Askofu Kilaini: Ndugai jibu hoja

Sijakuelewa kidogo..kwa hiyo Askofu kilaini amemtetea Sumaye ambaye yupo chadema??au Sumaye ambaye yupo CCM..mi naona kama umekurupuka vile ku analyse..mana aliye comment kuhusu posho ni Sumaye mwana CCM damu damu...biased.

mkuu mbona Kilaini yuko straight sana kwani hajaongelea upande wa itikadi ila alichosema kosa la mtu moja halifutwi na kosa la mtu mwingine. Kama bunge lilifanya kosa kwenye posho au la ndugai alitakiwa kutoa ufafanuzi siyo kusema mbona hata sumaye alifanya vivyo hivyo
 
Kanisa limekuwa mstari wa mbele sana ngoja tuone mwisho wake si bure...

Kweli aisee, lipo mstari wa mbele pia kwenye kutoa huduma za afya, elimu na ustawi wa jamii. Ndio maana kule Mafia ambako halipo mambo yapo nyuma sana. Unaonaje twende Mafia mimi na wewe tukaanzishe kanisa ili na wakazi wa huko wapate Maji Safi, Shule za Ufundi Stadi, Zahanati na juu ya yote kumjua Bwana wa Majeshi, Yesu Kristo aliye hai, mwokozi wa dunia?

Should we comrade? For the sake of poor Mafia people who are abandoned by their own government and .......
 
Du! Sasa ni wazi Kanisa linaenda bapaya la ajabu halina hata subira kama ya Rais wetu; Anaona je kama angesubiri warushiane madongo ndio mwisho aseme jambo!!!
 
Nadhani umekosa hoja. jukumu la kiongozi wa dini awe Askofu au Sheikh, ni kukemea maovu yote. Wanasiasa wakiwa wezi lazima wakemewe. kumbuka viongozi wa dini wana wafuasi wegi mno hata kuliko walivyo wanasiasa. Ni heri tukawasikliza tukaacha udini na itikadi za kisiasa.
 
Acha kupindisha hoja wewe. Tunachojadili ni iwapo Ndugai aka Mropokaji alikuwa sahihi au la kumshambulia Sumaye badala ya hoja aliyoitoa halafu wewe umekimbilia kuwahusisha maaskofu na CDM. Ni lini maaskofu walisema waziwazi kuwa wako upande wa CDM acha uchochezi kwa kuwagawa Watanzania kwa misingi ya Udini. Mbona kule Igunga yule mwanamke aitwaye Fatma Kimario alipondondosha mtandio wake viongozi wa dini ya Kiislamu walitoa matamko kuwa CDM hawafai kuchaguliwa kwa kumdhalilisha mwanamke wa kiislamu wakati maaskofu hawakusema kuwa kwa kuwa masheikh wanaunga mkono chama cha magamba na wao wanaunga mkno CDM. Sasa mdini hapo ni nani? Unafikiri kama siasa za udini zingehubiriwa kama unavyodai wewe CCM ingeshinda? Kikwete kachaguliwa na watu wa dini zote na si waislau peke yao. Acha udini wewe.
Maaskofu wanaowashambulia viongozi wanaochemsha ndani ya Serikali nadhani wako sahihi! ila sikubaliani nao pale wanaposhabikia na kutetea kauli za baadhi ya viongozi wa chama kimoja cha upinzani wakati nchi hii ni kuna vyama vingi vya kisiasa! hapa Maaskofu wanaonyesha unafiki kwa kushabikia Chadema tu!!

Tumeshuhudia kila anapoongea kiongozi wa Chadema kumlaumu Kiongozi Serikalini na kujibiwa basi anaefuata kutetea kauli za kiongozi huyo wa CDM anakuwa ni Askofu!!!

Sasa nauliza Maaskofu wao wameamua kushabikia na kutetea Chadema? jee, Mashehe na Maimamu nao wakiamua kuwa upande wa NCCR au TLP itakuwa ni kosa!

Ushauri wangu wa bure kwa Mababa Askofu nawaomba wabaki Makanisani kuchunga Kondoo wao kwani siasa imewashinda kwa kuamua kuwa wasemaji na watetezi wa Chadema!!!
 
Kweli aisee, lipo mstari wa mbele pia kwenye kutoa huduma za afya, elimu na ustawi wa jamii. Ndio maana kule Mafia ambako halipo mambo yapo nyuma sana. Unaonaje twende Mafia mimi na wewe tukaanzishe kanisa ili na wakazi wa huko wapate Maji Safi, Shule za Ufundi Stadi, Zahanati na juu ya yote kumjua Bwana wa Majeshi, Yesu Kristo aliye hai, mwokozi wa dunia?

Should we comrade? For the sake of poor Mafia people who are abandoned by their own government and .......

Lakini mkuu kule imejaa misikiti'ina maana wao hawawezi kufanya hizo kazi?na kama hawawezi matokeo ya wao kujazwa kwenye nafasi nyeti serikali itakuwaje?
 
i am always against viongozi wa dini kujiingiza kwenye siasa hata kama anachokizungumza kina ukweli ndani yake!

Ni katiba ipi inayokataza viongozi wa dini kujihusisha na siasa. Siasa ni sehemu ya maisha ya binadamu. Viongozi wa dini ni binadamu, na wao wanastahili kuishi.
 
Askofu Kilaini: Ndugai jibu hoja Send to a friend
Thursday, 05 January 2012 21:04
0digg
Waandishi Wetu
ASKOFU Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Mhashamu Methodius Kilaini, amemshangaa Naibu Spika Job Ndugai kwa kile alichoeleza kuwa amekwepa kujibu hoja ya msingi ya Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye inayohusu nyongeza ya posho za wabunge, badala yake, ameshambulia kiongozi huyo kama mtu binafsi.

"Sumaye kama mwanadamu anaweza akawa na upungufu mwingi, lakini alichokisema kuhusu posho tujihoji kina ukweli gani? Hilo ndilo la msingi. Alichotakiwa Ndugai ni kufafanua uhalali wa posho na sio kusema aliyetoa hoja hiyo, hana usafi wa kuhoji."

Katika kuonesha kukerwa na kauli ya Ndugai, kiongozi huyo wa kiroho alikemea kauli za baadhi ya wanasiasa kutotaka kukosolewa hata pale wanapofanya makosa na kutaka watu waachwe waseme ukweli bila kuzibwa midomo wala kubezwa.

" Watu waachwe waseme kweli wasibezwe. Kwamba naye (Sumaye) alijiongezea posho, hilo ni jambo lingine ambalo kama anataka (Ndugai), alianzishe mjadala watu wajadili. Lakini sasa tunazungumzia suala la posho za wabunge ambazo sote zinatukera,"alisema Kilaini.

Kwa mujibu wa Askofu Kilaini, si sahihi mtu kujadili hoja aliyoanzisha mtu kwa kuangalia udhaifu wa mtoa hoja. "Hakuna hoja ya msingi katika kumshambulia mtu anayetoa hoja kwa kutumia udhaifu wake, kwani ukweli utaendelea kuwa ukweli na udhaifu wa mtu ni jambo lingine."

Askofu Kilaini alisema: "Nataka watu wajue kwamba hakuna mtakatifu hapa, wote tuna udhaifu, lakini kama mwenzetu kasema ukweli tujadili hoja yake kwa moyo mkunjufu na sio kumpuuza kwa sababu tu eti aliyeongea ana upungufu fulani."

Aliongeza; "Ndugai lazima asome alama za nyakati. Huu sio wakati wa kutetea posho kwani hakuna atakayemwelewa. Watanzania wa matabaka yote wamezipinga sasa yeye akianza kuzitetea atabaki peke yake."

Wanasheria
Kauli hiyo ya Askofu Kilaini, iliungwa mkono na baadhi ya wanasheria waliozungumzia hoja hiyo jana ambao kwa nyakati tofauti walisema kitendo cha Ndugai kuponda maoni ya Sumaye, kimeonyesha kuwa si mtu makini.
Wakili wa kujitegemea, Lupia Augusto alihoji kama Ndungai alikuwepo bungeni wakati sheria ya kupandisha posho za viongozi wastaafu zilizomwezesha Sumaye kujiandalia uzee mwema, kwanini hakupinga. "Iweje aje na hoja hiyo leo?"alihoji.

Augusto alisema tabia aliyoionyesha Ndugai inatakiwa kutafsiriwa kama hakujua majukumu ya ubunge wake wa kuhoji na badala yake, alijua itamnufaisha.Alifafanua kwamba kitendo alichokifanya Ndugai ni ishara kwamba maoni yake yamekumbatia kujinufaisha na sio kunufaisha wananchi.

Alisema Ndugai ameanika udhaifu wake kwani hakuna rekodi zinazoonyesha kwamba alipinga hoja ya kupitisha posho ilipoletwa wakati Sumaye alipokuwa Waziri Mkuu.Augusto alisema kuna kila dalili kwamba kuna mambo mengi yanayofanywa kwa siri kwa maslahi ya wachache na kwamba wanapopingana ndipo mambo hayo hujitokeza wazi.

“Wananchi wajiulize alifanya nini kupinga, maana hapa anaazisha malumbano yasiyokuwa na tija baada ya watu kupinga posho ambazo wabunge wamejipandishia bila kuweka uzalendo mbele,”alisema

Awakera wananchi
Baadhi ya wananchi nao wameeleza kukerwa na kauli ya Ndugai dhidi ya Sumaye na kwamba ni mbinu za kuwatisha viongozi wastaafu wasitetee maslai ya Umma.

Mkazi wa Dar es Salaam, Kimazi Totera alisema Ndugai anatumia Bunge kama sehemu ya kutetea matakwa yake binafsi kwa kuziua kauli za viongozi wastaafu pale wanapotetea maslai ya Umma.

Fatma Haji alisema Ndugai ana siri kubwa kutokana na kuyajua mazingira ya uongozi ya awamu ya tatu kwa kudai Sumaye alijiwekea sheria ya viongozi wa juu wastaafu kulipwa asilimia 80 ya mshahara.
“Yeye kama kiongozi alikuwa wapi kupinga sheria ya viongozi hawa kulipwa kiwango hicho cha pesa ina maana naye ana chuki binafsi, tungemwelewa kama angesema mapema,”alisema Fatma.

Alichosema Sumaye
Jana alipotakiwa kuzungumzia hoja za Ndugai jana, Sumaye alisema," No comment," nataka kusoma na kuelewa vizuri alichokisema kwa hiyo unitafute kesho (leo)."

Kilichoamsha hasira za Ndugai ni kauli ya Sumaye alioyoitoa kupitia kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha ITV, kwamba ongezeko la posho za wabunge linaweza kuchochea makundi mengine kudai kama Wanajeshi, Polisi, Mahakama na walimu nao kutaka nyongeza, hivyo kumweka Rais katika wakati mgumu kufanya uamuzi.

“Mwanasiasa mzuri akifanya jambo akiona limewaudhi wananchi anatakiwa aliache, lakini pia kwenye hili huu mkanganyiko wa Spika na Katibu wake na huu ukimya wa Ikulu ni tatizo, tungependa waseme ili umma ujue hali ikoje,”
alisema Sumaye.

Alisema hatua ya Bunge kujipandishia posho ya kikao kutoka 70,000 hadi 200,000 kwa
siku haliingii akilini na kwamba, inakiuka utaratibu uliowekwa na serikali katika kulipa gharama kwa maofisa wake ikiwa ni pamoja na gharama hizo za fedha za kujikimu.
“Siyo kwamba napinga posho, wabunge wanastahili posho, lakini kwa kweli kujiongezea kutoka 70,000 hadi 200,000 siyo sahihi,” alisema Sumaye.

Alisema wakati yeye alipoteuliwa na Rais Benjamin Mkapa kwa awamu ya pili kushika wadhifa wa Waziri Mkuu, aligoma kwa sababu alikuwa amekwaruzana na wabunge kuhusu nyongeza ya posho.

“Nilimwambia wabunge watanikataa kwa sababu nimegombana nao sana juu ya suala la posho lakini akasema lazima uwe na mimi ndipo nikakubali, lazima hili suala liangaliwe mara mbilimbili…, leo wabunge mmejiongezea kesho jeshi, polisi na walimu nao watataka, tutafanyaje tusifanye mambo ambayo yatamuweka Rais pabaya,” alisema Sumaye.

Alisema posho ni jambo ambalo kwa sasa limekuwa tatizo kwa serikali na kwamba imefika wakati ofisi za serikali zimehamia hotelini, lengo likiwa ni watumishi wa umma kutafuta mwanya wa kulipana posho.

“Ndiyo maana watu wa TRA (Mamlaka ya Mapato Tanzania) wanakusanya fedha nyingi lakini ni fedha kidogo sana zinakwenda kwenye huduma za jamii, nadhani hili ni tatizo na ni utawala mbaya kabisa, lazima kuwepo mabadiliko kama kweli tunataka kuisafisha nchi yetu,” alisema Sumaye

 
Mh Ndugai,kama mbunge mwingine yeyote aliye na uzalendo,mbali na wadhifa wa naibu spika anaoubeba alipaswa kutii utu wake wa ndani.Kauli yenye wito kama vile majeshi ya ulinzi na usalama,walimu,madaktari,mahakama na taasisi zingine nyeti, wakianza kudai nyongeza za posho na marupurupu zisizokatwa/lipiwa kodi(paye)nchi itatawalika?Hiyo ndio maana ya kumweka rais pabaya!
Mapato yanayosemwa kukusanywa na mmt(tra) yatakidhi mahitaji hayo ya taasisi zisizozalisha(service institutions)?
Hakika siamini kama yaliyoandikwa ni kauli toka kinywani mwa Ndugai ninayemfahamu.Ndugai aliyesema 'KAMA NI DHARAU ZAO WAKAZIFANYIE HUKOHUKO'-mjadala wa sakata la wnm:Jairo,Ngeleja,Utouh na Luhanjo!
Ndugai ni tegemeo kwa mzalendo yeyote anaefuatilia mijadala bungeni.
Nahisi kama amekua-misquoted.
Nchi hii haina uwezo kabisa wa kulipa shs 200,000/= kwa siku moja kwa wabunge wapatao zaidi ya 400.Labda kama tunalazimisha nchi ifilisike kabisa.Hilo Ndugai analijua fika.Ndio sababu nachelea kuafiki kwamba analitetea.
 
Hivi Job kiswahili chake si ndo ayubu? Inabidi wazazi wabadilike,majina wanayotoa kwa watoto yameshindwa kureflect tabia na uadilifu wa wenye majina(mitume,mashahidi,watakatifu,manabii n.k) matokeo yake mijitu mijizi,mila rushwa,fisadiz,mibinafsi,yenye uchu,isiyo na utu,miongo miongo,minafiki ndio umechukua majina hayo ya manabii..., ujasiri wa mtu kutetea hizo posho unapatkana iwapo tu roho ya kiutu inaondoka n you remain like a programmable(not logical) machine. Watanzania wanaishi maisha ya nusu jehanam kutokana na umaskin ulokithiri lakin ayubu anatetea wao wajilimbikizie! Askof kilaini ameongea kweli inavyopasa tena kwa falsafa,lakini amin,amin,nawaambieni; mwovu shauri lenye uovu hawezi kuliamua. Ayubu na Anna(jina la bibi yake Yesu kristo) hawayaoni haya na hawawezi kuyaamua
 
Sifa kubwa ya mtu kupewa uongozi ccm ni kuwa lazime uwe na njaa ili uwalambe miguu wanaokuweka kama waandishi wa habari walivyofanya kwa kikwete pale mwanzoni. Sasa ndugai ana sifa hizo ndo maana wamempachika kama spika ili awe anapayuka kama spika ya redio.
 
Acha kupindisha hoja wewe. Tunachojadili ni iwapo Ndugai aka Mropokaji alikuwa sahihi au la kumshambulia Sumaye badala ya hoja aliyoitoa halafu wewe umekimbilia kuwahusisha maaskofu na CDM. Ni lini maaskofu walisema waziwazi kuwa wako upande wa CDM acha uchochezi kwa kuwagawa Watanzania kwa misingi ya Udini. Mbona kule Igunga yule mwanamke aitwaye Fatma Kimario alipondondosha mtandio wake viongozi wa dini ya Kiislamu walitoa matamko kuwa CDM hawafai kuchaguliwa kwa kumdhalilisha mwanamke wa kiislamu wakati maaskofu hawakusema kuwa kwa kuwa masheikh wanaunga mkono chama cha magamba na wao wanaunga mkno CDM. Sasa mdini hapo ni nani? Unafikiri kama siasa za udini zingehubiriwa kama unavyodai wewe CCM ingeshinda? Kikwete kachaguliwa na watu wa dini zote na si waislau peke yao. Acha udini wewe.
Acha kutudanganya, kwani kikwete amechaguliwa? hujui kuwa kaiba kura kwa kutumia usalama wa ccm!
 
Ndugai???..ajibu hoja gani ili hali ni mmoja ya wanafiki wanaotambua nini kinachoendelea huko jikoni kila siku tunaletewa chakula kibichiii

Tatizo hapa ni namna ccm ilivyowekeza kwa watu wasiomakini kwa misingi haswa ya kulindana. akina ndugai ni miongoni mwa wateule wachache waliokithiri kwa unafiki na u yes man (ndiyo mzee). utaona swala la posho kimsingi linaboa sana wananchi, na kwa namna fulani linatoa sura mbaya kwa ccm, na wa-ccm wenzangu wakae wakijua kuna hujuma zidi ya chama kwani waliomadarakani kwa sasa wanajitahidi kujiandalia mazingira ya kupata chao hasa baada ya kuona wameharibu na cdm wanakuja kwa kasi hivyo uhakika wa wao kushika dola ni mdogo 2015. chama makini hakiwezi ktk kipindi kama hiki kuwakera wananchi kizembezembe tu.
 
Ndugai huyu huyu si ndiye alishindwa kujibu hoja ya Tundu Lissu ,akaanza kusema magwanda,NDUGAI HANA SERA za kuzungumuza na wanaume akae pembeni masaburi huyo
 
tofauti ya mawazo ya ndungai na bokassa, mabutu na ngwema ni wote wezi wa mali ya umma isipokuwa ndungai tuu haongei kifaransa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! wewe ona shulke za kata zilivyo duni na chafu katika kila kona. halafu wabunge badala ya kupigania pesa ziende kuboresha shule hizo, wao wanataka revenue zote kutoka madini ua uranium zilipwe kwao!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! ndungai ndiye dakota wa kusema pumba hadhalani!!!!!!!!!!!!!!!

Jamani hawa watu waitwao wabunge, hawana hata uchogo msamaha kwa kiba pesa za umma kijanja namna hivyo?

kulaaniwa na mungu sio tuu kutembea uchi bali pia na kuiba pesa za umma kama ambavyo ndungai anavyotetea!!!!!!!!!!
 
Maaskofu wanaowashambulia viongozi wanaochemsha ndani ya Serikali nadhani wako sahihi! ila sikubaliani nao pale wanaposhabikia na kutetea kauli za baadhi ya viongozi wa chama kimoja cha upinzani wakati nchi hii ni kuna vyama vingi vya kisiasa! hapa Maaskofu wanaonyesha unafiki kwa kushabikia Chadema tu!!

Tumeshuhudia kila anapoongea kiongozi wa Chadema kumlaumu Kiongozi Serikalini na kujibiwa basi anaefuata kutetea kauli za kiongozi huyo wa CDM anakuwa ni Askofu!!!

Sasa nauliza Maaskofu wao wameamua kushabikia na kutetea Chadema? jee, Mashehe na Maimamu nao wakiamua kuwa upande wa NCCR au TLP itakuwa ni kosa!

Ushauri wangu wa bure kwa Mababa Askofu nawaomba wabaki Makanisani kuchunga Kondoo wao kwani siasa imewashinda kwa kuamua kuwa wasemaji na watetezi wa Chadema!!!
hivi Sumae yuko chadema!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom