Askari kutolipa nauli inanikera

Sina hakika kama ni sheria au mazoea kwa askari wetu,jeshi,polisi,magereza,zima moto na uhamiaji huwa hawalipi nauli hasa kwenye dala dala wanapoenda /kurudi kazini au kwenye shughuli zao zingine ili mradi tu wana sare zao,papo hapo wafanyakazi wengine,hata wenye vipato vidogo na wanafunzi wanalipa kama kawaida.Je ni kwamba kazi zao ni muhimu sana kuliko za wengine au ni kuwaogopa?

Hakuna sheria inayowapa mamlaka ya kutokulipa nauli, mambo wanayoyafanya ni wizi kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri.
 
Back
Top Bottom