Cynic
JF-Expert Member
- Jan 5, 2009
- 5,144
- 1,648
Makanisa makanjanja yadhibitiwe – Kilaini
Imeandikwa na Maulid Ahmed; Tarehe: 19th June 2009 @ 10:26 Imesomwa na watu: 230; Jumla ya maoni
Baada ya serikali kusitisha mpango wa kuyafutia misamaha ya kodi mashirika ya kidini na asasi zisizo za serikali, viongozi wa kidini wamepongeza hatua hiyo huku Kanisa Katoliki likiitaka kudhibiti makanisa yanayochipukia kama uyoga ambayo yanayotumia vibaya misamaha hiyo.
Sambamba na hilo, Baraza la Maaskofu wa Pentekoste (PCT) limekiri kuwapo tatizo la kuibuka kwa makanisa yanayojiita ya Pentekoste, yanayosadikiwa kutumia vibaya misamaha ya kodi na kueleza kuwa sasa hivi wanaorodhesha wanayoyatambua na kuyawasilisha serikalini ili kuyabana yanayoibuka kiholela.
Akizungumza na gazeti hili jana juu ya maoni ya kusitishwa kwa misamaha hiyo, Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Methodius Kilaini, alisema yapo makanisa mengi yanayoanzishwa yakiwa na lengo la kuitumia misamaha ya kodi kujitajirisha, hivyo serikali iache kuandikisha ovyo makanisa.
"Unakuta kanisa linaanzishwa likiwa na waumini 200, hilo kanisa gani, wanaanzisha ili wafaidike na misamaha ya kodi…miaka ya tisini, tatizo hilo lilionekana na serikali iliahidi kushughulikia makanisa hayo, lakini leo serikali inayaandikisha ovyo tu na katika muungano wa makanisa hayamo," alionya.
Kwangu mimi huu ni Ushauri wa hatari kwa nchi iliyojiwekea misingi ya uhuru wa kuabudu kwenye katiba yake. Yaani watz 200 wakitaka kuabudu wasihalalishwe kuabudu! Idadi gani ni halali?
Last edited: