Askari wa JWTZ auawa kwa ujambazi

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,386
Askari wa JWTZ auawa kwa ujambazi
Send to a friend
Sunday, 11 December 2011 21:03
0digg

Burhani Yakub, Korogwe.
ASKARI wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) wa Lugalo jijini Dar es Salaam ameauawa kwa kuchomwa moto na wananchi wenye hasira baada ya kumakamata akivunja duka la mfanyabiashara wa Kijiji cha Magamba Kwalukonge Wilayani Korogwe.

Askari huyo aliyetambuliwa kwa jina la Amoni Kashalankolo (35) mwenye kitambulisho namba MT.83200 alikuwa katika kundi la majambazi wanne waliovamia duka la mfanyabiashara James Lomwe wakiwa na silaha aina ya SMG yenye risasi saba.Kwa mujibu wa habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Costantine Massawe ni kuwa tukio hilo lilifanyika juzi saa 3 usiku katika kijiji cha Magamba Kwalukonge Wilayani Korogwe.

Watu walioshuhudia tukio hilo walisema, majambazi hao walivamia katika duka la mfanyabiashara huyo na kumtishia kwa silaha huku wakimuamuru awape fedha za mauzo na nyingine zilizopo ambapo waliweza kupewa.

Walisema wakati wa purukushani hiyo, familia ya mfanyabiashara huyo ilipiga kelele za kuomba msaada ndipo wananchi walipozingira nyumba yenye duka hilo ambapo mwanajeshi huyo alifyatua risasi iliyompiga
kwenye paja mmoja wa wanakijiji waliokwenda kusaidia.

“Katika purukushani hizo mjambazi wengine walifanikiwa kukimbia lakini wananchi waliweza kumkamata mwanajeshi huyo na kuanza kumuadhibu kwa kumpiga na baadaye wakamfunga tairi la gari shingoni na kumchoma moto,” alisema Massawe wakati akithibitisha habari hizi.

Kamanda huyo alisema baada ya kupewa taarifa askari walikwenda kijijini Magamba Kwalukonge ndipo wakaanza kufanya msako wa kuwanasa majambazi waliokimbia.Alisema katika msako huo askari wakishirikiana na wananchi waliingia katika msitu wa karibu na kijiji hicho wakakuta pikipiki moja, nguo maalumu za kufunika nyuso pamoja na sare za jeshi la JWTZ.

“Tupo katika msako mkali wa kufuatilia nyendo za majambazi waliotoroka baada ya kufanya tukuio hilo na tunapenda kuwahakikishia wananchi kuwa tutawanasa wakati wowote,” alisema Massaw
 
Duh, hiyo ni kali! bado Polisi hawajikamatwi wenyewe kwa sababu wanajua namna ya kujikwepesha. Lakini mara nyingi ujambazi wa kutumia silaha unakuwa ni mpana.
 
Sio kosa lake mjeshi.ni njaa tu.si kila mtu anatafutia mkate sehem yake ya kazi?ukianza na polisi wa usalama barabarani wanapo waomba ma dereva rushwa huku wakitishiwa kupelekwa polisi. Ni sawa tu na huyo mjeshi kumtishia maisha raia uhai ili apewe chochote cha kumsaidia ktk familia yake ukizingatia wajeshi walipunguziwa kibaba chao (resheni)
 
Back
Top Bottom