Dilunga
JF-Expert Member
- Apr 8, 2009
- 679
- 49
Kutoka mwanakijiji.com
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki Mwanza Mhashamu Antony Mayalla amefariki duniani. Hadi tunaingia mitamboni hatujajua bado chanzo cha kifo chake. Askofu Mayalla alizaliwa tarehe 23 Aprili, 1940 huko Mwabagole, Kwimba mkoani Mwanza. Baada ya masomo ya msingi na Sekondari na baadaye Useminari alipewa daraja takatifu la Upadrisho tarehe 20 Disemba mwaka 1970.
Aliteuliwa kuwa Askofu wa Musoma mwaka 1979 (miaka tisa tu baada ya upadrisho) na kuwa miongoni mwa maaskofu vijana wa Kanisa Katoliki akiwa na miaka 39 tu. Alisimikwa kuwa Askofu wa Jimbo la Musoma tarehe 22 Aprili, 1979 na Muadhama Kardinali Laurean Rugambwa akishirikiana na Maaskofu James Rubin M.Mafr. na Askofu Renatus Butibubage aliyekuwa Askofu wa Mwanza wa wakati huo. Kufuatia kujiuzulu kwa Askofu Butibubage mwaka 1987, Baba Mtakatifu Yohanne Paulo wa Pili alimteua Askofu Mayalla wa Musoma kuliongoza Jimbo Kuu la Mwanza kama Askofu wake Mkuu Novemba mwaka huo. Alisimikwa kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo la Mwanza 28 Februari, 1988 na hivyo kuanza utawala wa Utume wake wa kiaskofu.
Baada ya kusimikwa kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo hilo Askofu Mayalla alisimamia kwa kiasi kikubwa uhamishaji wa Makao Makuu ya Askofu kutoka Bugando kwenda kilima kingine cha Kawekamo maili chache toka Uwanja wa ndege wa Mwanza.
askofu Mayalla ameweza kusimamia na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo na kichungaji jimboni mwake huku akiongoza kwa kupata waseminari na mapadre wapya, kufungua seminari ya kwanza ya Wasichana Jimboni na vile vile kuendelea kufungua vituo vya afya, shule za sekondari na programu mbalimbali za Afya. Jimbo la Mwanza chini ya Askofu Mayalla limendelea kutoa mojawapo ya mafunzo ambayo kwa muda mrefu yalikuwa yanatolewa Mwanza tu nayo ni yale ya Clinical Pastoral Education ambayo yalikuwa yanahusisha watu wa dini mbalimbali kujifunza jinsi ya kuhudumia wagonjwa.
Wengi watamkumbuka katika maadhimisho ya Misa ya Papa Yohanne Paulo wa 2 kwenye viwanja vya Kawekamo Mwanza na pia katika misa ya kumuaga marehemu Baba wa Taifa huko Butiama ambayo yeye aliiongoza.
Mipango ya mazishi itajulikana baadaye.
Mungu ailaze roho ya marehemu pema peponi, Amina
Thank you man. Angalau Mwanakijiji ana vi detail detail kwenye taarifa zake sometimes, unapata ka biography ka marehemu kujua what kinda man we are dealing with here. Poleni wafiwa, wakatoliki na Watanzania sote.