Askofu Kakobe; What you are doing is not FAIR! Mungu hapendi

Kwa kakobe kuchelewesha mradi hakuna mtu hata mmoja aliyekufa kwa kukosa umeme, wala hakuna kituo chochote cha kijamii au shule, au hospitali iliyokosa umeme, labda wewe utusaidie kama hayo yametokea ktk eneo ambalo huo umeme ungeenda. Kwanza umeme wa kupitishwa na manguzo katikati ya miji ni jambo lililopitwa na wakati kwani utandazwaji wa nyaya mjini hufanya chini ya ardhi kwa kutumia amad cables. Na kama sio miradi ya kiwango cha chini kuendekezwa Tz, hiyo bara bara ya ubungo mwenge inayopita kwenye kanisa la kakobe ingekuwa imetengewa njia za chini kwa chini za maji safi, maji taka, simu, umeme sisi wenyewe nk. Kuna mradi pia kama wa gas ya songosongo, kule bomba lilikotoka kuja Dar kuwa maji yanayoweza kulilisha jiji kwa zaidi ya miaka 100. Kilichokuwa kinahitajika ni bomba la maji kutandikwa sambamba na lile la gesi hadi Dar, na hivyo kuondoa tatizo la maji dar. Lakini ni nani atafanya hayo kwa ajili yetu kama sio sisi wenyewe? Hebu tuachane na haya maono ya kuku na kuingia katika miradi ya kiwango na inayokidhi haja ya wakati huu. Haya manyaya ya kupitisha juu ni temporarily tu. Kwa nini ilazimishwe kuikosesha serikali na raia wake?
Nakubaliana na wewe mradi unaosema ungekuwa ni bora hasa km unavyozungumza. Je hoja yako ndiyo hoja ya Kakobe? Nini uwezo wa nchi ya dunia ya tatu kufanya miradi ya namna ile. Kumbuka hoja iliyopo mbele yetu ni umeme kuwafikia wananchi. Sasa unashangaza na madai yako kwamba umeme ule hauna maana. (rejea hoja yako, watu wangapi wanakufa kwa kukosa umeme!). Inashangaza km mpaka leo hii hutambui umuhim wa umeme huku upande mwingine ukizungumzia uwezekano wa kutandazwa umeme ardhini. Ni kweli gas inaweza ikapatikana na hata makaa ya mawe kiwira, je hii ndiyo project iliyopo mbele ya macho yetu?
 
Back
Top Bottom