Askari kutolipa nauli inanikera

Ulimakafu

JF-Expert Member
Mar 18, 2011
29,043
10,687
Sina hakika kama ni sheria au mazoea kwa askari wetu,jeshi,polisi,magereza,zima moto na uhamiaji huwa hawalipi nauli hasa kwenye dala dala wanapoenda /kurudi kazini au kwenye shughuli zao zingine ili mradi tu wana sare zao,papo hapo wafanyakazi wengine,hata wenye vipato vidogo na wanafunzi wanalipa kama kawaida.Je ni kwamba kazi zao ni muhimu sana kuliko za wengine au ni kuwaogopa?
 
si sheria bali wanaogopwa, aidha kutokana na hilo wanalilazimisha wao wenyewe (askari) hadi limezoeleka
 
si sheria bali wanaogopwa, aidha kutokana na hilo wanalilazimisha wao wenyewe (askari) hadi limezoeleka
Hapana si kwamba wanaogopwa. Suala hili lilipitishwa wakati wa Rais Mwinyii kutokana na madai kuwa vipato vyao ni vidogo na wanawatumikia wananchi. Well huu ulikuwa ni ujinga wa hali ya juu. Maana wenye magari hawasamehewi kodi na wala hawapewi sub-sidy yoyote. Kuna wakati nilikuwa UK, wazee above 60 years na walemavu wanapanda vyombo vya usafiri bure, lakini serikali ilikuwa inafidia gharama zile. Kwahiyo hawa wenye magari wangekaa wakajadiliana na serikali aidha wawape watumishi wao pesa ya usafiri au wawapunguzie nafuu ya kodi au sub-sidy kwenye mafuta ili wapate nafuu kwenye biashara. Vinginevyo dhana ya ujariamali inakuwa haina maana.
Tena mbaya zaidi unaweza kumkuta askari anasimamisha basi au hata gari ili amwombee jamaa yake lift.
 
Enzi zile za mabasi ya UDA kuna kipindi kuliibuka kundi la vibaka wa kutisha ndani ya mabasi wakiwaibia wasafiri, serikali ikatoa pendekezo kuwa askari polisi wapande bure mabasi ya UDA ili wawe wanawadhibiti vibaka wasiwaibie wasafiri.

Kipindi kile kilipopita maskari wote wakageuka kuwa ndio vibaka wa kutolipa nauli. Kimsingi hakuna sheria yeyote inayomlinda askari hawa wasilipe nauli endapo wamiliki wa vyombo vya usafiri wataamua kukataa na kuwafungulia mashitaka.

kama wanafunzi wanalipa kwa nini polisi wasilipe.
eti bwana .na wao(njagu) fulltime wanakula hela za wauza gongo,bangi na unga jumlisha na vibaka uchwara,tena mi naona hao njagu na jamii yao walipe mala mbili au laaa! !!!!bbwawe na usafiri zao uwezo wanao ajili wanachakachua hela na hiyo miunga yenyewe ndo wahusika wakuu wa fo sale, vile wanadaigi ni ushahidi lakini mmmmmmm?waweza skia imekamatwa kg 5 lakini kizimbani zikaja 0.000001 mpoooo?!
 
Walipe kama ni kazi,mbona mwl ni mfanyakazi wa serikali na analipa nauli...!?au mwl kpato chake kinatosha m nadhan hii nchi si democratic state ila ni millitary state...!
 
Nasema hivi,haya yote sisi ndo tunayalea yote haya.Uwe wizi mnabadirisha wizi eti ufisadi.
Askali wote inabidi walipe nauri kama watu au wasafiri wengi.Mambo hiyo yakome haraka. Hivi niulize kwenye ndege nako hawalipi??
 
Back
Top Bottom