Askofu aionya serikali ya JK: Ataka iache kudhoofisha upinzani, kulinda amani iliyopo, NEC haifai

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
13 DECEMBER 2011

*Ataka iache kudhoofisha upinzani, kulinda amani iliyopo
*Asema CHADEMA inaongoza kwa umaarufu nchini
*Adai kutoridhishwa na matokeo yanayotangazwa na NEC


Na Gladness Mboma, Moshi

ASKOFU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Kati, Dkt.Thomas Laizer, amesema Serikali ya Rais Jakaya Kikwete isifanye kazi ya
kudhoofisha nguvu ya vyama vya upinzani hasa wakati wa kupiga kura na kama hali hiyo itaendelea, wananchi watashindwa kuvumilia hivyo kusababisha uvunjifu wa amani na utulivu uliopo nchini.

Alisema Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA), kina umaarufu mkubwa kuliko vyama vingine vya siasa nchini hivyo umefika wakati wa Serikali kuviheshimu na kuvipa nafasi vyama vya upinzani ili viweze kufanya shughuli zao bila vikwazo hasa katika chaguzi mbalimbali.

Askofu Laizer aliyasema hayo juzi katika harambee ya kuchangia ukarabati na upanuzi wa kanisa la KKKT Nshara, lililopo Machame, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni za IPP, Bw. Reginald Mengi.

Katika harambee hiyo ambayo ilikwenda sambamba na Jubilee ya miaka 50 ya kuzaliwa kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa na Mbunge wa Hai, Bw.Freeman Mbowe, zaidi ya sh.milioni 200 zilichangwa.

"Kuna watu wanashindwa kutamka wazi kuwa CHADEMA ni chama maarufu hapa nchini, rushwa za kununuliana kanga wakati wa uchaguzi haziwezi kuwafikisha Watanzania popote, miaka 50 ya Uhuru itakuwa na maana kwetu kama tutaondoa chuki kandamizi.

"Kitendo cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutangaza matokeo na kukubaliwa hata kama hayana ukweli binafsi sikubaliani nacho, naomba tujirekebishe katika kipindi kingine cha miaka 50, tusipofanya hivyo amani tuliyonayo itatoweka," alisema.

Aliwasihi Watanzania kudumisha amani na utulivu uliopo sio katika mambo yanayohusu siasa pekee bali hata katika madhehebu ya dini kwa kuhakikisha jambo lolote ambalo litaonekana kufanywa kinyume, litatuliwe kwa mazungumzo.

Alisema Hayati Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kusema kuwa, "Mficha maradhi kilio kitamuumbua" hivyo amani iliyopo nchini itadumu kama haki itatendeka.

Askofu Laizer aliongeza kuwa ni jambo la kumshukuru Mungu kwa Tanzania kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru bila ya mapigano wala umwagaji damu na kusisitiza kuwa, kila Mtanzania awajibike kumuomba Mungu ili aendelee kusimamia amani miaka 50 ijayo.

Alisema maandamano yoyote yanayofanywa na wananchi au vyama vya upinzani kupinga mambo mbalimbali, lazima Serikali ikae chini, ijiulize na kutafuta ufumbuzi wa tatizo badala ya kutumia nguvu nyingi kuyazima na kusababisha madhara.

"Naipongeza Serikali kwa kujenga barabara ambazo awali hazikupitika kirahisi, naomba uboreshaji wa miundombinu uendelee katika kipindi cha miaka 50 mingine ili kuharakisha maendeleo ya sekta mbalimbali," alisema Askofu Laizer.

Mbunge wa Siha, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Bw. Agrey Mwanri, ambaye alikuwepo katika harambee hiyo, alisema Tanzania imepiga hatua kubwa ya maendeleo katika kipindi cha miaka 50 ya Uhuru.

"Ni jambo la kumshukuru Mungu kutufikisha hapa tulipo, nchi yetu inashirikiana vizuri na mataifa mbalimbali duniani, raia wa nchi hizo wamekimbilia nchini kwa sababu ya amani tuliyonayo," alisema.

Kwa upande wake, Bw.Mbowe alisema ujasiri wa kweli ni ule wa kukaa chini na kusikiliza wenzako kile wanachosema ili matatizo yaliyopo nchini yaweze kushughulikiwa.

 
To NEC should be rebuild to be free and fair no member of Chama Cha Mapinduzi as it memeber...
 
Askofu Laizer huyu,wakati mwingine wanawapigia debe Mafisadi,sasa hua sielewi kabisa mbona wanakua vigeugeu hawa Maaskofu kiasi hiki?
 
Askofu Laizer uko sahihi ila kuwa makini utabambikiwa ishu ya madawa ya kulevya sasa hivi,magamba ni noma na hawapendi mtu anayewaambia ukweli na yeyote anayeisifia cdm
 
Ngoja utawaona wenyewe watakuja sasa hivi.

Bila kujali cheo chango, nakubaliana na ulosema.
 

ASKOFU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Kati, Dkt.Thomas Laizer, amesema Serikali ya Rais Jakaya Kikwete isifanye kazi ya
kudhoofisha nguvu ya vyama vya upinzani hasa wakati wa kupiga kura na kama hali hiyo itaendelea, wananchi watashindwa kuvumilia hivyo kusababisha uvunjifu wa amani na utulivu uliopo nchini.

Alisema Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA), kina umaarufu mkubwa kuliko vyama vingine vya siasa nchini hivyo umefika wakati wa Serikali kuviheshimu na kuvipa nafasi vyama vya upinzani ili viweze kufanya shughuli zao bila vikwazo hasa katika chaguzi mbalimbali.

kumbe hata ccm haifui dafu kiumaarufu ikilinganishwa na chadema.....................hili litawachanganya wanamagamba..........
 
Mzee wewe fanya ya mungu na ya kaizari waachie wnaupinzani, unanielewa?!
 
Kama askofu ndivyo alivyosema nadhani hajakosea,kwa sababu
1.Hajasema ni maarufu kumpita nani ,kwa mtizamo wangu hajaonyesha upande mwingine.kwani maarufu vinaweza kuwa vyama vingi tu
2.Hajasema ndicho chama kinachopendwa zaidi na hata angesema hivyo ingekuwa ni kwa mtizamo wake tu.
3.Kuhusu tume,haki ni kweli kabisa lazima yazingatiwe.
 
Mimi niko tofauti sana na mchangiaji hapo juu, Aliyoongea baba askofu laizer yana ukweli kwa asilimia kubwa sana

1.Tume ya uchaguzi ni uchafu unaotakiwa kuondolewa haraka kabla ya 2015
2.Ukiona taasisi za dini zinaingilia siasa ujue nchi imefika pabaya na chama tawala kinatakiwa kikae chonjo kwa sababu mwisho wake unakaribia hata kabla ya 2015 kitakuwa taabani sana,
3. Ni kweli CDM kinakubalika sana sasa hivi kinachowaangusha elimu ya uraia bado haipo vijijini mfano mzuri ni Igunga CCM ilishinda vijijini tu.
4.ccm wanajua kabisa mtaji walionao ni wajinga wengi waliopo nchini(vijijini)
 
Ukweli utabaki kuwa ukweli tu. Taasisi za dini zina nafasi kubwa y akukemea uovu. Wizi wa kura ni uovu unaotaiwa kukemewa na vyombo vyote vya dini( Ukristo na Uislamu na wengine). Dhuluma na vitisho na udanganyifu lazima vikemewe na viongozi wa dini. Tulishakosea huko nyuma hatutakiwi tena turudie makosa yale ayle ili Taifa lisiangamie
 
Kwa hatua CCM ilipofikia haiwezi kusikia kitu na wala tusitegemee jipya...
 
Kwa hatua CCM ilipofikia haiwezi kusikia kitu na wala tusitegemee jipya...

Wamesikia Mkuu,Ila wamesema hawatajibizana na Viongozi wa madhehebu ya dini (Mh.Waziri wa nchi mahusiano Mzee wetu Tyson).Ni kweli Tusitegemee jipya.
 
Wamesikia Mkuu,Ila wamesema hawatajibizana na Viongozi wa madhehebu ya dini (Mh.Waziri wa nchi mahusiano Mzee wetu Tyson).Ni kweli Tusitegemee jipya.

Tyson hawezi kujibu kwakuwa ameambiwa ukweli mtupu. Kwahiyo ameamua kutumia njia hiyo ili liishe kimya kimya. Wakiona liko juu wataibua issue nyingine HOT kama kuundwa upya baraza la mawaziri
 
Ukweli utaendelea kuwa ukweli hata kama utajidhihirisha baada ya miaka 50. Baba Askofu Laizer amezungumza kwa anavyoamini na bila unafiki.
 
Safi sana baba Askofu, wakweli kama nyinyi mpo wachache sana, wengine ni wanafiki tu, wapo kama chaja ya kobe, inachaji kila aina ya betri.
 
Baba Askofu umenena na hatutaki kuwasikia wanaowaambia eti mfanye kazi ya Mungu na ya Siasa waachiwe. Waache kutupotosha kwani waumini wenu ni sehemu ya wananchi na walipa kodo wanaohitaji na kuguswa na mambo yanavyoendeshwa ndivyo sivyo. Ufisadi umeenda mbali umekuwa kansa iliyokomaa kiasi cha kufanya akili za watawala kujeuka about-turn. Hivi inaingia akilini watu kufanya shesere za ukwasi mkubwa (bilioni 64) katika mwezi mmoja wakati wanafunzi wanafanya migomo kwa kutokupewa mikopo; wafanyakzi wakiwemo waalimu hawajalipwa madai yao; vituo vya afya havina dawa na usafiri, maji ya shida, barabara hohe hahe. Zaidi ya kuwapasulia inatakiwa waingie kwenye nyumba za ibada waombewe. Mungu ibariki Tanzania na wabadilishe muelekeo wao.
 
Kama askofu ndivyo alivyosema nadhani hajakosea,kwa sababu
1.Hajasema ni maarufu kumpita nani ,kwa mtizamo wangu hajaonyesha upande mwingine.kwani maarufu vinaweza kuwa vyama vingi tu
2.Hajasema ndicho chama kinachopendwa zaidi na hata angesema hivyo ingekuwa ni kwa mtizamo wake tu.
3.Kuhusu tume,haki ni kweli kabisa lazima yazingatiwe.

Basi hata kuna askofu hapa?? Wote wanaganga njaa tu. Hamuoni wanavyowakaribisha wale wa Mndl kuchangisha fedha!! anatafuta tu namna ya kuzimishwa aache kusema hivyo kwa kupewa f.....e......d.......h.....a......, napita tu wala sichangii hii mada.
 
Back
Top Bottom