Askofu Malasusa msemaji wa familia ya Lowasa

Viongozi wa dini kwa mujibu wa Biblia takatifu hawapaswi kuwatenga wenye dhambi. Njooni kwangu ninyi nyote mnaolemewa na mizigo. Wenye dhambi pia wanapaswa kwenda kanisani kutubu dhambi zao. Lakini tunapaswa kuacha kuhukumu wengine ili nasi tusi tukahukumiwa.
Nimejaribu kudokoa kidogo kidogo hapa na pale maandiko katika kitabu kitakatifu ingawa sijaonyesha mistari husika. Nadhani hiyo ndiyo busara ya viongozi wa dini kutokuwatenga wale wao wawaendeao kwa unyenyekevu.Hata Yesu Kristo alipokaa na kula chakula na wenye dhambi wapo viongozi wa dini waliomshangaa, lakini Yesu aliwajibu " Sikuja kwa ajili ya watakatifu bali wenye dhambi ili waokolewe
Mkuu kwa kauelewa kangu kadogo Lowasa anasali pale azania front ambapo ndio shughuli nyingi za uongozi wa KKKT tanzania zinafanyikia so i hope wanajuana kabla hata ya Malasusa kuwa askofu... lkn hii ya viongozi wetu wa dini kuwabeba wenye pesa na madaraka na kuwapa sifa zisizohitajika hata pale wanapoonekana kutengwa na jamii kamekuwa sugu. na huwa ndio hapo naona safari ya mbinguni ni ngumu kwa kweli, hatuiigi mfano wa yesu aliye wasema wazi wazi viongozi wa kipindi hicho, any way labda ndio mambo leo ya kwenye dini haya
 
Namkumbuka Askofu JERY NGWAMBA askofu wa KKKT Dayosisi ya Mahariki na Pwani aliyekuwa akijihusisha na vitendo vya aibu na kuamua kukimbilia Marekani mpaka leo! ni kweli EL ni msharika wa siku zote pale Azania Front! Mungu anasema ole wenu waandishi na mafarisayo..........................................(mnaweza kuongezea ijnili inavyosema)
 
Back
Top Bottom