Askofu Kakobe na Upumbafu wa Watanzania

Bazazi

JF-Expert Member
Aug 18, 2008
2,806
3,476
Kama mjuavyo Bazazi ni mzururaji. Katika zungukazunguka yake amekutana na watu wengi ambao wanamuona Askofu Kakobe kuwa ni mtu mtata na wengine kumuona kuwa ni punguani flani. Lakini nilichokiona ni kuwa watanzania wengi ni wapumbafu na wala sio wajinga na wanaburuzika kirahisi sana. >Tafadhalini angalieni nguzo hizo anazolalamikia Kakobe zina umbali gani toka makazi ya raia ilhali WAYLEAVE inayopendekezwa na wataalamu ni mita 7.5 kila upande. >TANESCO ukitaka kuunganisha umeme unalipia waya na mita 463500/= na kama upo umbali wa mita 30 basi utahitaji nguzo ambayo moja wanauza 1,200,000/=. Pamoja na kuwavilipia vitu hivyo bado ni mali ya tanesco.Mtu mwingine ataunganishiwa umeme bila wewe kulipwa angalau kidogo kifidia gharama za nguzo. Bazazi ataendelea kuwa mshabiki wa Askofu KAKOBE na Mchungaji MTIKILA kwani wanatufungua macho acha watu wapumbafu waendelee kuwadharau kwani wamelishwa kasumba/afyuni (mihadharati) na CCM. Aluta continua mapambano bado yanaendelaea
 
....Lakini nilichokiona ni kuwa watanzania wengi ni wapumbafu na wala sio wajinga na wanaburuzika kirahisi sana....

Nakubaliana na wewe kuhusu kuburuzika kirahisi. Wapumbavu.... hapana. Nadhani ni waoga (isipokuwa maeneo machache).
 
Mshbiki tu hakuna kitu! Desparate, unatueleza gharama za kuunga umeme hapa.
Ilibkujenga jengo kubwa la namna ya kanisa la kakobe ni lazima afanye eia. Je y alifanya?
 
mshbiki tu hakuna kitu! Desparate, unatueleza gharama za kuunga umeme hapa.
Ilibkujenga jengo kubwa la namna ya kanisa la kakobe ni lazima afanye eia. Je y alifanya?

unao uhakika akufanya???
Comfirm ur statement pls!!!!!!
 
Je y alifanya?

Swali jibu!!!ama kiswahili nimekosea
je y alifanya??!!!ama y akufanya?
 
Big up Bazazi kwani hata mimi ni muathirika wa janga la Umeme kwani nimenunua Nguzo Tatu na wameniunganishia sasa majirani zangu walipokuja kujenga karibu yangu nao wametumia nguzo hizo hizo zangu nilipoenda Tanesco wamesema hawana Record na nguzo hizo wanachojua ni mali ya Tanesco. Yaani hawa Sisiemu wanatuzingua sana waziri anamsamaha wa kutolipia Nguzo je yeye si mtanzania???
 
Somo moja ambalo nalipata kutoka kwa sakata Zima la Kakobe ni kuwa, Umoja wetu ndio siraha yetu dhidi ya viongozi dhalimu wa hapa Tz........asante Kakobe kwa kutufumbulia macho hawa Watanzania wetu.
 
Kweli watanzania hatujui sheria na haki zetu hatuzijui.Tumezoea kuburuzwa. Angalia kama wakazi wa kipawa,wanalalamika wanalipwa fidia kwa sheria ya mwaka 47! vitu vingi vimeshabadilika unategemea wataweza vipi kupata makazi mapya ?Poor us!
Big up Kakobe!
 
Alah lakini jamani si hata sheria zetu ni za mwaka 47 na wanasheria wetu na wawakilishi wala hizo tume za sheria sijui hazijui kuwa tuna sheria kandamizi haiwezekani ati mimi nilipie nguzo tatu hadi ulokoni kwangu halafu wengine waje eti wachukue bure,nafikiri hili la huduma za tenesiko linahitaji uchambuzi wa kisheria ,hapo mwanzo mi nilikuwa mmoja wa waliokuwa nampinga Kakobe lakini kwenye hii nchi iliyojaa ubabaishaji inabidi kila mtu pale anapoaamini anatendewa si haki basi inabidi ugangamale kwa kila hali,mambo mengi nchi hii yanafanywa kienyeji mno mpaka mtu unashangaa kama si wehu au kama wana akili timamu
 
ukiangali kwa haraka utaona kana kwamba Kakobe ni mpuuzi, kama mimi nilivyokuwa anafikiria mwanzoni. Lakini kuna mtu akanifumbua macho madhara ya umeme mkubwa namna ile pamoja na jinsi inavyotakiwa upite mbali na makazi ya watu. Sasa hivi unakuta bado baadhi ya watu wanapita pale maeneo ya kanisa na kutamani kuwatukana washirika wa Kakobe jinsi wanavyolinda kumbe ni upumbavu ndo unaotutesa wa TZ.
 
Ngoja tusubiri hiyo ripoti ya BICO,si inatoka wiki hii.Japo sina imani nayo hata kidogo.naona kama ndio walewale.
 
Je y alifanya?

Swali jibu!!!ama kiswahili nimekosea
je y alifanya??!!!ama y akufanya?

Hii luga yako uliyitumia hapa inaonekana wewe umetoka shule juzi tu, au uko english kozi, au umenunu simu yako ya kwanza muda sio mrefu
 
Mshbiki tu hakuna kitu! Desparate, unatueleza gharama za kuunga umeme hapa.
Ilibkujenga jengo kubwa la namna ya kanisa la kakobe ni lazima afanye eia. Je y alifanya?


Askofu kakobe amejitolea kukupa darasa namna ya kudai haki yako na kuisimamia lakini naona kichwa yako nzito sana kuelewa, yaani kuna watu hapa wapo wapo tu hawajui wanatoka wapi na wanaelekea wapi.
Yani mtu anaipuka tu kwakuwa amezoea kubururwa anadhani ndio utaratibu au kawaida amka ndugu yangu tupa mbali hiyo blanketi uliyojifunika.
 
Askofu kakobe amejitolea kukupa darasa namna ya kudai haki yako na kuisimamia lakini naona kichwa yako nzito sana kuelewa, yaani kuna watu hapa wapo wapo tu hawajui wanatoka wapi na wanaelekea wapi.
Yani mtu anaipuka tu kwakuwa amezoea kubururwa anadhani ndio utaratibu au kawaida amka ndugu yangu tupa mbali hiyo blanketi uliyojifunika.

Thats my dady! you can say it again.Nadhani kuna umuhimu wa waTZ kusoma somo la sheria na haki zetu za msingi toka primary kama ilivyo kwa kiswahili na hesabu.Nadhani tutaamka.
 
ripoti ilishatoka kitambo na anayo kopi na ndiyo anaikataa wewe upo nchi gani?

Yupo nchini na huna sababu ya kuhoji ndo maana wengine tumeingia JF huku tunakuatana na mambo mengi kama sio yote yaliyo current; mathalan mie sikujua kama BICCO wameingia kwenye hili sakata; Ok tuendleee; hiyo ripoti ya BICCO inaweza kuletwa jamvini tukasoma?

Huenda kuna ukweli mkubwa kwa anachokikataa Askofu Kakobe; na si vibaya Enviromental experts wakajitolea kutuelimisha umma kuhusu hili ilhali sasa limejitokeza lakini naamini litatoa majibu kwa maeneo yote yapitiwa na high voltage kwa nchi nzima!

Tusipende kupuuza kila kitu tu kwa sababu kinatolewa na mtu anayetofautiana nasi kimsimamo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom