Leo nilikuwa nasikiliza Redio wapo 98.0FM, Gamanywa ametangaza kuongea na waandishi wa habari hapo keso kuhusu mambo ya uchaguzi mkuu, kwa maana ya kuingizwa udini kwenye uchaguzi wa mwaka huu.
Nimjuavyo Gamanywa ni rafiki sana wa KIKWETE, siku chache kabla ya kampeni kuanza alikuwa mgeni rasmi kanisani kwake mbezi sijui alikuwa anafungua nini, kwenye maelezo yake kikwete alijinadi jinsi alivyowasaidia kwenye mgogoro wa uwanja wa kanisa hilo mpaka wakaumiliki, may be aliwalipia, vilevile Gawanywa ni mteule wa Rais Kikwete kwenye tume ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI.
Je Askofu huyu anaweza kweli kuongea akiwa huru bila kuegemea CCM ili kulinda kibarua chake na kulipa fadhila kwa kusaidiwa ile ishu ya uwanja? Maana alishaanza kuponda dhana ya baadhi ya Wachungaji wenzake kutangaza kufanya ibada jumamosi ili kupisha siku ya jumapili watu wawe huru kupiga kura.
Je tutegemee la maana hapo keszho? Karibu mchangie wana jamvi