Askari watano mbaroni -Dar

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,125
ASKARI polisi watano wa Kituo cha Oysterbay cha jijini Dar es Salaam, wametiwa mbaroni kwa kuhusishwa na kifo cha Octavian Kashita (38) kilichotokea Jumapili wiki iiyopita aliyedaiwa kuhusika katika tukio la utekaji Askari hao wamekamatwa na jeshi la polisi nchini wakituhumiwa kusababisha kifo cha raia huyo katika mapambano dhidi yao.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema kuwa, tukio hilo la mauaji lilitokea juzi katika eneo la Victoria katika nyumba za serikali.

Alisema, polisi hao walikwenda eneo la tukio majira ya saa 1:00 jioni baada ya kupata taarifa kutoka kwa dada wa Bariki aitwae Sia Minja za kutekwa nyara kwa mtu aliyetajwa kwa jina la Bariki Minja.

Kova alieleza kuwa walipofika eneo hilo la tukio walipoelekezwa na huyo dada, waliliona gari aina ya Toyota Prado lenye namba za usajili T 864 BHC ambalo ndilo lililodaiwa kutumiwa na watekaji nyara hao na lkufanikiwa kuwakamata vijana wannne waliosadikiwea kuhusika na tukio hilo.

Alisema walipofanikiwa kuwakamata vijana hao walianza kuwahoji na katika gari hilo walimkuta mateka akiwa ndani ya gari hilo akiwa na watuhumiwa.

Alisema katika mahojiano hayo kulizuka vurugu kubwa kati ya polisi na watuhumiwa hao, na kutokana na vurugu hizo polisi mmoja alifyatua risasi na kumpata mtuhumiwa Octavian na kupoteza maisha papo hapo.

Kamanda Kova alieleza kuwa, katika uchunguzi wa awali uliofanywa na jeshi hilo ulibaini kuwa chanzo cha tukio hilo la utekaji nyara ni ugomvi wa muda mrefu wa kifamilia kati ya familia ya Bariki na familia ya Martha Makishe ambaye ni mzazi mwenzake ambapo walizaa mtoto mmoja.

Uchunguzi huo ulibaini mzozo huo wa kifamilia umefikia kufunguliwa kwa kesi ya madai namba 31 ya mwaka huu, katika Mahakama ya Kinondoni ambapo shauri hilo linahusisha ugomvi kati yao wawili kumtunza mtoto wao aitwaje Kinsley Bariki.

Hata hivyo Kamanda Kova alipotakiwa kutaja majina ya watuhumiwa hao wengine alisema majina hayo hayatwekwa wazi sasa kwa sababu za kipolisi na inaweza ikavuruga upelelezi.

Hata hivyo ilidaiwa katika watuhumiwa hao wanne yumo mwanafamilia ambaye inadaiwa ni mtoto wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Celina Kombani lakini Kamanda Kova hakuthibitisha hilo na kusema ni mwanafamilia tu kutoka katika familia hiyo ya waziri.
NIFAHAMISHE Tanzania news portal .: Habari za Tanzania :.
 
Back
Top Bottom