MaxShimba
JF-Expert Member
- Apr 11, 2008
- 35,772
- 4,054
MWANGALIZI Mkuu wa The World And Peace Organization (WAPO) International, Askofu Mkuu Sylvester Gamanywa, amesema huduma za Hakuna Lisilowezekana anazoziongoza, hazina wasiwasi kuhusu afya ya Rais Jakaya Kikwete kwa kuwa kila siku humweka katika maombi maalumu.
Aidha, amesema vifo katika umri mfupi miongoni mwa jamii, ni matokeo ya athari mbaya za mmomonyoko wa maadili ambao jamii haina budi kupambana nao kwa nguvu zote.
Askofu Gamanywa, alisema hayo juzi katika mahafali ya tano ya Shule ya Msingi na Awali ya Shalom, iliyopo katika Manispaa ya Temeke ambapo wahitimu 25 wa shule ya msingi na 50 wa shule ya awali, walitunukiwa vyeti na zawadi mbalimbali.
Akizungumza baada ya sherehe hizo, Askofu Gamanywa alisema mwaka 2005 wakati Rais akizindua kampeni ya Bora Subiri au Tosheka Naye, inayoendeshwa na huduma hizo katika mapambano dhidi ya ukimwi, walimpa ngao itakayomlinda hadi akamilishe kipindi cha uongozi wake.
Ngao tuliyompa kule BCIC Mbezi, ni ishara kwamba kwa Mungu hakuna lisilowezekana na pia, kila siku iendayo kwa Mungu, sisi tunaliombea taifa na rais tunamwombea tukimtaja kwa jina kabisa. Dua na sala zetu tunaamini Mungu anazisikia na zitamwezesha afya njema hadi amalize kipindi chake cha uongozi na kustaafu, alisema.
Hivi karibuni, Rais Kikwete aliishiwa nguvu na kukatisha hotuba yake wakati akihutubia katika maadhimisho ya miaka 100 ya Kanisa la African Inland Church kwenye Uwanja wa CCM, Kirumba jijini Mwanza.
Baadaye, daktari wake, Dk. Peter Mfisi, alisema hali ya afya ya rais si jambo linalowatia shaka wala kuwanyima usingizi yeye na mwenzake Dk. Maohamed Janabi kwa kuwa hana maradhi yanayoweza kumuathiri katika kulitumikia taifa.
Alisema Rais Kikwete ana maumivu ya shingo yaliyotokana na kuumia akiwa utotoni na wakati wa ujana na pia, ana damu nyingi kiasi kwamba, huipunguza kupitia Benki ya Damu (WB) kila baada ya miezi sita.
Katika mahafali hayo, Askofu Gamanywa alisema vifo vya watu wengi katika umri mdogo kutokana na ukimwi, dawa za kulevya, ukatili na mauaji ni matokeo ya taaluma nchini kutotoa kipaumbele katika suala la maadili.
Alitahadharisha kuwa, endapo jamii haitaunganisha nguvu toka serikalini, wazazi, walezi na vijana katika kuimarisha maadili, ipo hatari jamii ikashuhudia machafuko na athari nyingi za mmomonyoko huo.
Alisema mmomonyoko huo unachangiwa na kukua kwa teknolojia ya habari na mawasiliano kiasi cha kuwashinda wazazi kudhibiti mambo wayaonayo watoto na vijana katika mtandao wa kompyuta zikiwamo picha za ngono, vita, mauaji na ukatili.
Mkuu wa shule hiyo, Mwassa Jingi, alisema duniani pote, elimu ya msingi ndiyo haki pekee ambayo mzazi ana wajibu kuhakikisha mtoto haikosi na anaipata kwa kiwango kinachokubalika. Awali Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Hilda Ivatti, alisema kwa miaka miwili mfululizo, shule hiyo imekuwa aikifaulisha wanafunzi wote katika darasa na kuwa miongoni mwa shule kumi bora kitaaluma katika Mkoa wa Dar es Salaam.
FreeMedia