Askari ajitoa uhai kwa kuupoteza msafara wa Kikwete Tarime!!!

You have a point,nilikuwa nazungumzia uwezekano wa mtu kujiua kwa SMG,maana kuna watu wamekataa kuwa haiwezekani mtu kujigeuzia hiyo bunduki.Dhidi ya hapo,mimi sikuwepo eneo la tukio na wala sijui aina ya bunduki iliyotumika,sawsawa na hao wanaosema inawezekana kuna mtu kamuua huyo dada.nadhani umenielewa

Hassan unaweza kujipiga risasi ngapi moyoni kabla hujafa?
 
mungu aipe nguvu familia yake... inasikisisha sana kupoteza askari

lakini lazma kuna makosa ya kiufundi hapo, kwanza kupoteza msafara, pili kuwa mahabusu akiwa na silaha, nk. nk.

RIP

Mkuu DN,

Kwa sasa tunaiombea familia ya SUZY iwe na nguvu ili wavuke kipindi hiki kigumu. Pili kuna makosa mengi sana ya kiufundi hapa... inakuwaje mtu aliyewekwa mahabusu ajiue, alipata wapi silaha??!!! Pili taarifa zinasema alijipiga risasi nne upande wa kushoto kifuani pake... well we are know ali-aim moyo wake... the question come, unahitaji kujipiga risasi ngapi ili ufe katika moyo?

IGP Mwema, fanya utueleze ukweli kuna kingine ambacho hakisemwi sawa hapa!!!
 
Je, alikuwa ni mzoefu, au mgeni, au hajawahi kuongoza msafara? Mimi uona hapa Dar misafara uongozwa na polisi wa pikipiki pamoja na 'golf'/ landrover freelander', sasa je yeye alikuwa akiongoza kwa pikipiki? Usalama wa taifa walikuwa wapi kutoa maelekezo yote na programu nzima ikiwemo 'route' ya kupita? Hivi alitumia bunduki au bastola?

Isije kuwa ni namna ya kufuta ushahidi!!??
 
Labda hii itaweza kutoa mwanga zaidi

"Kitendo hicho kiliwachukiza viongozi na kuamuru kukamatwa na kuwekwa
mahabusu kwa askari huyo. Wakati akiwa mapokezi ghafla alichukua bunduki aina ya SMG na kujimiminia risasi tatu na kukata roho papo hapo," kilisema chanzo hicho.

Source: Mwananchi newspaper.

RIP Suzana

Wakuu which should be a trusted source?
 
Polisi ajiua kwa kuupoteza msafara wa Rais Kikwete,AJIPIGA RISASI AKIWA RUMANDE Monday, 05 July 2010 07:47

Anthony Mayunga, Tarime
Mwananchi

SAA chache tu baada ya msafara wa Rais Jakaya Kikwete, kuingia katika Kanisa a Anglikana, ili kuhudhuria sherehe za kuwekwa wakfu Askofu, askari polisi wa kike WP Suzana, amejiua kwa kujipiga risasi baada ya kuwekwa mahabusu kwa kosa la kuupoteza njia, msafara wa Rais.

Habari zilisema tukio hilo lililogeuka kuwa gumzo katika mji huo, lilitokea saa 8 mchana wa jana, katika Kituo cha Polisi Tarime, muda mfupi baada ya askari huyo kuwekwa chini ya ulinzi.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Tarime, Dk Charles Samson, alikiri kuupokea mwili wa askari huyo na kwamba alijipiga risasi upande wa kushoto wa kifua.

Kwa mujibu wa Mganga huyo, risasi hiyo ilipenya na kutokea nyuma ya bega.

"Ni kweli amejiua kwa kujipiga risasi ambayo imetokea nyuma ya bega. Kwa ufupi ni kwamba eneo hilo ni sehemu ya moyo, nimemfanyia uchunguzi wa awali na
kuthibitisha kuwa amekufa,"alisema.

Alisema taarifa kuhusu tukio hilo alizipata akiwa katika msafara wa Rais na kwamba alipokwenda kumfanyia uchunguzi marehemu, alibaini kuwa alikata roho muda mfupi,baada ya kujipiga risasi.

"Kitaalam kilichosabaisha kifo ni risasi maana nimefanya uchunguzi na kubaini, nasubiri uchunguzi mkubwa tukiwa na polisi ili tuwakabidhi maiti kwa ajili ya hatua nyingine,"alisema kwa masikitiko.

Chanzo hicho kilidai kuwa askari huyo ni miongoni mwa askari polisi waliotoka chuoni hivi karibuni na kwa hiyo si mzoefu.
... Baadhi ya wananchi wakizungumza na Mwananchi walisema hayo ni matatizo ya matumizi ya nguvu ndani ya jeshi[COLOR]



Alipotakiwa kuzungumzia suala hilo kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi katika Kanda Maalumu ya Polisi ya Tarime/Rorya, Constantine Masawe,alisema alikuwa nje ya ofisi."Niko Dar es Salaam na wala sikuwa na taarifa, amejiua kwa nini, maana sijaambiwa,"alisema.


Habari hii inanikumbusha mabaali sana kama miaka 2 iliyopita pale askari Polisi waliposema, kupitia vyombo vya habari, kuwa mahabusu kajinyonga kwa mkanda wa suruali akiwa selo. Ndugu wakaja juu kusema polisi ndio waliomwuua. Likazimwa kiaina ndugu hata wasielewe baada ya marehemu kuzikwa.

Mazingira yale yale tofauti ni style yamejirudia.

1. Mahabusu .....kajiua
2. Mahabusu ..... kajipiga risasi kwa kutumia SMG iliyokuwa kaunta
3. Kwa ni mahabusu ....polisi hawakujisumbua kuangalia usalama wake na mahabusu wengine waliokuwa mazingira hayo. SWALI KUBWA HILI
4. Dk Samsoni anawasaidia polisi....Kwanza,Yeye ni daktari wa kawaida wala si "Forensic pathologist or Anatomical pathologist". Pili, kasema "Ni kweli amejiua kwa kujipiga risasi..." Atasemaje kajipiga wakati wakati hakuwepo wakati tukio likitokea? Kwanini isiwe kapigwa risasi? Tatu, kwanini isiwe aliuliwa kwanza kisha maiti ikapigwa risasi. Akili inacheza "mdako"
5. Ni kweli kitaalamu kilichosababisha kifo ni risasi?
6. Kamanda Masawe hakuwa na taarifa anamuuliza mwandishi kajiua kwa nini, maana hajaambiwa.


Polisi na utumiaji nguvu kwa watu wadogo/wanyonge mbona Mzee wa vijisenti et al hawamwoshi nguvu walizonazo?
 
jama jama hii haiwezekani! hivi police wataacha lini kuuwa, hivi kweli mtu anaweza kujimiminia risasi nne kwa wakati mmoja? na huko mahabusu aliingia na silaha? huwa taarifa za hawajamaa ukizisoma unaweza kuchanganyikiwa,sawa mnyonge hana haki ila ipo siku bubu atasema,poleni sana wafiwa mungu yu pamoja nanyi:mad:

This is where many questions comes-by!!
If at all is an intended assassination, what is the motive?:mad:
 
Hassani,

Ukiwa Kibaha, unataka kwenda Kariakoo, utachukua barabara ya kuingilia Dar na kwenda kupitia Mbezi, Ubungo, Magomeni na mwisho Kariakoo. Ila pia unaweza ukatoka Kibaha ukaenda Mlandizi, Chalinze, Morogoro, Lindi, Vikindu, Kigamboni na ukachukua kivuko na mwisho ukajikuta Posta na kumalizia kuingia Kariakoo............... Cha ajabu ni watu kama wewe watasema "jamaa katumia njia safi sana na ya mkato".

Hata kama itakuwa imekunjwa kitako, badi siyo confortable kujipiga kifuani na inabidi uchukue muda. Ni rahisi zaidi kujiwekea bomba lake mdomoni na kumaliza kazi. Na hata mkiwa Jeshini wanafundisha hilo. Bastola wanajiwekea kichwani upande wa sikio na ni mara chache sana kujiwekea mdomoni.
Hebu angalia distance kutoka bomba la bunduki hadi kwenye sehemu ya kuweka kidole na kupiga.....
ak47afpht0.jpg
AK47S.jpg
 
Kwa Wanajeshi woote waliofundishwa kuuwa, akipewa target basi huwa wanatafuta sehemu mbili tu, USONI/kichwani na KIFUANI kwenye moyo. Ni Warusi tu ndiyo waliokuja na theory ya kutokuuwa ila kujeruhi. Wanadai mtu akiuawa, wenzake wanamuacha ila akijeruhiwa, basi hawawezi kumuacha ila itabidi wanajeshi wenzake wawili au walau mmoja ambebe na kumpeleka sehemu ya katibabu. Sasa hapo unakuwa umepunguza wanajeshi wawili.

Ukiangalia maelezo, unaona kabisa kuwa mtu na uzoefu wake aliingia kazini na kama alivyopewa shule, akamininiwa kifuani kwenye moyo.

Bila kujali ilivyokuwa, kwangu mie Suzzie katolewa KAFARA.
 
Masikini alikuwa kijana mdogo tuu wa miaka 22!! Mie tetesi nilizopztz kwa jamaa zango wa UWT zinasema kuwa Usalama wa taifa ndiyo waliomuua kwa risasi eti wanakomesha tabia ya uzembe inayo hatarisha maisha ya raisi!!! ukitaka kuamini angalia jinsi taarifa za kujiua kwake zinavyo jikanyaga, mara oo alikuwa mahabusu, mara oo hakuwa na kosa, maara oooo...n.k Kajipiga risasi 3 za SMG!! ALIITOA WAPI ALIKWA MAHABUSU?? alimnyang'anya askari mwenzie, mbona hawajasema...............
Utawala wa Kikwete umeshakuwa wa kidikteta.....yaoote hii ni kulamzimisha kumlinda dhidi ya kasoro zake nyingi...
Then kwanini Mwema anakimbilia kuunda tume???? kwanini isiundwe tume huru??? yaani tume iundwe na Mwema wakati na yeye ni sehemu ya tatizo!!!!! wasituchezee akili hawa wauaji.....hapa lazima ukweli ujulikanae..
 


Ndugu wapendwa nimesikitika na kushangaa jana kilichokuwa kikiongelewa hakuna asiyejua wazi baada ya mh marehemu kukosea aliitwa na kiongozi na kupewa masharti lukuki ambayo baada ya kuangalia kwa undani akaona ni mateso ya DUNIA na kuamua kujiua..

Mwema usisikilize sana hao wakubwa unowafata wakupe ukweli nenda uliza na watu wa chini...mmekuwa mkitafuna hela za serikali kila siku tume tume tume ya nini wakati iko wazi alipelekwa wapi na hata hiyo kuandika nina uhakika hata kushurutishwa ili jeshi lijione liko sawa

Kama alikuwa na hamu ya kujiua kwa nini akajiue baada ya msafara..polisi ni kazi za laana tu ni shida tu inawangangania watu kuwa mapolisi..ukweli ulio wazi wakubwa wa jeshi wamekuwa wakiwatesa sana mapolisi wa chini na si swala la kushangaa ma binti wengi kuvua nanii zao kwa ajili ya usalama wao.

Kama ungekuwa unasikiliza sana watu wa chini haya matatizo yasingetokea kumekuwa na umwinyi usio na maana jeshini ...tafadhali tunakuomba usihangaike na hao wakubwa wataishia kukuaribia jeshi lako!!!!
 
Last edited by a moderator:
kuna siku Mungu atachukizwa na huu uonevu, atashusha gharika la ajali kwa viongozi wajuu wanaohusika na utoaji wa uhai/dhulumu haki za watu wasiokua na hatia.

Ee Mungu naomba uwape utu viongozi wetu wenye mamlaka, watende yaliyo ya haki kwa wale wanaowaongoza,,,AMEN.
 
Jeshi la Polisi linawajibika na kifo hiki 100% Lakini kutokana na cheo na unyonge wa marehemu yataisha hivihivi. Kama kosa lililopelekea kuwekwa mahabusu kisha kusababisha kifo ni kuupotosha msafara wa Rais basi ni vema tamko litotelwe na mamlaka za juu zaidi ya RPC
 
Mkuu, SamsonMfalila uko sawa kabisa na hata mie naamini Mwema kapotoshwa. Ni hiyo ni ile ile laana waliyopewa 'askari" toka siku ile walipotoa ushuhuda wa uongo pale kaburini, siku alipofufuka Bwana Yesu. Walisema hivi nanukuu, "...wanafunzi wake walikuja na kuuiba mwili wa Bwana wao". Hivyo dhambi hyo hyo ndo inaendelea kuwatafuna hadi leo.

Hatutaki bla bla, jamii inahitaji ripoti kamili na siyo maelezo ya kupangwa.
 
Mtoa mada inaelekea ana more interesting and valuable infomation.
Please tujuvye zaidi.
Itatusaidia kulielewa vizuri jeshi letu la polisi.
 
Lakini ni Polisi haohao wakiambiwa piga risasi hao waandamanaji wa haki zao na bila kufikiri wanatekeleza huku wakicheka. Hili ni fundisho kwa askari wangine, msikubali kutumiwa na serikali kandamizi isiyosikia vilio vya watu wake. Maana mnaipa uwezo wa kuwateketeza hata nyie mkifanya makosa ya kiufundi ambayo hayawapendezi wao.
 
Kaka Samson, naona uko 'on line' tafadhali tudondoshee masharti hayo alopewa marehemu ili tuweze kuchangia mada kwa kuielewa.
 
Back
Top Bottom