Askofu Kilaini achemsha kwa ushauri huu!

Loo!! mtu akitaja tu Kanisa Katoliki unaguswa kweli na kuja juu ile mbaya. Badilisha jina basi..

Vyovyote utakavyoona ndio ivoivo..Mimi naona nachangia hoja ila wewe unao uhuru wa kuchukulia kuwa nakuja juu au chini, the choice is yours..

Kuhusu jina langu kama linakukera sana saga vyupa mimi nitakusaidia kukunywesha na safari laga. Jina langu litabakia hivihivi na nikuhakikishia hilo solidly, so mazee we just tambaa.
 
Watu wengi sana wanaanzisha makanisa kwa manufaa binafsi ikiwa ni pamoja na misaada na hizo tax excepmtions hivyo namuunga mkono Baba Askofu kwa ushauri wake kwa Serikali.. Ila kama jinsi alivyouwasilisha ndiyo iliyoleta mushkeli tumsamehe kwa kuwa naye ni binadamu na ana haki ya kukosea na kusamehewa. Cha muhimu tuzingatie alichokusudia kumaanisha kwenye ushauri wake.
 
Naaaam. Uhuru nnaozungumzia uliotolewa na katiba ni wa kuabudu. Utaratibu wa kuandikisha makanisa ni 'formality' tu, si mchujo. Kama katika kuandikisha makanisa/taasisi zingine zitachujwa basi hiki kitendo ni kinyume na kipengele cha katiba kinachotoa uhuru wa kuabudu. Askofu Kilaini anapendekeza moja ya vigezo vya kutokuandikisha taasisi ya dini iwe idadi ya waumini. Kama watu wawili wameamua wanataka kuabudu mawingu na katika hili hawavunji sheria yoyote ya nchi, wanastahili kunyimwa haki yao kikatiba ya kuabudu? Mkuu huoni 'contradiction' hapa?

Natambua Askofu Kilaini, kama mimi na wewe, ana haki ya kikatiba ya kusema analotaka ilimradi hamkwazi mtu.

Mazee, taasisi yeyote ile kabla ya kuandikishwa kwenye vitabu vya serikali inabidi ikidhi vigezo minimum, na hii si kwa makanisa tu. Kila mahali ndivyo ilivyo. Unaposema Kilaini ame-suggest hii criterion ya idadi ya waumini, sina hakika unachosema ni exclusive maana nijuavyo hili si geni na hujathibitisha kuwa hii criterion haikuwepo kabla ya ushauri alotoa.

Suala la kusema kutokuandikisha kanisa ni kukandamiza uhuru wa kuabudu, nadhani hilo ni suala la kikatiba. Mimi sio mtaalamu wa sheria na wala sio policy maker wala decision maker kwenye hii ishu. Ila naamini kikundi chochote kinacho-operate popote lazima kijulikane na kiwe kwenye kumbukumbu za serikali, kwa maana serikali ni muangalizi wetu sote. Vinaandikishwaje, hilo ni suala la utaratibu uliowekwa tayari.Utaratibu una mapungufu au la, hilo ni beyond the scope of this thread.
 
Si vizuri sana kutoa hadharani fact ambazo huna uhakika nazo ndugu yangu......yaani Kanisa lilianza na mitume 12 tu.....Hivi hawa mitume walikuja nyakati gani za historia ya kanisa? Kule kny agano la kale hakukuwa na kanisa?

Confirm facts zako kabla hujazimwaga.....utaharibu ndugu yangu!

Jibu lake ni; kwa kanisa katoliki limeanza kwa mitume. Ref, kanuni ya Imani "....nasadiki kwa kanisa Takatifu Katoliki la Mitume" Ila imani ya kikristo according to the bible imeanza kwa Ibrahimu; manabii, mitume na kisha kristo yaani mpakwa mafuta Yesu na "kanisa la Kristo" limeanza siku Yesu alivyo fufuka nae akawa mzaliwa wa kwanza na kichwa cha wale watakaofuata baada yake.Hiyo congragation ikawa initiated rasmi na roho matakatifu siku ya Pentekoste baada ya Yesu kupaa mbinguni. This is according to Felister's deduction through the Bible sasa mwenye facts zaidi ya hii wanisaidie na ndiyo maana naamini namba sahii ya "kanisa la Kristo" ni mtu mmoja alie anzisha yaani Yesu. Ila sisi tukaanzisha vikundi ili kuwe na utaratibu wa kueleweka katika kuhubiri injili ya Yesu na hapo ndo tatizo likaanza. Naamini leo Yesu akishuka aje kufanya vetting unaweza kukuta haya makundi yetu yote hatakubali kuwa ni kanisa lake ila huko sintopenda kuingia maana ni kazi yake yeye mimi ugomvi uko kwa wale wanaopenda kujifanyia vetting kwamba wao ndo reference point ya huyo Yesu wakitumia vigezo vya akili ambazo ni nywele na kila mtu ana zake.
 
Si vizuri sana kutoa hadharani fact ambazo huna uhakika nazo ndugu yangu......yaani Kanisa lilianza na mitume 12 tu.....Hivi hawa mitume walikuja nyakati gani za historia ya kanisa? Kule kny agano la kale hakukuwa na kanisa?

Confirm facts zako kabla hujazimwaga.....utaharibu ndugu yangu!

Waliokuwa wakiliamini ndiyo hao waliowafukuza hao 12 huko Israel na wakahamia Ulaya.

Niambie hilo agano la kale ni wapi kuna neno KANISA.
 
Mazee, taasisi yeyote ile kabla ya kuandikishwa kwenye vitabu vya serikali inabidi ikidhi vigezo minimum, na hii si kwa makanisa tu. Kila mahali ndivyo ilivyo.

Mpaka hapa tupo pamoja. Sina problem na taasisi kuandikishwa. Tatizo langu ni "mchujo" na vigezo vitakavyotumika.

Unaposema Kilaini ame-suggest hii criterion ya idadi ya waumini, sina hakika unachosema ni exclusive maana nijuavyo hili si geni na hujathibitisha kuwa hii criterion haikuwepo kabla ya ushauri alotoa.

Kuthibitisha kama alichosema Kilaini kilikuwepo au la is besides the point. Msimamo wangu ni kwamba mapendekezo ya Kilaini ni kinyume cha katiba. Period.

Suala la kusema kutokuandikisha kanisa ni kukandamiza uhuru wa kuabudu, nadhani hilo ni suala la kikatiba. Mimi sio mtaalamu wa sheria na wala sio policy maker wala decision maker kwenye hii ishu. Ila naamini kikundi chochote kinacho-operate popote lazima kijulikane na kiwe kwenye kumbukumbu za serikali, kwa maana serikali ni muangalizi wetu sote. Vinaandikishwaje, hilo ni suala la utaratibu uliowekwa tayari.Utaratibu una mapungufu au la, hilo ni beyond the scope of this thread.

This is defeatist thinking. Kama raia wa kutosha wakijitokeza waka weka wazi maoni yao kwamba katiba inakiukwa, basi serikali itabadili msimamo wake. Serikali isiyosikiliza matakwa ya wengi inakua ya kidikteta. Serikali yetu haiko hivyo.
 
Hapana hajamuamrisha mtu. Ametoa tu maoni yake na mimi ninayapinga
.
Naona unaanza kurudi kny mstari....! kula 5
Tujadiliane kwa amani.
Here we go!

Wapi nimemziba Kilaini mdomo?
Rejea post yako niliyoinukuu mwanzoni. Umehoji kwamba Kilaini ana Mamlaka gani ya kuhoji uhalali wa makanisa..... wakati huo huo ukisahau kuwa Kilaini ni raia wa Tz ambaye ana haki sawa na mtz yeyote kuhoji kila kitu kinanachoendelea hapa tz na kutoa maoni yake!....wewe tatizo lako ulikuwa unamchukulia Kilaini kama Kiongozi wa RC na ukaona hayo kama ni maoni ya Wakatoliki...kitu ambacho si kweli!

Kilaini anapohoji uhalali wa makanisa yenye "waumini 200" ana maana gani?

Soma vizuri ile post original.....Kilaini hakuhoji uhalali wa makanisa eti 200.....! hiki kipande kipo pale kama mfano.....katika kuishibisha hoja yake mkuu!

Anataka yafanywe nini?
Well, hoja yake ni kwamba serikali ifanye uchunguzi wa kina kabla ya kuyaandisha makanisa yanayosajiliwa siku hizi kama uyoga.....ili kuepuka kusajili makanjanja ambayo yapo kwaajili ya kutumia fursa zilizopo kujinufaisha. Anachosema..kama ikigundulika ni makanisa ambayo yapo kwaajili ya kujinufaisha binafsi ikiwa ni pamoja nakutumia misamaha ya kodi kwa manufaa yao basi wasiyasajili lakini kama itaonekana kuwa yapo kwaajili ya waumini wao na jamii kwa ujumla basi wayasajili...! Kumbuka si kila asemae bwana bwana.......?

Kiswahili unajua vizuri, ila punguza tu jazba
...ha!ha!ha! sikutaka kuonyesha jazba kny post yangu....sorry kama umenielewa vibaya!
Maswali kwenye post yangu ni 'rhetorical'.
Ha!ha!ha! bro....u not serious.....kama maswali yako ni ''rhetorical'' ilitakiwa ujue na hoja ya Kilaini ina mwonekano huo huo.....vinginevyo utatuchanganya

Sina maana kwamba Kilaini actually ameamua.
Sasa unamkomalia wa nini?

Nnachojaribu kuonyesha ni kwamba ana-contradict katiba
Hapa ndo tunashindwa kuelewana....bro aliitumia haki ya kikatiba kutoa maoni yake ambayo wewe na mimi tunatumia pia now kutoa maoni yetu!

...na at the same time anatetea maslahi yake/ya taasisi yake
. Yes nakubaliana na wewe kuwa anatetea maslahi si ya taasisi yake tu bali ya taifa zima. Kumbuka kama hawa waliopewa misamaha ya kodi wakiitumia kukwepa kodi basi wanaikosesha nchi mapato halali....hivyo maslani ya Taifa yanakuwa at stake. Pili serikali ikigundua kuwa bado kunaupotevu wa kodi kupitia misamaha hii itawafutia wote misamaha hivyo kuwaathili hata wale waliokuwa wanacomply vizuri na sheria....in that matter kama kina Kilaini wanafuata vizuri taaribu basi wataathirika na hapo ndipo maslahi ya taasisi yake yanapokuwa at stake!
 
Mpaka hapa tupo pamoja. Sina problem na taasisi kuandikishwa. Tatizo langu ni "mchujo" na vigezo vitakavyotumika.

Nashukuru kuwa tatizo lako liko kwenye mchujo.

Kuthibitisha kama alichosema Kilaini kilikuwepo au la is besides the point. Msimamo wangu ni kwamba mapendekezo ya Kilaini ni kinyume cha katiba. Period.

Naona tunarudi back to square one. Hivi kutoa maoni imekuwa kinyume cha katiba tangu lini?

This is defeatist thinking. Kama raia wa kutosha wakijitokeza waka weka wazi maoni yao kwamba katiba inakiukwa, basi serikali itabadili msimamo wake. Serikali isiyosikiliza matakwa ya wengi inakua ya kidikteta. Serikali yetu haiko hivyo.

Naamini kuwa katiba sio absolute and exclusive, na ndio maana hurekebishwa, kuboreshwa n.k .. na sipingani na nguvu ya umma kuishape nchi yao through katiba. Tukirejea kwenye mada ni kuwa Kilaini au Gamanywa , sio anayeandika katiba na wala hayupo kwenye mlolongo huo wa kisheria ..so its logical we can leave him out this issue , at least.
 
Makanisa kama yale yaliyojiingiza kwenye DECI wazee ni makanisa kweli au ujanja wa kupata fedha tu kutoka kwa wananchi masikini.
 
Makanisa kama yale yaliyojiingiza kwenye DECI wazee ni makanisa kweli au ujanja wa kupata fedha tu kutoka kwa wananchi masikini.

Labda useme weye pengine utaonekana huiingilii katiba au hutetei maslahi yako binafsi!
 
.

Rejea post yako niliyoinukuu mwanzoni. Umehoji kwamba Kilaini ana Mamlaka gani ya kuhoji uhalali wa makanisa..... wakati huo huo ukisahau kuwa Kilaini ni raia wa Tz ambaye ana haki sawa na mtz yeyote kuhoji kila kitu kinanachoendelea hapa tz na kutoa maoni yake!....wewe tatizo lako ulikuwa unamchukulia Kilaini kama Kiongozi wa RC na ukaona hayo kama ni maoni ya Wakatoliki...kitu ambacho si kweli!

Haya maneno yanaonyesha unashindwa kujibu hoja yangu unabaki kunitungia yako na kisha kuijibu.

Well, hoja yake ni kwamba serikali ifanye uchunguzi wa kina kabla ya kuyaandisha makanisa yanayosajiliwa siku hizi kama uyoga.....ili kuepuka kusajili makanjanja ambayo yapo kwaajili ya kutumia fursa zilizopo kujinufaisha. Anachosema..kama ikigundulika ni makanisa ambayo yapo kwaajili ya kujinufaisha binafsi ikiwa ni pamoja nakutumia misamaha ya kodi kwa manufaa yao basi wasiyasajili lakini kama itaonekana kuwa yapo kwaajili ya waumini wao na jamii kwa ujumla basi wayasajili...! Kumbuka si kila asemae bwana bwana.......?

Nani alizifanyia uchunguzi wa kina Taasisi za dini zilizokuwepo kabla ya mpango wa kusamehe kodi kuanza? Kama kweli inawezekana kufanya uchunguzi ukajua mtu ana nia gani, basi duniani kusingekuwa na uhalifu wa aina yoyote ile. Ni Mungu tu ndo anayeweza kujua mtu ana ajenda gani ya siri.

Yes nakubaliana na wewe kuwa anatetea maslahi si ya taasisi yake tu bali ya taifa zima.

Maslahi ya taifa zima ni kukwepa kodi?

Kumbuka kama hawa waliopewa misamaha ya kodi wakiitumia kukwepa kodi basi wanaikosesha nchi mapato halali....hivyo maslani ya Taifa yanakuwa at stake. Pili serikali ikigundua kuwa bado kunaupotevu wa kodi kupitia misamaha hii itawafutia wote misamaha hivyo kuwaathili hata wale waliokuwa wanacomply vizuri na sheria....in that matter kama kina Kilaini wanafuata vizuri taaribu basi wataathirika na hapo ndipo maslahi ya taasisi yake yanapokuwa at stake!

Ninavyofahamu mimi, jukumu la msingi (Primary objective) la taasisi ya kidini ni kutoa huduma za kiroho. Msamaha wa kodi ulitolewa kwa vitu vinavyotumika kwenye ibada tu kama Koran, Biblia, n.k. Pale taasisi za kidini zinaponufaika na msamaha wa kodi kwa bidhaa zisizotumika katika ibada (mfano vifaa vya ujenzi, magari, n.k) basi zinavuruga mfumo mzima wa kodi. Hii ndo sababu pekee inayopelekea watu kuanzisha taasisi za kidini (haswa makanisa) ili wanufaike na msamaha wa kodi. Serikali inafahamu kwamba njia pekee ya kuzuia ukwepaji wa kodi kupitia misamaha iliyotolewa kwa taasisi za kidini ni kutoza kodi bidhaa zote zisizohusika na ibada.
 
Naona tunarudi back to square one. Hivi kutoa maoni imekuwa kinyume cha katiba tangu lini?

No. Ni wewe mwenyewe ulibaki square one. Mimi nipo square two. Nasema kwamba matamshi ya Askofu Kilaini kwamba taasisi za kidinii zichujwe wakati wa kuandikishwa yanakinzana na uhuru wa kuabudu unaotolewa na katiba.

Naamini kuwa katiba sio absolute and exclusive, na ndio maana hurekebishwa, kuboreshwa n.k .. na sipingani na nguvu ya umma kuishape nchi yao through katiba. Tukirejea kwenye mada ni kuwa Kilaini au Gamanywa , sio anayeandika katiba na wala hayupo kwenye mlolongo huo wa kisheria ..so its logical we can leave him out this issue , at least.

Kama ikipigwa kura ya maoni na Watanzania walio wengi wakaamua hawataki uhuru wa kuabudu, mimi sina tatizo na hilo.
 
Kwangu mimi huu ni Ushauri wa hatari kwa nchi iliyojiwekea misingi ya uhuru wa kuabudu kwenye katiba yake. Yaani watz 200 wakitaka kuabudu wasihalalishwe kuabudu! Idadi gani ni halali?

Ushauri wa Kilaini ni mbovu haukuzingatia ukomavu wa kiuongozi kwa kiongozi mkuu kama yeye kwa sababu zifuatazo:

1.Kwa kiongozi aliyekomaa kiungozi ukidai kitu ukapata inabidi unyamaze usiendelee na kidomodomo.Aliomba kodi iondolewe imeondolewa na serikali ilibidi baada ya kutimiziwa alichotaka anyamaze asiendelee na kidomodomo kwa mtu mkomavu kiuongozi.

2.Utafiti nilioufanya kwa makanisa madogo nchi mbalimbali duniani hukataa kusajiliwa na serikali kwa sababu huamini kuwa Mungu na kaisari (Mtawala) ni vitu viwili tofauti.Na kwa misingi Hiyo ya utofauti wao hulipa kodi zote serikalini kama Yesu alivyowaagiza kuwa mpeni kaisari kilicho chake kaisari (kodi} na mpeni Mungu kilicho chake Mungu (sadaka).Wao hawaigusi serikali na serikali haiwagusi kila mmoja huheshimu mipaka yake.

Sasa serikali ilikuwa inalia ipewe chake wakatoliki hawataki kulipa cha kaisari (kodi) na wanaona fahari kutomlipa kaisari chake (kodi). Makanisa mengi madogo kwa taarifa yake Kilaini hayo anayosema yana watu wachache mengi hayana mpango wa kukwepa VAT. hujenga majengo yao bila kuomba misamaha ya kodi kwenye vifaa vya ujenzi na wala hawana mpango wa kuomba VAT iondolewe.Iwe simenti,nondo,baisikeli,magari,vinanda,magitaa n.k huvinunua na VAT zake hivyo hivyo na hawataki kuomba msamaha wa kodi kutokana na imani yao ya kidini kuwa lazima kodi ilipwe kama Yesu ALIVYOAGIZA.

Labda yeye Kilaini na usomi wake atueleze ni kwa mamlaka gani aliyonayo aweza kataa kulipa kodi wakati Yesu mwanzilishi wa kanisa alilipa kodi.Huo unafuu wa kusamehewa kodi kautoa kitabu gani cha biblia au kaupata wapi? Kama Yesu Alilipa kodi na mitume wake walilipa kodi hadi akafanya muujiza wa samaki ili ipatikane pesa ya kulipa kodi yeye kilaini na papa benedicto ni akina nani wasilipe kodi? Kanisa linalokiuka hata maagizo ya Bwana wao la kutaka walipe kodi na halitaki ni hatari.Napendekeza kanisa katoliki lifutiwe usajili au likubali kulipa kodi kama Yesu alivyoagiza ili liendelee kutambuliwa kama kanisa na si genge la maharamia wakwepa kodi ya VAT waliojificha nyuma chini ya altare ya kanisa ya kugawia sakramenti.

Kushambulia makanisa madogo kayaonea na mimi kama mpiganaji wa porini AMBAYE NI SAUTI KWA WASIO NA SAUTI nasema hapana.Hongereni makanisa madogo ambao huwa mnalipa VAT kwenye bidhaa mnazonunua na ambao hamjawahi kukanyaga serikalini hata kwa mjumbe wa nyumba kumi kujikomba msamehewe kodi ya VAT.Hongereni.Nyie mtaenda huko mnakoita mbinguni na Kilaini na wenzie wataenda gizani jehanamu kwenye kona yenye moto mkali siku ya kiyama kwa kukataa kumpa kilicho chake kaisari(VAT) kama Yesu alivyoagiza.

Kilaini alipaswa ajue kuwa Kutolipa VAT siyo kitu cha kuchekelea kwa makanisa yote kama ilivyo kwa Lutheran,Angilikana,katoliki na hicho kinachoitwa Baraza la makanisa ya wapentekoste cha akina Askofu Mwasota.Kwa makanisa mengi madogo kukataa kukataa kulipa kodi kama VAT ni upotofu wa kiimani.Na ndio maana waliamua KUJITENGA NA kuanzisha yao yenye waumini wachache lakini wenye nidhamu ya hali ya juu ya kulipa kodi zikiwemo za VAT wakipinga mfumo wa kishetani ndani ya makanisa makubwa yaendayo kinyume na Yesu alivyoagiza.

Ni heri kuwa na makanisa madogo yenye watu chini hata ya mia mbili lakini walipa kodi kuliko kuwa na mikanisa mikubwa yenye mamilioni ya waumini lakini hayalipi kodi.kiuchumi ni biashara kichaa.
 
Kwangu mimi huu ni Ushauri wa hatari kwa nchi iliyojiwekea misingi ya uhuru wa kuabudu kwenye katiba yake. Yaani watz 200 wakitaka kuabudu wasihalalishwe kuabudu! Idadi gani ni halali?
.

kwa hiyo wakitokea "akinakibwetele" waachwe tu kwa sababu ya uhuru wa kuabudu,udhibiti muhimu.
 
Makanisa na dini zote zinastahili kulipa kodi bila ulalamishi wala nini. Suala la usajili limeletwa kutokana na serikali kulalamika kuwa baadhi ya makanisa ni makanisa uchwara na yanatumia misamaha isivyo.

Wengine ndo wakashauri serikali iwe makini katika kusajiri hayo makanisa. Hapa nia ni kuiepusha serikali mgogoro wa kusajiri makanisa yatakayotumiwa kukwepa kodi. Huu ni ushauri mzuri. Tatizo ni kutekelezeka kwake. Kuna uwezekano mkubwa wa kuzua lawama ya kuingilia uhuru wa kuabudu.

Wengine wanashauri serikali iwe makini katika kutoa hiyo misamaha, hata kama itasajiri kila kikundi cha kidini bila scrutiny yoyote kwani serikali haina uwezo wa ku-scrutinize uhalali wa taasisi za kidini. Serikali haina utaalam katika mambo hayo. Huu nao ni ushauri mzuri ingawa tatizo la kiutekelezaji vile vile linabaki vile vile.

Tatizo mi naona ni kuyachukulia maoni ya Kilaini kama yalikuwa na maana ya kuifanya serikali ndo iwe muamuzi wa mwisho nani awe dini na nani asiwe. Kama alivyochangia mwingine kuwa ziko taasisi za dini zisizotaka hata hiyo misamaha ya kodi kwa sababu za kiimani. Imani yao inawaambia kulipa kodi ni lazima, kwa nini waombe misamaha?

Tafsiri za maneno au maandishi ya kidini mara nyingi huwa hazifanani ndo maana tuna dini na madhehebu tofauti nyingi sana.

Kwa kuwa kiwango cha ukwepaji wa kodi kimeshafika juu, serikali ifute misamaha yoote ya kodi. Ipunguze viwango vya kodi ili vilipike bila ulalamishi. Ili kuepuka matatizo mengi ambayo tunakutana nayo leo na tutaendelea kukutana nayo ni kuondoa kabisa huu utaratibu wa misamaha ya kodi kwa mtu, kampuni au kikundi chochote.

Ikiwa serikali inampenda sana mtu furani au taasisi furani basi iwape ruzuku au itafute jinsi ya kuwafidia. Lakini kodi ilipwe bila kukwepa au msamaha. Hii itaondoa matatizo mengi sana. Itapunguza mianya mingi sana inayotumiwa na wakwepa kodi wengi. Hili ndo litakuwa suluhisho la kudumu.
 
Let us see what does the law in Tanzania says in respect of worship.

Article 19 (2) of the United Republic of Tanzania's Constitution (1977) clearly states that worship and propagation of a religion is an individual's private affair and therefore the state authority shall not involve itself in the affairs and management of religious bodies.

Have a good one.
 
Serikali inatumia vigezo gani kutambua makanisa? Mtu au watu wakitaka kuanzisha kanisa na kwenda kujisajili serikalini wana takiwa kutimiza vigezo gani? Katika katiba ya nchi Kanisa hasa ni nini kutokana na definition ya katiba?

Mimi nadhani kama serikali imeweka utaratibu mzuri au katiba inaorodhesha vizuri nini kigezo cha kuhesabika na kutambulika kama kanisa basi sidhani kama mtu yoyte au kikundi chochote tu kinaweza kuanzisha kanisa. Tatizo bongo usanii tupu ..........

hapo juu tuko ukurasa mmoja Mkuu...............

Ukiwa na system inayofanaya kazi yake inavyotakiwa.......haya maneno ya huyu Ndugu Kilaini wala yasingekuwa na maana........

....sidhani kama Kilaini kakurupuka tu........he has seen and experienced....who knows.......the ball is with the Government now.........let them take a note!
 
.

kwa hiyo wakitokea "akinakibwetele" waachwe tu kwa sababu ya uhuru wa kuabudu,udhibiti muhimu.

Mwanaluguma, hebu nipe link kati ya ''ukibwetere'' na ''idadi ya waumini + kusamehewa kodi". Sioni.
 
Back
Top Bottom