Askari Magereza Hii ni Aibu!

Ndallo

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
7,619
4,292
Naamka asubuhi leo tarehe 19 April nakwenda kujinunulia gazeti langu la Mwananchi gazeti hili limepambwa na picha moja kubwa inayoonyesha askari wawili wakike na watatu wakiume wakiwa wamempiga Tanganyika jeki mama mmoja na chini kuna maandishi yanayosomeka: Mtuhumiwa chini ya ulinzi halafu chini yake kuna maneno yasemayo mwanamke akiwa amedhibitiwa na askari magereza wa mkoa wa Morogoro baada yakudaiwa kufanya fujo! sasa kinachonishangaza ni kuwa kweli askari watano kumshika mwanamke mmoja tu? askari wa bongo wanahitaji mafunzo ya ziada sasa.
 
Asante, hata mimi nimeiona picha, kweli ni udhalilishwaji wa hali ya juu, naomba wale wanaofuatilia mambo ya unyanyasaji kama huu waingilie kati mambo kama haya ya aibu kubwa.
 
Nami nimeiona mpk ile nguo yake ya ndani inaonekana.Wanamdhibitije huyu wakati hana hata silaha?Au sifa kwa boss alikuwa karibu.
 
Naamka asubuhi leo tarehe 19 April nakwenda kujinunulia gazeti langu la Mwananchi gazeti hili limepambwa na picha moja kubwa inayoonyesha askari wawili wakike na watatu wakiume wakiwa wamempiga Tanganyika jeki mama mmoja na chini kuna maandishi yanayosomeka: Mtuhumiwa chini ya ulinzi halafu chini yake kuna maneno yasemayo mwanamke akiwa amedhibitiwa na askari magereza wa mkoa wa Morogoro baada yakudaiwa kufanya fujo! sasa kinachonishangaza ni kuwa kweli askari watano kumshika mwanamke mmoja tu? askari wa bongo wanahitaji mafunzo ya ziada sasa.

Kumbe Tanganyika jeki bado inatumika!!!!!!!!!!!!!
 
Huu ni unyanyasaji wa kijinsia! haiwezekani ukamshika mtuhumiwa tena mwanamke kama hivi inaonyesha ni jinsi gani askari wanatoa hukumu bila mahakama.
 
Nadhani haki na wajibu wa mtuhumiwa ni vitu vya lazima hawa maaskari wafundishwe na kuvizingatia.,kuna siku watuhumiwa watakataa huo udhalilishaji..
 
Naamka asubuhi leo tarehe 19 April nakwenda kujinunulia gazeti langu la Mwananchi gazeti hili limepambwa na picha moja kubwa inayoonyesha askari wawili wakike na watatu wakiume wakiwa wamempiga Tanganyika jeki mama mmoja na chini kuna maandishi yanayosomeka: Mtuhumiwa chini ya ulinzi halafu chini yake kuna maneno yasemayo mwanamke akiwa amedhibitiwa na askari magereza wa mkoa wa Morogoro baada yakudaiwa kufanya fujo! sasa kinachonishangaza ni kuwa kweli askari watano kumshika mwanamke mmoja tu? askari wa bongo wanahitaji mafunzo ya ziada sasa.

Je askari magereza ana mamlaka ya kumuweka mtu chini ya ulinzi? Do they have the power to arrest.

Nadhani hawana mamlaka hayo, huyu mama anaweza kufungua kesi na kupata pochi ya kutakata. Sheria inawapa mamlaka ya delea na wafungwa tuu na si vinginevyo
 
...Kibaya zaidi ni kuwa mwanamke anadhalilishwa na askari mwanamke. Sad.
 
Naona wanafuata mkumbo tu, sababu pale walikuwepo askari karibu 5... sasa nikashindwa kuelewa lengo la "tanganyika jeki" ni kuudhihirishia umma kuwa tumemkamata, au ni kumuweka chini ya ulinzi ili asikimbie!??
Ni ulimbukeni mwingine kwa maafande wetu!
 
hivi INAKUWAJE HUKO NDANI MAGEREZANI?, KAMA HAPA NJE URAIANI MBELE YA MACHO YA WENGI INAKUWA HIVI????????? *NAULIZA,HIVI RAIS,NA W/MKUU HUWA WANAYASOMA MAGAZETI HAYA???
 
Kweli Asante, kweli inauma na sijui huko walikompeleka huenda hata walimfanyia vibaya. My God ona mambo hayo.
 
Hana adabu kivipi, na kama kakosa, watumie njia sahihi za kumkamata mtu bana.
 
Back
Top Bottom