Askofu Anthony Mayalla is no more

"Lakini, msifurahi kwa vile pepo wanavyowatii; bali furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni." Luka 10: 20.

Kazi aliyokutuma Bwana Yesu umeimaliza vyema. Pumzika kwa amani na watakatifu wa Bwana huko Jerusalem mpya.
 
R.I.P bishop mkuu Mayalla na commnity nzima ya Mwanza.

Maane you mean the bishop and the whole Mwanza community should Rest in Peace?

Mungu akulaze pema Baba Askofu. Poleni wafiwa wote yaani familia, jamii ya Mwanza na watanzania wote.
 
kwa wale wote waliosoma seminari za nyegezi, makoko ,sengerema na pia shule zilizo chini ya jimbo kuu la mwanza kama bukumbi, st joseph girls seminary na sumve naamini mtamkumbuka vema baba askofu anthonius mayalla alipenda sana elimu na aliwekeza muda wake mwingi katika suala hili na zaidi ya yote aliwapenda mapadre wake sana na kuwalea vizuri hivyo kupunguza migogoro ya mapadre na askofu wao ukilinganisha na majimbo mengine kweli tutamkosa sana, natoa pole kwa wafuatao pia,FR R.NKWANDE, FR.KUBEJA, FR.NINDILO WALEI WOTE, WASEMINARISTI WOTE, NA WAAMINI WOTE.MUNGU AMLAZE BABA MAYALA MAHALI PEMA PEPONI AMINA.
 
R.I.P Askofu Mkuu Anthony Mayalla! Mungu aliyekupa karama na aliyekuteua kuchunga kondoo wake wa Jimbo Kuu la Mwanza na kabla ya hapo Jimbo la Musoma, yeye mwenyewe akupokee katika makao yake ya milele. Binafsi nakukumbuka sana kwani nimetumikia chini yako na ni wewe uliyenipa sakramenti ya Kipaimara!
 
Ninamkumbuka ArchBishop Mayala kwa suala moja tu. Kuwadharau mapadre wazawa wa Jimbo la Musoma. Hadi leo hakuna Padre MZALIWA wa Jimbo la Musoma amekuwa ASKOFU. Kwa nini?
 
Mwenyezi Mungu Aiweke Pahali Pema Peponi Roho Ya Askofu Mayalla. Amina.

SteveD.
 
Amevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo ameumaliza Imani ameilinda.
Katika mikono ya Mwenyezi upate pumziko la milele baba Askofu.
 
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi na kuwapa nguvu na faraja ndugu, jamaa, marafiki na waumini wote katika kipindi hiki kigumu kwao~AMEN
 
Baba Askofu Mayalla akitoa Kipaimara
Mayalla.JPG
 
Back
Top Bottom