Askari wa JKT ndani ya STK 3970 aporomosha matusi ya nguoni kulinda msafara wa kiongozi!

Hakuna aliyejibu swali , swali ni Je Jkt wana mamlaka ya kisheria ya Kuwa na msafara barabarani ? Swali la pili , kama mtoa thread alikuwa amekosea Je alikuwa halali kwa wanaosimamia msafara kumtukana.

Maswali haya sioni kama yana ikitikadi ya chama au post za awali alizopost.
 
Asante sana mkuu Ngambo Ngali , kuna watu humu wako eecentric wanafikiri kwa kadri walivyoruhusiwa na chama chao na si vinginevyo.

Matokeo yake wanaonekana kama watu wasio uwezo wa kifikiri na kutoa contribution makini.

Kama nilivyosema hapo nyuma hao ni wa kuwasamehe bure.
 
Badala ya kulalamikia matokeo ungeanza na chanzo kwanza. Kwa nini ulitanua? Hata mie niwapo kwenye foleni huchukua sana madereva wenye tabia mbovu kama yako.
 
Hakuna aliyejibu swali , swali ni Je Jkt wana mamlaka ya kisheria ya Kuwa na msafara barabarani ? Swali la pili , kama mtoa thread alikuwa amekosea Je alikuwa halali kwa wanaosimamia msafara kumtukana.

Maswali haya sioni kama yana ikitikadi ya chama au post za awali alizopost.

Naona bado mpo Great Thinkers mnaofuatilia mambo kwa makini.
Wengine hao kama JanjaWEED,Wozoza na wengine sijui kama wamefuzu hadi kiwango kipi katika kuchambua habari.

In fact, kama ilivyo wanachama wengi wasio makini humu jamvini, wanashindwa kabisa kujipambanua kwa kutoa fikra mbadala.

Kwa kifupi mi naona Mkuu Masopakyindi hakuchukua tahadhari kuovertake magari ambayo ilikuwa inaonekana kama msafara.

Lakini ni vyema viongozi wawe na gari ya polisi mbele na nyuma ya msafara ili uonekane wazi.

Huyo askari aliyetukana, sasa huyo ni kibaka na si askari aliyepitia depot ya mafunzo.
 
Badala ya kulalamikia matokeo ungeanza na chanzo kwanza. Kwa nini ulitanua? Hata mie niwapo kwenye foleni huchukua sana madereva wenye tabia mbovu kama yako.
Kutanua na ku-overtake ni vitu viwili tofauti kabisa.
Kutanua ni kukuta foleni iliyosimama na HAKUNA RUHUSA ya kupita , kwa mfano kwenye junction. Na hili linatokea mijini.
Ku-overtake ni kulipita gari linaloenda kwa mwendo mdogo kuliko wako, hii ni scenario ya barabarani huko mbugani

Hivyo ni vitu viwili tofauti .
 
Kweli humu ndani kuwa wengine wanaharibu maana ya halisi JF "tgt"Anyway pole sana mkuu siunajua vijana wetu wakiwa karibu na mabosi zao wanajifanya wajua kazi kumbe hamna kitu zaidi ya kihelehele tu, kwani mimi sioni sababu ya yule askari kukutusi wakati makosa yalikuwa yao kwa kutokuonyesha ishara ya msafara
 
Hakuna sheria inayozuia ku-overtake (sio kutanua) ila ni muhimu kuchukua tahadhari.

Kwa mazingira uloyataja kati ya rail overpass na daraja la Ruvu si mahali pa ku-overtake hasa kama kuna gari zaidi ya moja mbele na ni usiku.

Kwamba askari akakuporomoshea matusi ya nguoni hilo halivumiliki lakini sitaraji askari wa majeshi yetu kwa sasa awe na tabia tofauti na hiyo.

Ameonyesha watanzania we are too personal, not good at discussing issues ndo maana hata hapa umeishia kuitwa majina badala ya kujadili hoja tarajiwa.

Ushauri: next time kuwa makini na unaendeshaje 100km za mwisho baada ya safari ndefu maana at that stage dereva huwa amechoka. Hii ni moja ya chanzo cha ajali nyingi za barabarani.
 
Ulikuwa msafara wa wenda tuliza maandamano ya Uamsho Mlandizi unajua tena JKT akishaona JW alivyotamba Kariakoo nae kapanda bichwa
Pole mkuu kwa tusi wangekupa cha ncha kali
 
kama wewe ulivyokuja kulalamika kutukanwa, na yeye analalamika kuwa-overtake bila ustaraabu.... na yale maeneo ni mabaya sana kwa ajali.....lakini siku hizi kutukana tusi ni kama kibwagizo tu sawa na ku-overtake bila ustaraabu.!
 
Mkuu sijui kama unaelewa hiyo stori yenyewe.

Kutanua ni kama kuna foleni iliyosimama, na hakuna ruhusa ya kupita e.g. Kwenye intersection.
Mimi nilikuwa na overtake slow moving vehicles, elewe tofauti hiyo.

Kama umeshawahi kuendesha masfa marefu utaelewa situation hiyo, hasa kama umekwisha cover 750km na zaidi.
Kama wewe scope yako ni scenarios za magomeni na foleni za jijini si rahisi kuelewa.
Hayo maeneo unayoyasema speed limit ni 50, sasa wewe utasemaje kulikuwa na slow moving wakati wenzako walikuwa wanatii sheria? na wewe inaonekana ni mgeni hiyo barabara eneo hilo ni hatari sana kwani barabara inakutowa barabara na kukutupa nje kabisa kwa sababu haina kiwango na hasa kama gari yako inatumia matairi myembamba.
 
Namba mbili ni jee hapo ulipo overtake hakuna alama zilizokuwa zinakataza ku-overtake? maana kama speed limit ni 50 kama anavyosema Matola sitegemei kuwa unaweza kuovetake hapo...
 
Last edited by a moderator:
Nisahihishe mkuu, lakini ni kati ya daraja la treni na daraja la mto ruvu.

Usithubutu kufanya tena jambo hili Mkuu, hilo ni eneo hatarishi, ajali nyingi sana zinatokea maeneo hayo kwa kutaka kuyapita magari ya mbele kama ulivyotaka kufanya, ungrvumilia ufike maili moja ndipo uyapite. Ila misafara mwisho ni saa 12 jioni, kumbe unaweza kumshtaki huyo askari asiye na nidhamu ndani na nje ya jeshi.
 
Back
Top Bottom