Askari Magereza anapolinda usalama mkutano wa Kampeni.

Indume Yene

Platinum Member
Mar 17, 2008
2,950
711
Watanzania wengi tumekuwa na mazoea ya kuwaona askari magereza wakisindikiza wafungwa mahakamani, kulinda wafungwa mahospitalini n.k

Hapa hali ni tofauti, sijui hapa huyu askari magereza alikuwepo kwa ajili ya kuangalia usalama au kumsikiliza Mh. Zitto.
Angalia picha na toa maoni.
4.JPG

5.JPG
 
Attachments

  • Magereza2.JPG
    Magereza2.JPG
    74.6 KB · Views: 95
  • Magereza.JPG
    Magereza.JPG
    48.4 KB · Views: 86
Aah wapi huyu alikuwa anasikiliza sera tu. Anajua anachokifanya sema kosa kutinga kwenye hizo yunifomu za kikazi. Yuko kimaslahi zaidi kuliko kulinda usalama.
 
Hao jamaa pembeni ya maaskali ndo wajumbe tosha kabisa wa mabadiliko. Hawadanganyiki, wala hawana chama lakini wanataka mabadiliko.
 
Aah wapi huyu alikuwa anasikiliza sera tu. Anajua anachokifanya sema kosa kutinga kwenye hizo yunifomu za kikazi. Yuko kimaslahi zaidi kuliko kulinda usalama.

Mkuu nakubaliana na wewe, hapa alikuwa anasikiliza sera kwa makini ila ameharibu kutinga na gwanda. Jamaa asipoangalia wanaweza kumdondoshea kitumbua chake. But demokrasia ndiyo hiyo, waache watu wachague viongozi wao wanaowapenda na si kuwachagulia au kulazimisha wachague chama fulani.
 
Aah wapi huyu alikuwa anasikiliza sera tu. Anajua anachokifanya sema kosa kutinga kwenye hizo yunifomu za kikazi. Yuko kimaslahi zaidi kuliko kulinda usalama.

Mpaka angeenda nyumbani kubadilisha nguo angepitwa na uhondo maanake alikuwa anatokea kazini!
 
wote wameguswa na hotuba ya Mh. Kabwe, duh lakini jamaa anaonekana BETA FIMBO maanake hata troza inapwaya kimtindo ndo' maisha ya watumishi wa kulinda usalama wetu.
 
Inafurahisha kuona maaskari wote ktk mkutano ule (polisi, wa kike na kiume, mgambo na mjela) walivyo makini kusikiliza. Naamini nao wanatamani mabailiko. Hawadanganyiki pia
 
Aah wapi huyu alikuwa anasikiliza sera tu. Anajua anachokifanya sema kosa kutinga kwenye hizo yunifomu za kikazi. Yuko kimaslahi zaidi kuliko kulinda usalama.
Hapana mkuu, huyo ask. magereza, alitokea mbali sana ili amsikilize mkuu Dr. Slaa, hivo hilo vazi analitumia ili akwepe kulipa nauri! cimnajua afande akiwa kwenye gwanda halipi nauri?
 
Huyo sio wa ''Panic Security Company'' kweli?...majeshi yetu yana kapelo siku hizi?

Kilichonishangaza zaidi ni nguvu alizonazo huyu afande mwenye V3 kuchanganya nguo za kiraia(kapelo) na za kijeshi. Enzi zetu huyu akirudi kambini ni ex.drill mpaka ana -:A S-cry:
 
Alitaka kukaa mbele ikabidi avae jezi kama wanapoenda kuangalia mpira pale Taifa. We unafikiri hapo wanalinda? Hao wansikiliza sera tu
 
Wakuu ninajitahidi kupasua mbavu zangu kwa comments zenu.
Huyo jamaa ni magerza askari na hapo alikuwa anamsikiliza rais wa sita wa tanzania.
 
Siyo kuwa kuna wafungwa wamekuja kwenye kampeni na yeye kaja nao?
 
Japo kuwa kura ni siri!! huyu bwana yuko wazi kabsaa, kura kwa mbunge wa chadema ila kwa rais anajaribu kuubeep mkutano umpatie t-shit ya chadema vinginevyo kura itakuwa
kwa chechemee, anataka sanduku liongezeka wanduguu??:bowl:
WANASIKILIZA KWA UCHUNGU SANA HADI HURUMA
 
Back
Top Bottom