GAMBLER
JF-Expert Member
- Nov 22, 2009
- 303
- 11
Awali Risasi Jumamosi lilipenyezewa tipu juu ya kuwepo kwa Askofu mmoja (jina tunalo), anayemiliki gari aina ya Hammer inayokadiriwa kuwa na thamani ya ngawira za kitanzania Milioni 250 na ushee ambapo uchunguzi ulianza mara moja na kutengeneza kichwa cha habari hii.
Katika ishu hiyo, baadhi ya waumini walilieleza gazeti hili kuwa, gari hilo analotumia Mtumishi huyo huku akivalia krauni ya uaskofu, likitiwa mafuta ya shilingi elfu thelathini (30,000) haliwaki hivyo humlazimu kuweka wese la shilingi laki tatu (300,000) ili kukamilisha mizunguko yake ya siku moja.
Katika nusanusa ya makachero wetu ilibainika kwamba, mbali na baadhi ya watumishi hao kumiliki magari, majumba na vitu vya kifahari, lakini pia mavazi na mfumo wao wa maisha unawashangaza baadhi ya kondoo wanaowaongoza.
Ilisemekana pia kuwa, mmoja wa viongozi hao (naye jina tunalo), amekuwa akitinga madhabahuni na pamba za mtoko mmoja zikiwa na thamani ya shilingi laki tano na nusu (550,000) huku akitoa ushuhuda kwa waumini wake kuwa, hayo ni matunda ya kumtumikia Mungu.
Katika chimbua chimbua ya hapa na pale, mapaparazi wetu walitonywa pia kuwa, mmoja wa viongozi hao ambaye yeye hujitambulisha kuwa ni Nabii, akiwa katika harakati zozote barabarani hupewa eskoti ya msururu wa magari na vingora kama ule wa rais wa nchi.
Ernest Madewe, ambaye ni muumini wa moja ya makanisa ambayo kiongozi wake yuko kwenye listi hiyo, aliliambia Risasi Jumamosi kuwa, kondoo wa Mungu wamekuwa wakikamuliwa fedha bila kujali umasikini unaowakabili.
Alisema: Kuna wakati tunajaza fomu maalum za kueleza mali tulizonazo ili kuhakikisha tunatoa fungu la kumi linaloendana na kile tulichonacho bila kujali kuwa kuna baadhi yetu tuko hoi na hatuna kitu.
Suala la sadaka linapaswa kuwa siri ya mtu na Mungu wake, lakini kinachoshangaza, jamaa wanakaba kupita kiasi.
Baadhi ya maaskofu, wachungaji, walimu na manabii wanaosifika kwa kutoa huduma ya kiroho vizuri ni pamoja na Onesmo Ndegi wa Kanisa la Living Water kanisa la makuti lililopo Kawe na Mch. Getrude Lwakatare Mama Lwakatare wa Kanisa la Assemblies of God la Mikocheni B, yote ya jijini Dar.
Wengine ni Askofu Zakaria Kakobe wa Kanisa la Full Gospel lenye makao yake makuu pembeni mwa Barabara ya Sam Nujoma, Josephat Mwingira wa Kanisa la Ephata Ministry na Askofu Silvester Gamanywa wa Huduma ya Hakuna Lisilowezekana, nayo ya jijini Dar.
Listi hiyo ndefu inaungwa na Mch. Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufalme na Ufufuo lililopo Ubungo, Anthony Lusekelo Mzee wa Upako wa Ubungo Kibangu na Nabii GeorDavie wa Kanisa la Ngurumo ya Upako lenye makao yake makuu mkoani Arusha.