Askofu Kulola: Kuna mtandao wa kisiasa makanisani

Watanzania!
Unajua huyu jamaa yetu bila fitna mambo hayaendi. Sasa ukisoma hiyo stori ya gazeti la uhuru kuhusu Kulola utaona kabisa ni story iliyojaa udini! Kwa sababu wanataka watu wa-conclude kuwa Kikwete anapingwa kwa ajili ya uislam wake na Dr Slaa amependwa kwa sababu ya Ukristio wake. Hizi zote ni technics za Kikwete baada ya kuona mambo si mazuri!

Uhuru ni nini? Kuna mtu bado anasoma uhuru.
 
Mzee Kulola anapaswa kufahamu kuwa Wakristo kwa umoja wao walimchagua JK kuwa Raisi tena kwa kuambiwa kuwa ni chaguo la Mungu, hapo udini haukuzungumzwa. Leo hii watanzania wamemchoka JK, wakristo kwa waislamu. Kukataliwa kwa jk hakuna uhusiano wowote na dini, hii ni propaganda tu ya si si emu. Kazi imemshinda, maisha ya watanzania yanazidi kuwa duni, vijana hawana ajira, mafisadi wametawala, na yeye mwenyewe jk yuko kwenye list ya mafisadi nk. Hii ndiyo sababu waislamu kwa wakristo wanataka mtu mbadala, mwenye maono ya kuwaletea watanzania ukombozi wa kweli. Huyo ndiye tunamtaka, na tayari Mungu ametupatia viashirio, watanzania tusipoteze nafasi hii. Mtu ni Dr Slaa tu
 
Huyu askofu na Lusekelo ni watumishi mufilisi. Shule ndio inawapa shida. Pia harufu za ufisadi haziwakosi. Ukiwasikiliza utajiuliza hivi hawa ni watumishi wa Mungu yupi?
 
Wakristo na Waislamu wanajua kuchagua pumba na mchele. Hakuna kiongozi yeyote wa dini kwa matamko au maelekezo yasiyo na mantiki atawapeleka kama vile wakristo wa karne za giza waliokuwa watumwa wa mapapa mafisadi. Ni vizuri kurejea reformation na kujua kuwa renaissence ilikwishafuta zile nyakati. Huwezi tu kusema piga kura hivi na watu wote (maana makanisani na misikitini kuna watu wa kila sampuli) wakakukubalia bila kufikiri. Mzee Kulola usiwe na wasiwasi tutapiga kura zetu kwa kutumia akili zetu na kutathimini yote waliyotufanyia siku za nyuma!!!!!!
 
Mimi ni muumini wa EAGT lakini kwa hili Askofu wangu mkuu kapotoka. Ninamuombea!!!
Babu tazama maslahi ya nchi na taifa... waruhusu watu wakapige kura tarehe 31 na using'ang'anie ibada ya jumapili ya tarehe 31 na maombi yasiyo na majibu (hayako kwenye utaratibu wa Mungu). Mungu ameleta uchaguzi ili tumchague Kiongozi kama wana wa Israeli walivyochagua wafalme. Leo unatupa utaratibu usiokuwa Kibiblia kabisa. Utashangaa kuwa mahudhurio yatakuwa madogo sana kanisani siku hiyo. Mimi ni mmoja wa watakao kosa ibada. Nitaenda kusali TAG.
 
Kipofu akimwongoza kipofu mwenzake wote hutumbukia shimoni. Moses ni kipofu kwa zaidi ya miaka mitano sasa na kibaya zaidi hajitambui kuwa kipofu. Huyu ndie aliyemnadi Jk ni chaguo la Mungu, sasa anachofanya ni kujaribu kumsaidia mungu aliyemchagua kikwete asishindwe na raia zake.
 
Hivi Kumbe Moses Kulola bado yuko hai? nilimwona pale Shycom miaka 20 imepita. Mzee kama uko hai umechoka usiongee maana huu umri wa kula ugoro, lewa, kojoa,lala.
 
ana mgawo wake hapo, mjukuu ambaye ni mwimbaji wa injili mbona anaimba siasa na amenyamaza? toa boliti jichoni mzee ndipo utaona kibanzi kwa mwenzio....
mbona hao watu mnaowatuhumu leo walisema JK ni chaguo la Mungu mkachekelea bila kukemea kuwa wametumia jina la Mungu bure? leo wamesema msichague mafisadi mnalilia kama watoto....mnataka kutuaminisha kuwa CHICHI m ni mafisadi na tuendelee kuwapa kura?
katika hili MTUMISHI nakupinga kwa ujasiri kabisa, i wish ningekuona kwa macho ni kuambie kweli hii.....injili ya siku hizi sio kama ya zamani ambapo mliweza hata kufundisha mapotofu bila kupingwa na waumini leo tunakupinga ukienda kinyume na kweli ya Mungu....unapinga siasa kanisani unamalizia kwa kupiga kampeni....
i guess umeishiwa mzee wangu hasa ktk hili uko nje kabisa ya point,unapinga watu kutowachagua mafisadi? wewe unatakatuongozwe na mafisadi?
Aisee... kuna siku wengi tutakimbia hapa jukwaani.
Yaani watanzania mnajua kujenga hoja kwa kiwango kizuri sasa. nakumbuka enzi za akina cicero na akina brutus wake ambapo kama hukujua public skeaking baas weye hufai kwenye seneti wala cheo chochote kwa warumi. The art of speaking
 
Wakuu zangu,
naposoma mada hii na hoja zake nashindwa kuelewa kama watu wanampinga huyu Askofu na kuhalalisha yanayofanyika au ndio ktk ustaarabu wa nyani haoni kundule!.

Tunapiga vita Udini iwe unafanywa na Masheikh misikitini au Mapadre makanisani, sasa mimi sioni baya lolote hasa kwa kiongozi wa dini kama huyu kasimama na kukemea matumizi ya Udini ili kumpata Kiongozi. Tena naweza kumpa pongezi kubwa kiongozi huyu kwa sababu sijaona upande wa Waislaam akitokea kiongozi pia kama huyu kukemea propaganda zinazoendeshwa na baadhi ya Masheikh!.

Jana tu nimesikia hotuba ya Mh. Membe huko Lindi, nikaanza kujiuliza hivi kweli taifa letu linakwenda wapi? Hivi kweli imefikia wakati tunawanadi viongozi wetu kwa jinsi walivyoweza kugawa kazi kulingana na dini za wahusika, tena tukatukuza maamuzi hayo kwa sifa kubwa kuonyesha jinsi JK alivyopendelea zaidi waumini wa dini nyingine. Na navyowajua waislaam na hasa wakazi wa Lindi watachukulia hotuba hiyo kuonyesha jinsi CCM inavyokumbatia Ukristu na pengine kuzidisha chuki zaidi baina ya waumini... Hotuba kama hizi hazijengi ila zinabomoa kwani zinaegemea upande mmoja tu wa sarafu..

Ningeshauri serikali na viongozi wote wa vyama ktk uchaguzi huu kutotumia Udini kwa aina yeyote ile kwani wakuu zangu msifanye mchezo. Huko Bongo sasa hvi siasa ni Dini kila anayezungumzia uchaguzi huu ni habari ya kumchagua Muislaam au Mkristu sio tena sera wala chama.. Tumefikia hali mbaya sana na hakika shuzi hili litafuatiwa na kimba ambalo Watanzania wengi litatupasua msamba!. Na maadam tumefikia hapa na bado wapo watu wenye akili zao timamu wanashabikia kila lisemwalo kwa rangi zao wenyewe basi tumefika mahala njia panda na hakika Uchaguzi huu hautakuwa salama...
 
1. source Uhuru = CCM
2. Huyu mzee he is the biggest hypocrite, 2000 in Dodoma alisema is the end of the
world akasema tutaonana mbinguni, shetani huyu
3. EAGT alianzisha kwa manufaa ya familia yake, pia alisema JK chaguo la Mungu back in
2005
4. ujue anazeeka vibaya look how he is, hata nywele zipo kama hazichani, ur fake bishop
look his face anaongopa, haongei kama bishop, fake, hajui watu wanajua mambo these
days
5. Waganga njaa kama Flora mbasha wanabweka bweeh:hurt: majukwaani kumpigia debe JK. mbona asiseme, Uzee mwingine unakuja vibaya, au anaota huyu,:glasses-nerdy::A S-confused1: shindwa, endelea kula
SADAKA za watu that is what u are for period
6, wakati JK anashindwa kuwakamata mafisadi na bado anawatetea wakina ndege ya uchumi:plane:, mvua ya kununua:rain: ila tumedanganywa jamani mmmhhhh na wenzake, huyu mzee alikuwa wapi? anaota:A S 33: mwacheni

Dr Slaa gooooooo:rockon::peace::israel:
 
Mkuu pengine umesoma kwa haraka lakini nakuomba sana msome tena kisha soma waliyosema NEC halafu nambie hata wao wamekosea kitu gani kwani wote hawa wanazungumza kitu kimoja. Sasa pengine wewe nambie ungekuwa mchungaji na ktk nafasi ya huyu mchungaji ungewambia nini bora zaidi waumini wako kuhusiana na upigaji kura uchaguzi huu!
 
Wakuu zangu,
naposoma mada hii na hoja zake nashindwa kuelewa kama watu wanampinga huyu Askofu na kuhalalisha yanayofanyika au ndio ktk ustaarabu wa nyani haoni kundule!.

Tunapiga vita Udini iwe unafanywa na Masheikh misikitini au Mapadre makanisani, sasa mimi sioni baya lolote hasa kwa kiongozi wa dini kama huyu kasimama na kukemea matumizi ya Udini ili kumpata Kiongozi. Tena naweza kumpa pongezi kubwa kiongozi huyu kwa sababu sijaona upande wa Waislaam akitokea kiongozi pia kama huyu kukemea propaganda zinazoendeshwa na baadhi ya Masheikh!.

Jana tu nimesikia hotuba ya Mh. Membe huko Lindi, nikaanza kujiuliza hivi kweli taifa letu linakwenda wapi? Hivi kweli imefikia wakati tunawanadi viongozi wetu kwa jinsi walivyoweza kugawa kazi kulingana na dini za wahusika, tena tukatukuza maamuzi hayo kwa sifa kubwa kuonyesha jinsi JK alivyopendelea zaidi waumini wa dini nyingine. Na navyowajua waislaam na hasa wakazi wa Lindi watachukulia hotuba hiyo kuonyesha jinsi CCM inavyokumbatia Ukristu na pengine kuzidisha chuki zaidi baina ya waumini... Hotuba kama hizi hazijengi ila zinabomoa kwani zinaegemea upande mmoja tu wa sarafu..

Ningeshauri serikali na viongozi wote wa vyama ktk uchaguzi huu kutotumia Udini kwa aina yeyote ile kwani wakuu zangu msifanye mchezo. Huko Bongo sasa hvi siasa ni Dini kila anayezungumzia uchaguzi huu ni habari ya kumchagua Muislaam au Mkristu sio tena sera wala chama.. Tumefikia hali mbaya sana na hakika shuzi hili litafuatiwa na kimba ambalo Watanzania wengi litatupasua msamba!. Na maadam tumefikia hapa na bado wapo watu wenye akili zao timamu wanashabikia kila lisemwalo kwa rangi zao wenyewe basi tumefika mahala njia panda na hakika Uchaguzi huu hautakuwa salama...

kweli kabisa Mkuu.................inabidi viongozi wote wakuu wa dini wakutane na watoe tamko ili kutowavuruga/kutowachanganya wananchi.............
 
kweli kabisa Mkuu.................inabidi viongozi wote wakuu wa dini wakutane na watoe tamko ili kutowavuruga/kutowachanganya wananchi.............
Mkuu wangu, nashangaa watu tunashindwa kabisa kujizuia na aibu hii ya Udini kiasi kwamba tunaanza kukumbatia vitu vinavyofanywa na vichaa.. Hao Masheikh uchwara waliopewa Bakwata kama chombo chao cha ufisadi tena ati sheikh wa msikti wa Manzese sijui Kinondoni Mtambani ambao wanajulikana kabisa kwamba hawana elimu zaidi ya kuganga njaa, leo nasi watu wazima na akili zetu tunakuja mchukia kiongozi wa dini kama huyu ambaye kasema vitu ambavyo hakuna kiongozi hata mmoja aliyeweza kukemea iwe JK, wastaafu, Sheikh mkuu au Kardinali Pengo wote wamekaa kimya hali Udini unaingia hatua mbaya zaidi.

Haya sii maswala ya kushabikia hata kidogo kwani CCM wanataka ya Rwanda dalili zake zitokee within hizi week mbili zilizobakia hivyo kuwatia wasiwasi wananchi na kumchagua Dr.Slaa. Hakuna silaha mbaya kama kuzusha FEAR among us, ukisha weza kujenga fear ndani ya mioyo ya watu hakika hakuna msalie kwani waathirika sio Waislaam wala wakristu isipokuwa ni sisi sote kwa ujumla wetu. Na CCM mtandao ndicho wanachokitafuta baada ya kushindwa mbinu zote..

Hao viongozi wa dini mkuu wangu wote zuga tu..hatuna imani ya dini sisi wote zuga tu, leo hii akitokea Pharaoh akabadilisha fimbo kuwa nyoka hakuna cha Sheikh mkuu wala Kardinali wote watatoka mkuku...imani ndogo! - mtanisamehe wenye imani kubwa na viongozi wenu.
 
Mkuu pengine umesoma kwa haraka lakini nakuomba sana msome tena kisha soma waliyosema NEC halafu nambie hata wao wamekosea kitu gani kwani wote hawa wanazungumza kitu kimoja. Sasa pengine wewe nambie ungekuwa mchungaji na ktk nafasi ya huyu mchungaji ungewambia nini bora zaidi waumini wako kuhusiana na upigaji kura uchaguzi huu!

"NEC=CCM, KuLOLA=CCM therefore NEC=Kulola" kama unajua mathematics
 
Askofu Kulola sasa kutumika katika TV kumsadia JK

askofu.jpg

Siku chache baada ya Askofu wa makanisa ya Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) Mosses Kulola, kutamka kuwa kuna mtandao wa kisiasa makanisani ambao unampigia debe mmoja wa wanasiasa nchini.

CCM imeamua kumtumia katika Kampeni za lala salama kujaribu kubadili mtazamo wa Wakristu kwa kumtuma Paschal Mayala kupitia kampuni yake kumrekodi ili watengeneze kipindi maalum ambacho kitalipiwa na CCm na kurushwa Star TV, TBC na ITV.

Uamuzi huo umefikiwa na Kikao cha Familia baina ya Ridh 1, Miraji na Bibi na Bwana jakaya Kikwete baada ya kukubaliana na mtoto mmoja wa Askofu huyo na kuelezwa kuwa akaongee na Askofu na wao CCM watamlipa.

Baada ya mazungumzo hayo kufikiwa jukumu la kumlipa fedha Kulola amekabidhiwa Waziri Ngeleja mkoani Mwanza ambapo jana amewasiliana na Askofu huyo kwa faragha na kumkabidhi mzigo wake na leo Paschal Mayala anasafiri kutoka Dar kuja Mwanza kwa kazi hiyo ya kutengeneza kipindi maalum.
 
Ni hatari sana dhambi inapofika patakatifu kama altareni na kuwahusisha wahudumu waliotukuka.
 
siungi mkono masuala ya udini, lakini Askofu Kulola sio msafi kama anavyojaribu kuonyesha!. kwanini haelekezi tuhuma hizo kwa viongozi wa dini wasiokuwa wakristu ambao pia wanafanya vitendo hivyo?, nani alimwambia kwamba kiongozi wa dini anapaswa kuendelea kuomba huku waumini wake wakiteketea kwa ufisadi?

gazeti linataja kuw ani mmoja kati ya viongozi wa dini wanaoheshimika sana, nani kasema?

Wakati ule wa mgogoro wake na askofu Emanuel lazaro kabla ya kujitoa TAG na kuelekea alipo hivi sasa anaweza kutueleza kilitokea kanisani Tabora?

Anawezwa kutueleza kwa nini Binti yake aliyeolewa na Bwana wa kwanza aliyekuwa akiishi jirani na hospitali ya Bugando alimfungisha ndoa mara mbili?
Aisee. JF si mchezo. yaani hata ushuzi ukiupiga mwaka 90 watu watakuletea hapa rangi yake lol.

Askofu Kulola ni mzee sana sasa, nguvu zimemwishia na anadhani watanzania wooote ni wajukuu zake. Alipaswa kwanza kumshauri mjukuu wake kwamba ondoka kwenye mtaguso wa kisiasa hubiri injili. kisha ndo aje kutuambia kwamba EENYI WAAAATU WA MUNGUUU! MSITUMIE MADHABAHU KUPIGA KAMPENI ZA WAGOMBEAA!! Lakini pia sijaona mtumishi yeyote wa mungu akisema kwamba mchagueni fulani au fulani bali wanasema chagueni watu safi wenye kuonesha mwelekeo wa kuwaletea maendeleo.

Enzi za mfalme YEHOSHAFAT aliwaita Manabii mia nne wa Mungu wamtabirie kama aende vitani au la. Wakamwambia kwea kwani Mungu atamtia adui yako mikononi mwako. ila akaletwa nabii mmoja aitwaye MIKAYA ambaye akasema nenda ukaanguke vitani. Na akasema kwamba roho wa uongo ameingia kwenye vinywa vya manabii ili Mungu akakuue kule vitani. Mfalme akamwonea hasira na kumfunga mikaya lakini alipoenda vitani hakurudi mzima. soma Mambo ya Nyakati 18: 3 - 34
Ujumbe wangu kwa Mzee Kulola ni kwamba. hata mtumishi wa Mungu anaweza kuwa kama Sedekia mwana wa Kenaana kwa kumtabiria kikwete yale ambayo Mungu hakupanga mbele yake. Kuna uwezekano mtu asirudi nyumbani salama safari hii.

Watanzania tuachwe kumchague tumtakaye. na tuhamasishane namna ya kuchagua kilicho bora. Tuna haki ya kumpigia kampeni tumkatake. ila hatujatumia mimbari kufanya hivyo. Kwa kuwa tumetoa sifa za yule afaaye na mzee kulola ameona mgombea wake hana sifa hizo ameanza kujifanyia pembe za chuma na kuanza kutabiri

Askofu Kulola sasa kutumika katika TV kumsadia JK

askofu.jpg

Siku chache baada ya Askofu wa makanisa ya Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) Mosses Kulola, kutamka kuwa kuna mtandao wa kisiasa makanisani ambao unampigia debe mmoja wa wanasiasa nchini.

CCM imeamua kumtumia katika Kampeni za lala salama kujaribu kubadili mtazamo wa Wakristu kwa kumtuma Paschal Mayala kupitia kampuni yake kumrekodi ili watengeneze kipindi maalum ambacho kitalipiwa na CCm na kurushwa Star TV, TBC na ITV.

Uamuzi huo umefikiwa na Kikao cha Familia baina ya Ridh 1, Miraji na Bibi na Bwana jakaya Kikwete baada ya kukubaliana na mtoto mmoja wa Askofu huyo na kuelezwa kuwa akaongee na Askofu na wao CCM watamlipa.

Baada ya mazungumzo hayo kufikiwa jukumu la kumlipa fedha Kulola amekabidhiwa Waziri Ngeleja mkoani Mwanza ambapo jana amewasiliana na Askofu huyo kwa faragha na kumkabidhi mzigo wake na leo Paschal Mayala anasafiri kutoka Dar kuja Mwanza kwa kazi hiyo ya kutengeneza kipindi maalum.

Du! Pascal ni ya kweli haya best?

Kama ni kweli, kuwa makini Mkuu hasa kama mazingira yake yana utata hata kama wewe ni mfanya biashara na unahitaji pesa.

Kumbuka historia ndiyo inaandikwa. Angalia dhamira yako!

I hope unaweza kusimamia kile ambacho unakihubiri.
 
Wakuu zangu,
naposoma mada hii na hoja zake nashindwa kuelewa kama watu wanampinga huyu Askofu na kuhalalisha yanayofanyika au ndio ktk ustaarabu wa nyani haoni kundule!.

Tunapiga vita Udini iwe unafanywa na Masheikh misikitini au Mapadre makanisani, sasa mimi sioni baya lolote hasa kwa kiongozi wa dini kama huyu kasimama na kukemea matumizi ya Udini ili kumpata Kiongozi. Tena naweza kumpa pongezi kubwa kiongozi huyu kwa sababu sijaona upande wa Waislaam akitokea kiongozi pia kama huyu kukemea propaganda zinazoendeshwa na baadhi ya Masheikh!.

Jana tu nimesikia hotuba ya Mh. Membe huko Lindi, nikaanza kujiuliza hivi kweli taifa letu linakwenda wapi? Hivi kweli imefikia wakati tunawanadi viongozi wetu kwa jinsi walivyoweza kugawa kazi kulingana na dini za wahusika, tena tukatukuza maamuzi hayo kwa sifa kubwa kuonyesha jinsi JK alivyopendelea zaidi waumini wa dini nyingine. Na navyowajua waislaam na hasa wakazi wa Lindi watachukulia hotuba hiyo kuonyesha jinsi CCM inavyokumbatia Ukristu na pengine kuzidisha chuki zaidi baina ya waumini... Hotuba kama hizi hazijengi ila zinabomoa kwani zinaegemea upande mmoja tu wa sarafu..

Ningeshauri serikali na viongozi wote wa vyama ktk uchaguzi huu kutotumia Udini kwa aina yeyote ile kwani wakuu zangu msifanye mchezo. Huko Bongo sasa hvi siasa ni Dini kila anayezungumzia uchaguzi huu ni habari ya kumchagua Muislaam au Mkristu sio tena sera wala chama.. Tumefikia hali mbaya sana na hakika shuzi hili litafuatiwa na kimba ambalo Watanzania wengi litatupasua msamba!. Na maadam tumefikia hapa na bado wapo watu wenye akili zao timamu wanashabikia kila lisemwalo kwa rangi zao wenyewe basi tumefika mahala njia panda na hakika Uchaguzi huu hautakuwa salama...

.
Tumefikia hapa mahali pabaya kwa kusababu ya kiongozi tulie nae kutokuwa na uwezo wa kuunganisha mshikamano wa taifa. Hili nalo pia limesukumwa na hulka yake ya kuendesha mambo kisanii. So huu udini ni tunda la mti, na mti wenyewe ni Jk.
 
askofu kulola sasa kutumika katika tv kumsadia jk

askofu.jpg

siku chache baada ya askofu wa makanisa ya evangelistic assemblies of god tanzania (eagt) mosses kulola, kutamka kuwa kuna mtandao wa kisiasa makanisani ambao unampigia debe mmoja wa wanasiasa nchini.

Ccm imeamua kumtumia katika kampeni za lala salama kujaribu kubadili mtazamo wa wakristu kwa kumtuma paschal mayala kupitia kampuni yake kumrekodi ili watengeneze kipindi maalum ambacho kitalipiwa na ccm na kurushwa star tv, tbc na itv.

Uamuzi huo umefikiwa na kikao cha familia baina ya ridh 1, miraji na bibi na bwana jakaya kikwete baada ya kukubaliana na mtoto mmoja wa askofu huyo na kuelezwa kuwa akaongee na askofu na wao ccm watamlipa.

Baada ya mazungumzo hayo kufikiwa jukumu la kumlipa fedha kulola amekabidhiwa waziri ngeleja mkoani mwanza ambapo jana amewasiliana na askofu huyo kwa faragha na kumkabidhi mzigo wake na leo paschal mayala anasafiri kutoka dar kuja mwanza kwa kazi hiyo ya kutengeneza kipindi maalum.

vipande 30 vya fedha = kulola aka yuda escariot???
 
Back
Top Bottom