Askari wa usalama barabarani alieupoteza msafara wa Rais Kikwete ajiua akihojiwa polisi Tarime

Jan 23, 2011
62
13
2010 wakati wa uchaguzi mkuu kuna askari wa usalama barabarani alituhumiwa kuupoteza msafara wa mgombea urais kwa tiketi ya CCM J.M.KIKWETE.Baada ya kukamatwa askari huyu na akiwa chini ya ulinzi akihojiwa inadaiwa aliingia ndani ya gala la kutunzia silaha la kituo kikuu cha polisi TARIME na gala kuu la kanda maalumu ya kipolisi ya TARIME RORYA na kisha kujipiga risasi na kufa papo hapo!!

SWALI
- Je, aliyekuwa akimhoji alichukuliwa hatua gani kwa kosa la kumwacha huru mtuhumiwa aliye chini ya ulinzi wake?

- Je, mtunza stoo wa gala hilo la polisi aliyekuwa zamu siku hiyo alichukuliwa hatua gani kwa kosa la kuruhusu askari mtuhumiwa aliye chini ya ulinzi kuingia galani na kuchukua silaha?

- Je, mkuu wa polisi wa upelelezi alihusika ktk mauaji ya askari huyu ilikupoteza ushahidi wa maelezo ya askari huyo?
 
TUKIO HILI limejaa utata naomba mwenye taarifa kama tume iliunda atwambie nini kilichotokea hadi askari huyo akajiua akiwachini ya ulinzi tena silaha aliichukua galani!!
 
Kwani hawakuunda tume hawa jamaa ? Na si wajua Tume huchukua miaka bila majawabu?
 
2010 wakati wa uchaguzi mkuu.....kuna askari wa usalama barabarani alituhumiwa kuupoteza msafara wa mgombea urais kwa tiketi ya CCM J.M.KIKWETE.......baada ya kukamatwa askari huyu na akiwa chini ya ulinzi akihojiwa inadaiwa aliingia ndani ya gala la kutunzia silaha la kituo kikuu cha polisi TARIME na gala kuula ya kanda maalumu ya kipolice ya TARIME RORYA na kisha kujipiga risasi na kufa papo hapo!!......SWALI (1)............JE? alie kua akimhoji alichukuliwa hatua gani kwa kosa la kumwacha huru mtuhumiwa alie chini ya ulinzi wake................(2)JE.....stookipa wa gala hilo la police .alie kua zam siku hio alichukuliwa hatua gani kwakosa la kuruhusu askari mtuhumiwa alie chini ya ulinzi kuingia galani na kuchukua silaha..!!..........(3)JE.....mkuu wa polisi wa upelelezi alihusika ktk mauaji ya askari huyu ilikupoteza ushahidi wa maelezo ya askari huyo.!!.


Watanzania watu wa matukio.

Inakuwaje tukio la 2010 unatuletea leo tulijadili?

Kesha kufa, uba taka nini tena? Kuwakumbusha waliofiwa? Endelea na current news, ugeni wako usiutumie kuturudisha na kutukumbusha mambo ambayo hata hayana mshiko kwa jamii
 
Habari hii kweli niya mda mrefu sasa lakini katika kumbukumbu za utendaji na uwajibikaji wa jeshi la police kwa matukio 2010 lipo na litakuwepo hadi mwisho wa jeshi letu lapolice nimuhimu watanzania wafahamu ilikuaje ASKARI HUYO WAKIKE ALIE KUA AKIONGOZA MISAFARA YA MAGARI HASA YA MGOMBEA WA URAIS KWA TIKETI YA CCM ajipige risasi akiwa chini ya ulinzi tena kituo kikuu cha police kanda maalumu ya kipolice TARIME RORYA!?
 
Watanzania watu wa matukio.

Inakuwaje tukio la 2010 unatuletea leo tulijadili?

Kesha kufa, uba taka nini tena? Kuwakumbusha waliofiwa? Endelea na current news, ugeni wako usiutumie kuturudisha na kutukumbusha mambo ambayo hata hayana mshiko kwa jamii

Mambo ya kale mkuu yanatupatia mwanga wa kinachotokea leo,yanatuwezesha kuunganisha dots! its worth asking. naunga mkono thread.
 
Hw mafisadi utawaweza? Watakuwa wameshalimaliza kimya kimya.
Na nakumbuka yule askari hakuwa mzoefu sana kwa shughuli yake!

Wenye taarifa zaidi watujuze wajamen!
 
Lahh, hili tukio nalikumbuka sana.

Dada yetu ambaye ndiyo alikuwa kamaliza mafunzo, akapewa kazi ya kuongoza msafara.

Kwa kutokufahamu na ugeni, akafanya makosa na kuupoteza msafara wa Rais.

Wao kama "ETI" aliyemuuwa Kenedy, wakaamua kumpoteza ili kuuwa ushahidi.

Inabidi kila mwaka, siku huyo bibie aliuawa, basi tunaweka kumbukumbu yake hapa JF.

Mungu ampe mapumzisho mema na huku akiwasubiri hao waliomtenda.
 
Ilikuwaje askari mmoja aupoteze msafara wa Rais??? Haiingii akilini. In amana ni yeye alikuwa ametangulia mbele na pikipiki akakosea njia au?
 
Watanzania watu wa matukio.

Inakuwaje tukio la 2010 unatuletea leo tulijadili?

Kesha kufa, uba taka nini tena? Kuwakumbusha waliofiwa? Endelea na current news, ugeni wako usiutumie kuturudisha na kutukumbusha mambo ambayo hata hayana mshiko kwa jamii

Angekufa bibi yako ndo ingekuwa na mshiko eeh?
 
askari alishakuwa na kosa na kihojiwa haruhusiwi kushika silaha ( bunfuki) so Ulikuwa je?
 
Kwa wale wanaokumbuka tukio hilo ni kuwa eti alijipiga risasi tatu kifuani kwa SMG. Jaribu kupata muundo wa smg kisha fikiria alivyo ishika kujipiga risasi mbili kifuani
 
Back
Top Bottom