Kwahiyo anatupa ushauri gani, wakati tunasubiri hicho kipigo..!!??
Askofu Emmanuel Lazaro wa T.A.G anayehutubia mkutano mkubwa mjini Arusha amebashiri kuwa nchi moja ya jirani itaivamia na kuitwanga Tanzania. Askofu huyo akaitaja kabisa Rwanda na kudai kuwa TZ haitaiweza Rwanda!
Kwani huyo Askofu ana uhusiano gani Rizmoko na Savimbi maana ndiyo wenye ule mzigo.Mwambie akasaidie wenzake wamekamatwa A.kusini na mzigo
Samahani ndugu zangu Wakiristo nawauliza kitu kimoja kutokana na alivyoandika huyu jamaa " HIVI MUNGU WENU ANA MAPUNGUFU NA UPUMBAVU? " pia nimesikia Lema alikuwapo ndani ya mahubiri.
Ushauri kwa waumini wa kanisa lake,wajitahidi kutoa sadaka mana hiyo ni njia mpya ya kudai sadaka
Hivi nani huwa anawapa uaskofu? Maana siku hizi kila mtu anajiita Askofu!
Askofu Emmanuel Lazaro wa T.A.G anayehutubia mkutano mkubwa mjini Arusha amebashiri kuwa nchi moja ya jirani itaivamia na kuitwanga Tanzania. Askofu huyo akaitaja kabisa Rwanda na kudai kuwa TZ haitaiweza Rwanda![ i/QUOTE]
Hapana huyu ni mwongo.
Kazi tunayo na hii yote ni siasa za ugomvi na uonevu za ccm na washirika wake dhidi ya wanyonge, hivyo watu wanamakovu ya uonevu yaliyopelekea uzalendo kupotea kabisa , inakuaje unawanyima watu ajira kisa hawana anayewafahamu kwenye majeshi halafu ukizidiwa wanawarudisha wanao nyuma waliokuwa wamewapa vyeo kwenye majeshi kwa upendeleo ili wamtangulize yule wa mtaani waliyemnyima ajira. Hapo hata mimi siwezi kubaliDah!! ... tulipofikia kunahuzunisha.
Huyu Bishop, aliwahi kutoa UNABII kuhusu Tanzania na Burundi, alizunguka nchi nzima aliitwa IKULU kuelezea hicho alichokuwa anasema ameambiwa na Mungu, akiwa Mbeya Mh Mkuu wa Mkoa Enzi hizo Paul Kimiti , alimwita (Ilikuwa kabla ya kwenda Ikulu) akamwambia yeye (Bishop Lazaro) ni NABII wa uongo na hajatumwa na Mungu aache kuwatia hofu watanzania, Bishop Lazaro akamwambia Mungu ndie aliyekupa nafasi hiyo, na ana uwezo wa kumtoa!! Mh Kimiti alijibu kwamba elimu yake ndiyo iliyompa ukuu wa Mkoa! Nadhani the rest is history!! Kimiti aliyewahi mpaka kuwa Waziri leo si Mkuu wa Mkoa na umaarufu wake kushney!! Huyu Bishop ana Kanisa pale Moshi, hana kashfa yoyote na ana washirika nadhani zaidi ya 4,000!Ninachoweza kusema kwa kifupi tu ni kuwa Mzee Emmanuel Lazaro (Askofu Mkuu Mstaafu wa TAG) ni kati ya viongozi wa dini wanaheshimika sana kwa huduma yao ya kiroho ndani na nje ya nchi. Ni mtu mzima mwenye umri zaidi ya miaka 70 na sijawahi kusikia kashfa katika utumishi wake kwa miaka zaidi ya 30 ambayo nimemfahamu. Tunaweza tusikubaliane na unabii huu aliotoa (maana tunatofautiana sana kwenye mambo ya imani), lakini hatuna pia sababu ya kumtukana, kumdhalilisha na hata kumwita nabii wa uongo au mchungaji wa mshahara kama ambavyo baadhi yetu wanafanya kwenye thread hii. Asanteni kwa kunisikiliza!
hana lolote.he is just seeking popularity.Askofu Emmanuel Lazaro wa T.A.G anayehutubia mkutano mkubwa mjini Arusha amebashiri kuwa nchi moja ya jirani itaivamia na kuitwanga Tanzania. Askofu huyo akaitaja kabisa Rwanda na kudai kuwa TZ haitaiweza Rwanda!