Askari wa jwtz aliyetembeza kichapo jang’ombe apandishwa kizimbani

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
Written by Ashakh (Kiongozi) // 18/03/2011 // Habari // 6 Comments

Na Khamis Amani
ASKARI wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wa Kambi ya Bavuai Migombani, amefikishwa mahakamani akikabiliwa na shitaka la kuwashambulia raia huko Jang’ombe wiki iliyopita.
Askari huyo MT 83992 PTE, Emanual Elistile Ngondo (29) mkaazi wa Mombasa wilaya ya Magharibi Unguja, alifikishwa mbele ya hakimu Khamis Ali Simai wa mahakama ya wilaya Mwanakwerekwe, kujibu tuhuma za shambulio la hatari.
Shitaka hilo liliwasilishwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashitaka wa mahakama hiyo Said Mohammed Hemed, Mwanasheria wa serikali kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP).
Katika maelezo yake aliyoyatoa mahakamani hapo, Mwanasheria huyo alidai kuwa, Emanuel Elistile Ngondo, alimshambulia Ali Omar Ngasa kwa kumpiga mikwaju, magongo pamoja na mkia wa taa, tukio lililotokea Jang’ombe wilaya ya Mjini Unguja majira ya saa 9:00 za jioni.
Sambamba na tukio hilo, Mwanasheria huyo alidai kuwa siku hiyo ya Machi 9 mwaka huu, alimfunga Ali kwenye bomba la maji katika kambi ya Jeshi ya Bavuai iliyopo Migombani wilaya ya Mjini Unguja, na kumsababishia kupata maumivu makali mwilini mwake.
Kwa mujibu wa Mwanasheria huyo wa serikali, mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 225 cha sheria namba 6/2004 sheria za Zanzibar.
Mahakama ilipomtaka kujibu madai hayo ya upande wa mashitaka aliyakana na kuomba kupatiwa dhamana, ombi ambalo halikuwa na pingamizi mahakamani hapo.
Pamoja na kukana tuhuma hizo, upande wa mashitaka ulidai kuwa upelelezi wake tayari umeshakamilika, na kuomba tarehe ya kusikilizwa pamoja na kutolewa kwa hati za wito kwa mashahidi.
Kesi hiyo imeahirishwa kwa kusikilizwa hadi Machi 31 mwaka huu, na mtuhumiwa ametakiwa kujidhamini mwenyewe kwa fedha taslimu shilingi 50,000 pamoja na wadhamini wawili wenye vitambulisho, ambao kila mmoja ametakiwa kusaini bondi ya kiwango kama hicho cha fedha.
Hadi mwandishi wa habari hizi anaondoka mahakamani hapo jana, mtuhumiwa huyo alikuwa bado hajatekeleza masharti hayo ya dhamana.na wakazi wa Mombasa znz walisema hawamtaki askari huyo ktk aneo lao na kuomba Serekali ya smz kumfukuza kazi kwa kukosa madili ya kazi ya Jeshi.





6 Comments on "ASKARI ALIYETEMBEZA KICHAPO JANG’OMBE APANDISHWA KIZIMBANI"


  1. 4da667c2cbc29d44b60992ddca86c36b

    Habbeeeesh 18/03/2011 kwa 8:09 mu · Jibu
    Tunapowambia harakisheni Maandamano ya kuvunjwa Muungano munatwambia bado ingali mapema!!! Eti kwanza tusubiri mjadala wa Katiba… Munaona mambo hayo, sisi tulisema mapema ya kwamba, hawa wapigaji watakuwa ni hawa hawa ‘WASHEEENZ’ angalieni majina hayo..


  2. 5ca03c6fd6e2ebea64fec7056ea2a4d8

    mahuluku tabu 18/03/2011 kwa 8:51 mu · Jibu
    NA haina haja ya viongozi wa Zanzibar kushikilia mambo ya mafuta,mpaka hili muungano uvunjwe na ZANZIBAR ieleweke ni nchi na mamlaka yake, eti jeshi la ulinzi,,, hata sheria hawaielewi kama si wahuni ni majambazi ,sio vikosi vya ulinzi, ONLY THE BEST WAS PROOF ENOUGH TO PULVERISE.,……..YOU NEVE GET DIVISION MUCH LESS DE-CEIT.ALLAH BLESS ZANZIBAR


  3. 13e38b498ed5c60336c2c6032e4b7da9

    Ali 18/03/2011 kwa 9:15 mu · Jibu
    kusema kweli Huu muungano Hapa zanzibar unafaida gani vilevile mimi napenda kujua kwani huu Muungano nikule kuangana baina ya Familia mbili au kuungana kwa kua tujuane tu kwakweli siyo hivyo tu
    Mimi kwa upande wangu huu muungano ungepewa heshima yake sawa na Familia mbili pale zinapo ungana kwa upande wa mwanamke na wamwanamme mimi naamin huu nio Muungano wa kikweli kwa sababu lolote litakpotokea upande wowte baina ya pande mbili hizo likiwa zuri au baya basi litajadiliwa napande zote mbili, pia isitoshe kusea kweli Muungano wetu huu hauna faida yeyote ile kwa wazanzibar kwa hiyo Viongozi wakae kitako na kuangalia maslahi ya wazanzibar na siyo ya watanganyika……………… I LOVE EVERY BODY .


  4. b7a77011638f608cff362de6645de3f5

    zamko 18/03/2011 kwa 9:19 mu · Jibu
    Huyo Mwanajeshi kwanza hana asili ya Kizanzibari na ndio maana akafanya anavotaka. Emanuei Elistiles Ngondo hili ni jina la wapi? Sio hao hao WALA WATU wanaojivisha magwanda Mekundu ya damu. Nia yao ni Kuimaliza Zanzibar.
    Wakati Umefika kuvamia vituo vya JWT kwa mabomu ya Mafuta ya Petroli kama vinavovamiwa Vilabu vya Pombe vya Wahazanakki na Malichela.


  5. 352fc700365208232c18e143abfc0fe1

    mchongoma 18/03/2011 kwa 10:50 mu · Jibu
    Wananchi waZanzibar woote watafurahi sana kuwa serikali ya [SUK]] GNU itachukuwa khatuwa munasaba na inayofaa kwa wahalifu kama hawa na baadae kuwasafirisha kule walikotoka!!!!, yaani kuwarudisha makwao kama vile zinavyo fanya NCHI ZOTE DUNIAN.
    Hii itakuwa nifunzo kubwa kwa kila anaye fanya uhalifu, ujambazi na uvunjaji wa amani na utulivu katika nchi na italeta uwelewano muaffka ambao kila mtu atakaa na hisia kubwa ya kustahiyana na kuhishimiana bila ya kuoneana, kwani itokeapo kumuonea binaadamu mwezako?? ndio chanzo chakueneza chuki na kutokuaminiana.
    NAWASILISHA
    MCHONGOMA


  6. 612bbf9095d066a6b2709e700f5e09ec

    CCM-ASP ZNZ 18/03/2011 kwa 11:41 mu · Jibu
    Nilitegemea atashitakiwa yeye na wenzake kwa makosa mengi sana na wala sio moja. Wako wapi wale wengine waliopigwa ? au wao hawahitaji kumshitaki.
    Ninawasiwasi jeshi limemtoa muhanga huyu peke yake ili kuwaficha wengine, na pia inawezekana alishafanya kosa huko jeshini au siku zake za kuhamishwa zimeshawadia.

 
Back
Top Bottom