubali hawa Maaskpfu wanastahili lawama zote, wamemwachia Pengo, Malasusa na Mokiwa peke yao ndio wanapambana na mafisadi. Wengine wamebaki wakijikomba kwa watawala waovu! Kwa Masheikh sijui maana sijui kitabu chao kinasemaje kuhusu jambo hili maana wao nao ndo wako kichakani zaidi! Mnasemaje wadau kuhusu hawa maaskofu vipofu?

Tupige kura ya kutokuwa na imani nao maana kuna wengine wanafaidika na pesa za mafisadi.
 
Baba Askofu Mhogolo Godfrey, ni kiongozi wa kiroho mwenye upeo wa hali ya juu sana, sisi wengine ndio umetufumbua macho hongera mtumishi wa Mungu wewe ni msomi tunakukubali
 
Askofu Godfrey Mdimi Mhogolo wa Dayosis of Central Tanganyika Mkoani Dodoma,amemjia juu Katibu Mkuu wa Chadema na chama chake kuwa wana wachezea Watanzania kwa kujijengea umaarufu rahisi(cheap popularity). Askof Mhogolo katika mahubiri ya Ijumaa Kuu alisema kitendo cha Dr Slaa kutaja watuhumiwa wa Ufisadi mwaka 2007 huku akiwa na Ushahidi juu ya wanaotuhumiwa na Ufisadi huku akitembea na ushahidi kwenye briefcase ni Kujitafutia Umaarufu na kuwapotezea muda Watanzania! Kama umemkamata mwizi na una ushahidi kwa nini usiende mahakamani na Watuhumiwa washitakiwe!? Kitendo cha Dr Slaa kuongeza tena orodha ya Watuhumiwa huku aliowataja haja peleka ushahidi wake mahakamani kwa orodha ya mwaka 2007 ni kazi ya pwagu na pwaguzi! Ana wahadaa Watanzania kutokana na uelewa wao mdogo hasa vijana wanao mshabikia! Alimalizia kwa kusema Chadema imekaa na mtizamo wa kutaka watu waiunge mkono kwa fujo na maandamano lakini Viongozi wake wako kwa kujitafutia Umaarufu wa kisiasa. Akaonya Wanapofanya maandamano yao na uvunjifu wa amani kama ya jijini Arusha wakumbuke kuna amani ya Watanzania ambao si wafuasi wa vyama.

Sasa hiki anachokifanya CCM "KUJIVUA MAGAMBA" tukiiete je? Kwa shinikizo la Dr.Slaa, CHADEMA na nguvu ya wananchi wamekiri kua MAFISADI. Mbali na Dr.Slaa kuwataja, CCM na JK mbali na kukiri kuwa wao mafisadi na vyombo vya sheria viko mikononi mwao HAKUNA HATUA ZOZOTE WANAZOZICHUKUA Mbali na ngonjera za kujivua magamba.

HAPA NANI MSANII?
MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
kwaiyo ukiingiliwa na mwizi nyumbani kwako na unaushahidi huendi mahakamani kwasababu wewe sio serikali.kabla ujaongea humu shauriana na mkeo

Wakati alipotegewa vinasa sauti chumbani Dodoma na akalalamika na Polisi wakaja kuchunguza hadi leo hawajatoa ripoti! Unategemea nini? Tanzania kuna mambo ukipeleka Polisi na mahakamani ni tabu tu! Kama mimi nimeamua kuanzisha mahakama yangu! Juzi juzi niliibiwa nikaripoti watu wakakamatwa hawakukaa dk 20 tena wakadhaminiwa na mkuu wa Polisi, siku iliyofuata wakaliza watu wengine kama 6 hivi, wakakamatwa hawkukaa nusu saa baada ya walalamikaji kuondoka! Hivi majuzi nimewafuma mahali,mmoja nimevunja mguu mwingine mkono! Nataka nitafutwe mimi sasa. Na nimeamua niendelee kujifua vizuri kwenye fani yangu ya Karate: karibuni kwenye hiki chama maana hii nchi tuendako waoga hawatakuwa na chao.
 
MGOGO NA CCM?????!?!???????? Haina haja ya tochi mana watu tunaoishi dodoma tunawafahamu,whr is KANU??????????????????
Askofu Godfrey Mdimi Mhogolo wa Dayosis of Central Tanganyika Mkoani Dodoma,amemjia juu Katibu Mkuu wa Chadema na chama chake kuwa wana wachezea Watanzania kwa kujijengea umaarufu rahisi(cheap popularity). Askof Mhogolo katika mahubiri ya Ijumaa Kuu alisema kitendo cha Dr Slaa kutaja watuhumiwa wa Ufisadi mwaka 2007 huku akiwa na Ushahidi juu ya wanaotuhumiwa na Ufisadi huku akitembea na ushahidi kwenye briefcase ni Kujitafutia Umaarufu na kuwapotezea muda Watanzania! Kama umemkamata mwizi na una ushahidi kwa nini usiende mahakamani na Watuhumiwa washitakiwe!? Kitendo cha Dr Slaa kuongeza tena orodha ya Watuhumiwa huku aliowataja haja peleka ushahidi wake mahakamani kwa orodha ya mwaka 2007 ni kazi ya pwagu na pwaguzi! Ana wahadaa Watanzania kutokana na uelewa wao mdogo hasa vijana wanao mshabikia! Alimalizia kwa kusema Chadema imekaa na mtizamo wa kutaka watu waiunge mkono kwa fujo na maandamano lakini Viongozi wake wako kwa kujitafutia Umaarufu wa kisiasa. Akaonya Wanapofanya maandamano yao na uvunjifu wa amani kama ya jijini Arusha wakumbuke kuna amani ya Watanzania ambao si wafuasi wa vyama.
 
kwaiyo ukiingiliwa na mwizi nyumbani kwako na unaushahidi huendi mahakamani kwasababu wewe sio serikali.kabla ujaongea humu shauriana na mkeo

Nadhani ndugu yangu hufahamu kuwa katika nchi yetu mwenye mamlaka ya kufungua mashitaka ya jinai wa aina yoyote ile ni Jamhuri. Mtu binafsi anaruhusiwa lakini Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) anaruhusiwa kuingilia kati na kupewa jukumu la kuendesha kesi hiyo. Pale DPP anapoingilia kati utamaduni uliopo ni yeye kuamua kufuta mashitaka yale na ndio maana mashitaka binafsi hayafunguliwi nchini kwani ni kupoteza muda. Katika mazingira hayo mtu huna njia nyingine zaidi ya kufungua mashitaka katika mahakama ya watu ambao ndio wenye nchi.

Kwa bahati mbaya utamaduni ambao ninauona umejengeka katika nchi yetu na hata michango inayotolewa na manazi wa ufisadi ni kuwa kila kitu lazima kiende mahakamani na wanasahau kuwa kuna njia nyingi za kumuua mbwa. Waweza kumunyonga, kumpiga risasi, kumkaba, kumpiga mkuki, kumnyima chakula na kadhalika na kadhalika.

Nadhani Askofu huyu nia na upendo wake kwa nchi yetu ni mdogo kwani anatumia kutoelewa taratibu za uendeshaji wa mashitaka nchini kudanganya watu kuwa Dk. Slaa kutoa tuhuma hizo nzito mbagani(hadharani) ni uchochezi. Hoja ni kuwa wale wote ambao wanaona wamechafuliwa majina yao wao ndio wakimbilie mahakamani na kudai fidia dhidi ya Dk. Slaa ukimya wao na kutumia waganga njaa kama Askofu huyo kunathibitisha kuwa tuhuma dhidi yao ni za kweli na hivyo wanatakiwa kuwajibishwa na wenyenchi yaani sisi Watanzania. Nadhani kama na wewe ulikuwa hujui taratibu za kuendesha kesi za jinai umeelimika na utaacha unazi katika masuala mazito kama haya na kujiunga katika vita vya kupinga ufisadi na kuwapa moyo wote wale wanaoendesha vita hivyo vitakatifu.
 
Hivi hiyo amani inayosadikiwa kuvunjwa ni ipi wajameni? Mie mwenzenu siioni hiyo amani.nisaidieni tafadhali
 
Acha uongo wewe, Slaa hakuacha upadri kwa sababu ya kutaka kuwakomboa watanzania. Kiapo cha useja kilimshinda! Wachumba angemuachia nani? Halafu mbona huyu hamumtukani sana kama MUFTI? Au kwa sababu ni wa zizi lile lile? tehetehetehe Chadema mnafurahisha!

Useja ni uamuzi na kuacha ni uamuzi, acha kuongea usiyoyajua.
Halafu suala la mchumba au mke ni mambo binafsi, hata wewe tukikuchunguza una matatizo kibao ya kinyumba, hayo ni mambo ya watu wawili kuwa na akili wewe
 
Baba Askofu Mhogolo Godfrey, ni kiongozi wa kiroho mwenye upeo wa hali ya juu sana, sisi wengine ndio umetufumbua macho hongera mtumishi wa Mungu wewe ni msomi tunakukubali

Kama kauli aliyoitoa kuhusiana na Dk. Slaa ndio kipimo cha usomi na upeo wa juu ni bora basi dunia hii hakuna wasomi na mazuzu ndio waliosoma.
 
Tatizo ni kwamba hapa tz hatuna viongozi wa dini wenye ujasiri kama wa Yohana Mbatizaji ambaye alithubutu kumkosoa mfalme hadi akakatwa kichwa. Siku hizi baadhi (wengi) wa wanaoitwa viongozi wa dini hawana upendo kabisa kwa watanzania na wana tamaa kubwa sana ya pesa kiasi kwamba wameishia kwenye pay-roll ya chama cha magamba, infact nao ni magamba ambayo jk anajaribu kuyavua ila sidhani kama ni rahisi kwa kobe kujivua gamba lake bila kuhatarisha maisha yake mwenyewe!
 
Yawezekana huyu askofu akawa hajamaliza hata kindagaten. Kwani hoja za Dr hata watoto wa chekechea ukiwaelimisha vizuri wanakuelewa sembuse huyu.
Mmmmh kazi bado ipo.
 
Unajua wakubwa, jina askofu limeshachakachuliwa mno, usishangae hao wanaojiita maaskofu. Askofu anafahamika, askofu hoja yake inafahamika.
Mimi sishangai kuona watu wa namna hii, wapo tu Tanzania, Kama wakubwa mnavyojua kweli mahakamani kufanya nini ? CDM inapiga kelele za mwizi huyoOOOOO!

Nilidhani mhogolo naye angetumia jiwe alilonalo la madhababu kupiga kelele, ni Kama CCM wenyewe wameanza kupiga kelele mwizi huyo, PCCB wangekuwa wametulia nao wangetumia rungu lao kumdunda huyo mwizi na ndio wale njagu wangepeleka mahakamani.

CCM imekiri wapo mafisadi tujadili nani anayepaswa kuwapeleka mahakamani? nani anayewahadaa wananchi, Je ni yule anayesema wapo ni kweli wapo na yule anyekanusha hakuna wezi kisha anasema wapo na wako nyumbani kwao na wana pesa walizoiba na zingine walishakula pamoja na wakanunulia mavazi na chumvi kwa wanakijiji?
 
Kwanza kabisa Ukitamka Askofu wa Dayosis ya Central Tanganyika. Utagundua hizi ni fikra mgando zinaelekea kuzungumzwa. Yaani yeye haoni bado baadhi ya watu wameacha nyadhifa zao kwa ajili ya kuwajibika na mmulikaji wa hayo ni Dr Slaa. Yeye kama yeye kwenye ufisadi hakosi, yumo kabisa maana anawaibia maskini na kujinufaisha mwenyewe. Mimi siwezi kumwombea asamehewe maana yeye ndiye anayepaswa kutuombea sisi na nchi yake. Lakini anakuwa wa kwanza kukemea harakati za ukombozi!!!!. Kuna walakini.
 
Back
Top Bottom