askari wa Hifadhi ya Selous

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
WAZIRI wa Katiba na Sheria, Celina Kombani,ameuagiza uongozi wa mbuga ya hifadhi ya Selous wilayani Ulanga, kuacha mara moja kuwapiga na kuwafanyia unyama wananchi wanaoingia katika maeneo ya hifadhi, kwa jili ya kuchimba dhahabu .

Waziri Kombani ambaye pia ni Mbunge wa Ulanga Mashariki (CCM), alitoa agizo hilo juzi akiwa katika ziara ya kuwashukuru wananchi kwa kumchagua tena kuwa mbunge.

Agizo hilo lilikuja baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi wa vijiji mbalimbali kuwa wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya ukatili mno vikiwamo vya kuchomwa moto katika sehemu za siri.

Kwa mujibu wa wananchi hao, ukatili huo unafanywa na askari wa hifadhi pale wanapowakamata wakichimba madini ya dhahabu katika maeneo ya Kijiji cha Ketaketa, kilichoko mpakani mwa hifadhi hiyo.

Akiwasilisha malalamiko hayo kwa waziri Kombani, Fadhil Mwingili wa Kijiji cha Mwaya, alisema vijana wengi wanaokwenda katika machimbo hayo, wamekuwa wakiteswa na kufanyiwa ukatili.

Malalamiko kama hayo yalitolewa pia na wakazi wa vijiji vya Luhombero, Ilonga, Iputi na Ketaketa, ambao walisema askari wa Hifadhi ya Selous, wamekuwa wakutesa watu .

Kwa upande wake, Diwani Ketaketa, Rashidi Kachengela, alithibitisha kuwapo taarifa zinazohusu askari hao kuwakamata wachimba madini na kuwatesa vibaya.

Hata hivyo alisema bado kuna utata kuhusu nani mmiliki halali wa eneo lenye madini.Kwa mujibu wa diwani huyo, utata huo ni kati ya Kijiji cha Ketaketa na Hifadhi ya Selous.Kwa upande wake, Kaimu mkuu wa hifadhi, Ramadhani Mkhofoy, alikiri habari kuhusu askari wake, kutumia nguvu za ziada, kuwadhibiti wananchi.

Waziri Kombani alisema tayari ameshawasiliana na ofisi ya ardhi, ili kujua mmiliki halali wa eneo hilo.
 
Back
Top Bottom