Askofu awaasa Watanzania kumwombea Rais Kikwete

Kadogoo

JF-Expert Member
Feb 26, 2007
2,073
341
30th January 2011

JKM%2814%29.jpg

Rais Jakaya Kikwete

Askofu Mkuu wa Kanisa la Evangelist Assembly of God, (EAGT), Mosses Kulola, amewataka Watanzania nchini kumwombea Rais Jakaya Kikwete na kuacha kuwasilikiza wanaosema hafai kuongoza kwa sababu ni wahaini wa neno la Mungu.
Aliyasema hayo wakati wa kukabidhi nyumba 15 kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu zilizojengwa na Shirika la Kimataifa la Compassion nchini, (CIT), wilayani Kongwa.

"Muwekeni mbele Rais Kikwete msikubali kuyumba pale na kusema aah sisi hatufai huyu msimsikilize huyo mtu ni haini wa neno la Mungu,"alisema.
Alisema Wakristo wanapaswa kumtii Mungu kwa kumpenda Rais Kikwete anayewajali watu maskini.

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Lembris Kipuyo, alisema maofisa wa serikali wanapaswa kwenda kuangalia nyumba hizo kwa kuwa zimezingatia thamani halisi ya fedha.
"Nilikuwa namshangaa Mungu sana kazi ilivyofanyika, kazi hiyo ilifanyika vizuri sana, nyumba zimejengwa kwa kiwango cha ubora wa hali ya juu kwa kuzingatia value for money (thamani ya fedha),"alisema.

Mkurugenzi wa CIT, Joseph Mayala, alisema shirika hilo limekuwa likisaidia watoto 65,000 walioko katika mazingira magumu kutoka mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Dodoma , Singida, Morogoro, Mwanza, Tabora, Shinyanga, Mara na Iringa.
Alifafanua kuwa mbali ya shirika hilo kuhudumia watoto walio katika mazingira magumu, pia limekuwa likisaidia wanawake wajawazito.
Nyumba hizo zilibomolewa na mafuriko yaliyotokea kati ya Desemba 24 mwaka juzi na Januari mwaka jana, zimegharimu sh. milioni 75.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
 
samahani hizo nyumba zimejengwa na nani kwani inavyoonekana huyo askofu amelewa misaada.ni kweli msaada ni mkubwa ila anatakiwa aangalie maisha ya mtanzania wa leo.jamani napata:target::target:natamani ku:frusty:ila naogopa nisijepata:A S-confused1:
 
atupishe tu wala hafai.....huyu askofu nae vipi?

jamaa hajali watu hasa maskini halafu yeye anakuja na nyimbo kuwa anajali?
 
30th January 2011

JKM%2814%29.jpg

Rais Jakaya Kikwete

Askofu Mkuu wa Kanisa la Evangelist Assembly of God, (EAGT), Mosses Kulola, amewataka Watanzania nchini kumwombea Rais Jakaya Kikwete na kuacha kuwasilikiza wanaosema hafai kuongoza kwa sababu ni wahaini wa neno la Mungu.
Aliyasema hayo wakati wa kukabidhi nyumba 15 kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu zilizojengwa na Shirika la Kimataifa la Compassion nchini, (CIT), wilayani Kongwa.

“Muwekeni mbele Rais Kikwete msikubali kuyumba pale na kusema aah sisi hatufai huyu msimsikilize huyo mtu ni haini wa neno la Mungu,”alisema.
Alisema Wakristo wanapaswa kumtii Mungu kwa kumpenda Rais Kikwete anayewajali watu maskini.

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Lembris Kipuyo, alisema maofisa wa serikali wanapaswa kwenda kuangalia nyumba hizo kwa kuwa zimezingatia thamani halisi ya fedha.
“Nilikuwa namshangaa Mungu sana kazi ilivyofanyika, kazi hiyo ilifanyika vizuri sana, nyumba zimejengwa kwa kiwango cha ubora wa hali ya juu kwa kuzingatia value for money (thamani ya fedha),”alisema.

Mkurugenzi wa CIT, Joseph Mayala, alisema shirika hilo limekuwa likisaidia watoto 65,000 walioko katika mazingira magumu kutoka mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Dodoma , Singida, Morogoro, Mwanza, Tabora, Shinyanga, Mara na Iringa.
Alifafanua kuwa mbali ya shirika hilo kuhudumia watoto walio katika mazingira magumu, pia limekuwa likisaidia wanawake wajawazito.
Nyumba hizo zilibomolewa na mafuriko yaliyotokea kati ya Desemba 24 mwaka juzi na Januari mwaka jana, zimegharimu sh. milioni 75.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

Mhh....,nampa pole sana mzee Kulola,hivi anaelewa CIT ni shirika linalomuwakilisha nani?Kwa nje linaonekana lina nia njema,lakini ukimenya mpaka ganda la sita,jamaa wametanda.Namheshimu sana mzee Kulola lakini awe mwangalifu zaidi.Unayesema ndiye kumbe siye.CIT siye,kaingizwa mkenge.Nahuyo Kikwete anayesema tumuombee anajua ni mtumishi wa nani?Wengine wameshakataliwa!
 
Huyu nae ni fisadi mwingine. Huwezi kumtetea Kikwete kama una akili nzuri, lakini naona sasa wameona kugonganisha imani mbili haitoshi sasa wanataka kuwagonganisha wakristo kwa wakristo.
Tutayaona
 
Huyu Askofu kakosa vitu vya kutuomba Watanzania tuviombee?
 
Jamani msameheni bure Askofu Kulola, yule ni babu haswa! Nafikiri hata hajui nini kinaendelea nchini!! yaani nimechekea na hii sentensi...Alisema Wakristo wanapaswa kumtii Mungu kwa kumpenda Rais Kikwete anayewajali watu maskini. hahahahah! Kikwete anajali maskini!!!!!???????..... Kweli Pole mzee Kulola... na hivi ndivyo mwananchi wa kawaida anavyoelewa juu ya serikali yetu tukufu!..
 
Ikiwa ni issue ya kumfagilia kikwete huwezi kuwasikia hao UVCCM na kina Sheikh nani sijui wanalalamika huyo Askofu kaingilia siasa! Subiri mtu amkosoe uone moto wao...
 
Hivi huyu Bishop anajua EPA, Deepgreen, Meremeta, Tangold, Kagoda, Rada, kiwira, Dowans na Richmond zingejenga majengo mangapi? Mi nadhani wakristo tumwombe Mungu aingilie kati wizi huu wa fedha zetu kabla ya kuanza kumuombea huyu jamaa ambaye anajijua ni dhaifu lakini bado anataka kutuongoza na kuwazuia wenye dhamira ya kweli kushughulikia hizo issues.
Kwa kuwa namheshimu huyu Bishop namshauri akae kimya asiamshe hasira zetu vinginevyo hebu amsaidie kwanza kutoa maelezo ya kwa nini hachukui hatua juu ya wizi huo wa wazi kabisa na ambao wahusika wanajulikana dhahiri kabisa.
 
Hivi kweli nimekosa wa kumwombea hadi nimwombee huyu? Mh, sala nyingine zitamsumbua tu Mungu!
 
Ikiwa ni issue ya kumfagilia kikwete huwezi kuwasikia hao UVCCM na kina Sheikh nani sijui wanalalamika huyo Askofu kaingilia siasa! Subiri mtu amkosoe uone moto wao...
Sheikhs & UVCCM:
Ukimfagilia= Poa, hujaingilia siasa
Ukimkosoa= Vipi tena, siasa na dini, UDINI huu!
Conclusion : Shame on you Sheikhs & UVCCM
 
Huyu askofu avue magwanda aingie kwenye siasa. Ila sio vibaya kumuombea raisi wa nchi.
 
Kuna ajali nyingi sana zinatokea kila siku ni lini itampata Moses Kulola apumzike maana kichefuchefu anachonipa nimsikiapo huwa siku yote inaharibika
 
Huyu ndugu anatuona watz ni wapumbavu nini?hivi yeye haoni udhaifu wa jk ktk kuongoza taifa hili,madudu yote yanayofanywa na serikali yeye hayajui!Vipi hali ngumu ya maisha,vp uduni wa huduma za jamii,vp rushwa na ufisadi,hayajui haya!ningemuona ana busara kama angetuasa tumuombee ili akubali kuachia madaraka na ampishe atakayeweza kazi hii.
 
Hivi huyo Askofu anatoka pori gani? Mara hii tu amesahau kwamba Kikwete anao ulinzi wa majini? Tumuombee ulinzi kwa Mungu yupi tena? Askofu amuulize kwanza Sheikh Yahya iwapo yuko tayari kuingiliwa katika kazi yake...
 
huyu askofu anatafuta namna ya kuishi.badala ya kutuambia tumpende na kumuhesshimu mungu anatuam bia tumueshimu mtu anaelindwa na majini. nadhania nae nikulola manunuzi.kelele zote anaafuta namna ya kumuwini huyu mgonjwa!!!!!!!!!!!!!!!!!!! ha ha ha haaaaa!!!!!!!!!!!!!!!! tumekustukia siji tena kanisani kwako.
 
mmh...Hawa manabii wa siku hizi....sijui kama anakumbuka JK alivyoanguka wakati alivokaribishwa na AIC mwanza baada ya maombi makali.Kolola seek permision from Shekh Yahya
 
Rewind back ur memory way back to 2010 national ellection campaign
 
Back
Top Bottom