Askofu Kakobe Asipuuzwe: Ni kama David Koresh na Camp Davidians!

Kakobe ananguvu sana za mungu,mwaka 2000,aliamua kuitoa ccm madarakani akampigia kampeni mrema nchi nzima,sema tu kura za mrema hazikutosha.
 
Mkuu Hute, kwanza asante kwa kueleza unachokijua kumhusu Askofu Kakobe na sipingani na wewe, pia nakiri kukosea aina ya gari kweli ni Nissan Patrol au Safari, ilionekana kama mpya, labda kutokana na matunzo!. Pia nakiri wengi wa waumini wa kanisa la Kakobe ni matajiri na wana magari, ila wengi zaidi hawana magari na kwenye ule msiba walitembea kwa miguu!.

Naomba nisizidi kumsakama huyu sijui kama ni man of God or man of god!, naomba niwaache wenye imani zenu!, japo sijafanya utafiti rasmi, ila Badra na Ngeleja are reachable!, kama ni kweli umeme pale haupiti, then ndio nitazidi kutishika na kuogopa, kwa sababu Mungu alisisitiza mpeni Kaizari yaliyo ya Kaizari na mpeni Mungu, yaliyo ya Kimungu, umeme ni ya Kaizari!, sababu za kuuzuia usipite hapo, zilikuwa genuine enzi za analojia, sasa ni digitali, hakuna tena interference, sasa huyu ni Mungu kweli anazuia umeme usipite kuwahudumia mamia kwa maelfu ya watu for no apparent justified reasons?!. I doubt!.

Mambo ya katiba ni mambo ya Kaizari, siamini kama ni kweli ni Mungu ndie aliyemweleza Kakobe maneno ya unabii kwenye ule waraka wa vitisho kwa JK, naamini Kakobe atakuwa kaambiwa na mungu, hivyo hakuna chochote kitakacho tokea!, ila pia kama ni kweli umeme pale haupiti, then serikali inazijua nguvu za mungu wa Kakobe, hivyo soon watamuungamia vinginevyo nizo nguvu zilizozuia umeme usipite, zinaweza kukisambaratisha Chama Cha Mapinduzi!.

Zishindwe!.

Pasco


Teh Teh Teh

Mkuu Yani nafurahi sn kuona mambo haya! Eti ccm itasambalatishwa !
 
Teh Teh Teh

Mkuu Yani nafurahi sn kuona mambo haya! Eti ccm itasambalatishwa !
Mkuu Ntuzu, nimefuatilia hoja zako kule, nimekukubali sana. Bwana Wetu Yesu Kristo alituasa "Tafuteni kwanza ufalme wa Mbingu, mengine yote mtapewa kwa ziada!".

Wachungaji wa dunia hii wanaanza kupokea maelekezo ya bwana wa dunia hii na sawa wanawaelekeza wafuasi wao kuwa ule ni ujumbe wa Mungu wao wautafute ufalme wa dunia hii!. Yaani badala ya kumpa Mungu yaliyo ya Kimungu na kumpa Kaisari yaliyo ya Kaisari, wao wanaandika waraka kwa Kaizari na kumsingizia Mungu ati watu wake sasa wautafute ufalme wa Kaisari na kumtishia Kaisari asipowasujudia watausambaratisha ufalme wake!.
Hawa sio watu wa kupuuzwa hata kidogo!.
Pasco
 
Mkuu Ntuzu, nimefuatilia hoja zako kule, nimekukubali sana. Bwana Wetu Yesu Kristo alituasa "Tafuteni kwanza ufalme wa Mbingu, mengine yote mtapewa kwa ziada!".

Wachungaji wa dunia hii wanaanza kupokea maelekezo ya bwana wa dunia hii na sawa wanawaelekeza wafuasi wao kuwa ule ni ujumbe wa Mungu wao wautafute ufalme wa dunia hii!. Yaani badala ya kumpa Mungu yaliyo ya Kimungu na kumpa Kaisari yaliyo ya Kaisari, wao wanaandika waraka kwa Kaizari na kumsingizia Mungu ati watu wake sasa wautafute ufalme wa Kaisari na kumtishia Kaisari asipowasujudia watausambaratisha ufalme wake!.
Hawa sio watu wa kupuuzwa hata kidogo!.
Pasco

Thx Mkuu!

Unajua Mkuu ilikua Ni utamaduni kwa Waisrael akizaliwa tu Wakati akiwa Mdogo anakaririshwa Amri kumi za Mungu, na Km unakumbuka kile kisa cha kijana tajiri na Kiongozi aliekutana na Yesu! Cha kwanza kuulizwa na Yesu zilikua Ni Amri! Kwahiyo Rafiki ya Pasco usitishwe na utitili Wa mafungu ya Biblia hapa! Hawa Ni kawaida Yao kuimba mafungu Km ngonjera! Lkn yote hayo hakuna andiko hata moja ktk Biblia linawarihusu kuchanganya mambo ya Mungu na ya Dunia!
 
Pasco Leo Mkuu nitawaomba hao wanaotetea tuyaangalie maandiko! Na Kikubwa Ninachotaka kuangalia Ni kutokana na waraka Wa Askofu! Kweli Huyo anamwabudu Ni Mungu Wa kweli? Mafundisho yake yako vp mpk tuamini Kua Hiyo Ni Mungu Wa kweli? Maana ktk Yohana Wa kwanza 4:1 tumepewa angalizo juu ya hizi roho! Na ata Mathayo 24 pia!

Kwahiyo Km Uzi huu utakuwepo mpk jioni itakua pouwa Maana saiz naingia ktk Majukumu kidogo!
 
Last edited by a moderator:
Askofu alinyamaza, akaniangalia machoni kwa kunikazia macho kama anahasira fulani, nami nikajisikia baridi ya ghafla nikataka kuanza kutetemeka na kusikia kizunguzungu ile staili ambayo hatimaye watu huanguka chini. Nikajishika imara kwenye kiti, nikwamwambia Askofu, nimeyaondoa maswali yangu yote, hana haja ya kuyajibu tena!. End of interview.
.

...Haa ha ha ha.Ungekomaa nae uone mwisho wake.
 
Unncecessary OVER-ANALYSIS na inalenga kupotosha ukweli. Suala la Waumini wa Kakobe kusimamia kile wanachokiamini ni sahihi kipimwe kwa hoja na sio hizi ad hominem. Vyombo husika vitalifanyia kazi hili suala kwa taratibu zilizopo. Haya mengine ni yenu na ni vyema mkadili nayo wenyewe kwenye vichwa vyenu.
Abdulhalim, sawa unaweza sema hii ni unnecessary and OVER-ANALYSIS, lakini tunapokuja kwenye mustakabali wa binadamu hizi hizi unnecessary over analysis ndizo zinazotupa majibu ya mambo magumu kibinadamu.
Alichokisema Philemon kina ukweli pia kwani waumini hao hao wa Kakobe wanapokesha nje na kuumwa mbu kisha wakapata maleria watahitaji huduma za afya, sasa usifikirie hili halina athari kwa namna moja ama nyingine. Wakati mwingine tunailaumu serikali bure kwa kushindwa kuihudumia jamii ilihali ni sisi wenyewe wana jamii ndio tunasababisha matatizo tena kwa ukaidi wetu wenyewe.
Mwana JF mwingine amenukuu vizuri tu maandiko "Zipimeni kila roho zinazoliitia jina la Bwana kwa kuwa sio zote zatoka kwake..." Lakini pia hayo hayo maandiko yanasema "Siku hizo wataibuka manabii wa uongo na kuwapotosha wanadamu kwa mafundisho yao..." Vile vile maandiko yanasema " Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa..."
Mi sikwambii kwamba Kakobe na wengine wengi ndio hao wanaosemwa na maandiko lakini nakupa rai tu uyapime yanayosemwa nao na ukiona yana ukweli kwako, basi fuata. Kupanga ni kuchagua ndugu yangu. Lakini tusivunje sheria za nchi au kuzuia huduma zisiwafikie wananchi "individual interests" na mambo mengine ya namna hiyo kwa kisingizio cha Imani, mimi naamini kwa hilo hata huko mbinguni halikubaliki.
 
hao watu hukaa hapo mchana na usiku,kina mama kwa kina baba,kwa vijana.swali ni je,wanafanya kazi zao saa ngapi?na hao kina mama wanakaa na waume zao saa ngapi?ndio maana watu husema wafuasi wa kakobe ni masikini,sababu mtu analala na kushinda kanisani anafanya kazi saa ngapi?na kamwe hukuti wale wenye magari wanakesha hapo na kushinda hapo,ni wale pangu pakavu tia mchuzi kama mimi,ukimwona na kiatu soli imekaa upande,wanatia huruma kwa kweli,tena wengine ni vibibi!!!!!

hatumsemi vibaya,ila ni kweli serikali inabidi iingilie katui kama ilivyofanya kwa wale waumini wa kwenda ulaya bila passport kwa IMANI.kama ni haki yao wanafuatilia kwanini serikali isiwapatie ili kuokoa hawa wananchi na mateso???pale nje pana baridi na mbu wakali!!!!!!!
Mi nakwambia Princepesa, tunaangamia kwa kukosa maarifa. Hivi unategemea ukawa na familia imara na thabiti kwa kushinda na kulala kanisani? Unategemea utakuwa na amani katika ndoa yako kwa kukesha kanisani? Uchumi wako binafsi na wa familia yako utaongezeka vipi ikiwa wakesha hapo? Huku ni kuendelea kutiana umaskini jamani.
Tutabaki kulalama ooh mke wangu hatulii.. mara mume wangu ana kimada... watoto hawasikii.. kumbe chanzo ni sisi wenyewe.
 
Nimemkumbuka Askofu Kakobe, ni mwaka 2010 nilishauri mtu huyu asipuuzwe!.

Paskali
 
mama yangu na baba yangu hadi sasahivi wanasali kwa kakobe, wamesali pale miaka mingi sana. mimi nilipokuwa kijana sijaondoka kwa wazazi wangu nilisali kwa kakobe miaka mingi sana. ninamfahamu kakobe mno, walokole ni wengi, na wachungaji wao wana nguvu kubwa, utaona mwakani kama wachungaji wa PCT wakiamua kupiga kampeni dhidi ya ccm, ndio utawajua. kumbuka kipindi cha kikwete walokole waliwaambia waumini wao kuwa kikwete ni chaguo la Mungu na walokole walimpa kura kikwete. wakiambiwa ccm ni adui wa Mungu hawataipigia kura hata mara moja.

walokole wamesahaulika, walokole tz they make something like 10 million population kwasasa.

wachungaji wa PCT wana makanisa karibia kila kijiji cha tz, na analosema askofu dsm ndilo litakaloenda hadi kijijini kaabisa.
Nafanya kumbukizi, ni kweli walokole walipokuwa 10 milioni by then, walisahaulika, jee sasa watakuwa wangapi, na jee wamekumbukwa?, ni kweli walisahaulika sana, afadhali Askofu Kakobe ametukumbusha kuwa walokole nao, japo hawavumi lakini wapo. Sasa mtakumbukwa, nasikia Askofu Kakobe anatafutwa!, nasubiri kwa hamu nisikie wakimkamata, watamuhoji kuhusu nini, maana wakimuudhi, akitoka na kuwaambia waumini wake kuwa "ccm ni adui wa Mungu hawataipigia kura hata mara moja", ila 2020...

Paskali
 
Kwa lugha nyingine, Nguvu za Askofu Kakobe zimewahypnotize waumini wake kwa kiwango cha juu, kiasi kwamba, chochote atakachowaambia wafanye, watafanya, ndivyo ilivyokuwa kwa David Koresh na wafuasi wake wa Camp Davidians na Askofu Kibwetere na wafuasi wake ambao mwisho wao wote waliishia kuteketezwa kwa moto na kujilipua kwa mabomu kwa ahadi ya safari ya mbinguni kwenye uzima wa milele, imewadia!.

Huu uandishi mwingine btwn the lines???. Unafanya tuhuma za reja reja au macho yangu?


hypnotize
ˈhɪpnətʌɪz/
verb
past tense: hypnotized; past participle: hypnotized
  1. produce a state of hypnosis in (someone).
    "a witness had been hypnotized to enhance his memory"
    synonyms: mesmerize, send into a trance, put under, put out, put to sleep
    "a witness had been hypnotized to enhance his memory"
    • capture the whole attention of (someone); fascinate.
      "she gazed down, hypnotized by the swirling tide"
      synonyms: fascinate, entrance, beguile, spellbind, hold spellbound, enthral, transfix, be unable to take one's eyes off, captivate, bewitch, enrapture, grip, rivet, absorb, magnetize; More
      informalbowl over, knock out
      "they were hypnotized by the dancers"
      antonyms: bore
Translate hypnotized to
Use over time for: hypnotized
 
Nafanya kumbukizi, ni kweli walokole walisahaulika sana, afadhali Askofu Kakobe ametukumbusha kuwa walokole nao, japo hawavumi lakini wapo. Sasa mtakumbukwa, nasikia Askofu Kakobe anatafutwa!, nasubiri kwa hamu nisikie wakimkamata, watamuhoji kuhusu nini, maana wakimuudhi, akitoka na kuwaambia waumini wake kuwa "ccm ni adui wa Mungu hawataipigia kura hata mara moja", ila 2020...

Paskali
Mayalla kwa taarifa yako Kakobe sasa kwishney tembelea makanisa yake TZ mengi yamefungwa nilikuwa Mtibwa kanisa lake limekuwa gofu hakuna waumini hata hapo Mwenge waumini wamepungua sana na kwa kuwa ameanza kucheza na moto naamini very soon utamchoma kwelikweli.
 
Nafanya kumbukizi, ni kweli walokole walipokuwa 10 milioni by then, walisahaulika, jee sasa watakuwa wangapi, na jee wamekumbukwa?, ni kweli walisahaulika sana, afadhali Askofu Kakobe ametukumbusha kuwa walokole nao, japo hawavumi lakini wapo. Sasa mtakumbukwa, nasikia Askofu Kakobe anatafutwa!, nasubiri kwa hamu nisikie wakimkamata, watamuhoji kuhusu nini, maana wakimuudhi, akitoka na kuwaambia waumini wake kuwa "ccm ni adui wa Mungu hawataipigia kura hata mara moja", ila 2020...

Paskali
Atakae mhoji asije kuking'ang'ania kiti kama wewe na hapo ndo ukawa mwisho wa mahojiano te te te ....
 
Wanabodi,
Saa hizi ni Saa 8:39 za usiku!, yaani usiku wa manane, nimepita nje ya kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, la Askofu Zakaria Kakobe, nikashuhudia mamia ya waumini wake wamekaa kwenye viti na meza nje ya kanisa hilo huku limepambwa na disco lights zinazobadilika badilika rangi, kwa mgeni aweza dhania ni night club fulani.

Nimeshauri asipuuzwe kwa sababu mimi ni mmoja ambaye ninatoa ushuhuda jamaa ana nguvu, yaani he has powers! Niliwahi fanya nae mahojiano miaka ya nyuma, nikamuuliza hiyo daraja ya Uaskofu alipewa na nani?. Alijibu na Mungu mwenyewe!. Nikauliza kuhusu tuhuma mbalimbali zinatupwa kwake na watu wa mataifa, zikiwepo yeye kuwa tajiri wakati waumini wake wako kwenye umasikini uliotopea, kuhusu Mkewe kuwa ndio Mweka hazina, kuhusu kama hayupo inawekwa kanda kuhubiri.

Na swali la mwisho nilimuuliza kuhusu ukweli kuwa waumini wake wanavuliwa dhahabu na anaziteketeza kwa moto, nikamuomba angalau anionyeshe lilipo hilo tanuru nishuhudie smelted gold deposits kwa macho yangu mwenyewe.

Askofu alinyamaza, akaniangalia machoni kwa kunikazia macho kama anahasira fulani, nami nikajisikia baridi ya ghafla nikataka kuanza kutetemeka na kusikia kizunguzungu ile staili ambayo hatimaye watu huanguka chini. Nikajishika imara kwenye kiti, nikwamwambia Askofu, nimeyaondoa maswali yangu yote, hana haja ya kuyajibu tena!. End of interview.

Huu ni uthibitisho tosha kuwa Askofu Zakaria Kakobe ananguvu fulani, hivyo sio wa kupuuzwa.

Kitendo cha kuwaona waumini wake kwa mamia, wanalala macho usiku kucha kwa kumsikiliza Askofu wao akiwaamuru kuhakikisha wanaipinga serikali in the name of God, ninaamini hao walala nje, wanalala macho hapo nje kwa imani 100 kwa 100 kuwa huko nako ni kumtumikia Mungu Baba na sio kumtumikia binadamu mwenye jina la Askofu.

Kwa lugha nyingine, Nguvu za Askofu Kakobe zimewahypnotize waumini wake kwa kiwango cha juu, kiasi kwamba, chochote atakachowaambia wafanye, watafanya, ndivyo ilivyokuwa kwa David Koresh na wafuasi wake wa Camp Davidians na Askofu Kibwetere na wafuasi wake ambao mwisho wao wote waliishia kuteketezwa kwa moto na kujilipua kwa mabomu kwa ahadi ya safari ya mbinguni kwenye uzima wa milele, imewadia!.

Kama kuna yoyote ambaye ni muumini ama aliwahi kuwa muumini akatusaidia sisi akina Tomaso, kwa kutupa ushuhuda wa msingi wa nguvu za Baba Askofu Zakaria Kakobe kama ni za Mwanga au za giza ili nasi tumuaminiye na tumfuate, vinginevyo huyu ni mtu mwenye nguvu za ajabu na siyo wa kupuuzwa hata kidogo!.

David Koresh wa Camp Davidian alipuuzwa hivi hivi, Joseph Kibweteere nae alipuuzwa hivi hivi, kilichofuata sote tunakijua.

NB. Mode, hii siyo ya dini na imani, ni ya politics of religion.

Paskali
Mungu akusamehe bure.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom