Askari ajitoa uhai kwa kuupoteza msafara wa Kikwete Tarime!!!

jama jama hii haiwezekani! hivi police wataacha lini kuuwa, hivi kweli mtu anaweza kujimiminia risasi nne kwa wakati mmoja? na huko mahabusu aliingia na silaha? huwa taarifa za hawajamaa ukizisoma unaweza kuchanganyikiwa,sawa mnyonge hana haki ila ipo siku bubu atasema,poleni sana wafiwa mungu yu pamoja nanyi:mad:
 
Huyo WP anapaswa kuhurumiwa yeye pamoja na familia yake nahisi alijiua kwavile; Kwanza, imetokea Tarime na ukisema Tarime maana yake Chadema (kwa akili ya CCM). Pili, Vitisho alivyopewa na wakuu wake alihisi adhabu atakayopewa itakuwa ni sawa na Kifo tu na akaona heri ajiue mwenyewe bila kusubiria kifo cha mateso. Hata hivyo bado tuna haki ya kupewa taarifa sahihi za kifo cha dada huyu, japo nahisi taarifa haitakuwa natofauti kama ile ya kifo cha Imrani Kombe au hata ile ya wale jamaa toka Mahenge.

Ni mwaka wa uchaguzi tutaona mengi sana kabla ya Oktoba.
 
Rest in peace,ina maana usalama wa taifa hawapafahamu huko? huu sio uzembe wa WP bado wote.
 
Mkuu Kisoda2:

Nukuu za vyombo vya habari zinasema Askari huyo alikuwa "mapokezi" na yawezekana alikuwa bado "hajarudisha" silaha - na hii silaha yawezekana ni "bastola":







ALL-IN-ALL: uchunguzi zaidi unahitajika: Siamini kama Askari anaweza kuwekwa "chini ya Ulinzi" akabaki na silaha mkononi - hii ni kwa Tanzania pekee



Ni kweli nadhani alikuwa na bastola maana hawezi kuongoza msafara huku amebeba smg
 
ukiwa na smg then ukajipiga risasi haiwezi kuzid moja

huyu kajipga 3 trhna kwa smg?

kuna kitu hapo
 
Huyo WP anapaswa kuhurumiwa yeye pamoja na familia yake nahisi alijiua kwavile; Kwanza, imetokea Tarime na ukisema Tarime maana yake Chadema (kwa akili ya CCM). Pili, Vitisho alivyopewa na wakuu wake alihisi adhabu atakayopewa itakuwa ni sawa na Kifo tu na akaona heri ajiue mwenyewe bila kusubiria kifo cha mateso. Hata hivyo bado tuna haki ya kupewa taarifa sahihi za kifo cha dada huyu, japo nahisi taarifa haitakuwa natofauti kama ile ya kifo cha Imrani Kombe au hata ile ya wale jamaa toka Mahenge.

Ni mwaka wa uchaguzi tutaona mengi sana kabla ya Oktoba.

point noted.
 
Risasi sio konzi. Huwezi kujipiga risasi moja ukaweza kijipiga nyingine, licha hizo nne. Something is very wrong here. The whole story stinks of spin!
 
maskini Dada wa watu katolewa Mhanga bila kujua.....atkuwa aliuwawa ili kuficha ukweli...manake tangu lini Mahabusu akawa na silaha nzito hivyo??au labda alipewa akalazimishwa ajiue kabla hajauwawa....ooh its so sad and unbelievable!
Kikwete ni Nuksi tu ndo maana kila akizindua kitu lazima itokee skendo...mara majina ya wilaya yamekosewa...au anazindua kitu kumbe kesi iko mahakamani au mradi kama wa Maleria kumbe umejaa dhuluma tupu na mengine meengi tu...!sijui nani alumiwe,wasaidizi wake au usalama wa Taifa?RIP Suzana.:disapointed:
 
Naomba kutoa pole kwa familia ya WP Suzana hasa baada ya kupotelewa kwa binti yao.

Najua Mzee Mwanakijiji unanisoma,sina jinsi ya kuelezea ama kuhoji tukio hili ila naamini kwa kuwa wewe ni mzee kidogo kuliko mimi unaweza kutetea kitendo hiki na kuweka mifano mizuri zaidi ambayo italeta Maana.

Nafahamu fika ulifanya hizi kwa yule binti wa chuo cha mtakatifu augustino(Nsia),ukafanya hivyo kwa Mhe. Sophia Simba na sasa sioni vibaya kama ukifanya utetezi kwa WP Suzana.

Sina nia mbaya ya kukosana na Watu wa usalama wa taifa, lengo la kuandika haya machache si kwa kuwashtaki kwa Rais Jakaya Kikwete ila ni kuwekana sawa tu. Vivyo hivyo hata wakuu zangu wa Polisi ujumbe huu ni sawa na semina elekezi tu.

Mhe. Masha naomba uunde tume kuchunguza kifo hiki na ijulikane nini kilifanyika na kama kuna haja ya kubadilisha amri ama maelekezo huu ndiyo muda wake.

Mkuu Mwema, naomba ulitolee maelezo hili sababu lina madhara makubwa sana kwa polisi wengi ambao wanafanya kazi ya kulinda raia wa taifa hili.

Rais kikwete nakupa pole sana sababu najua hili litakuwa limekuhuzunisha sana, Mungu akupe moyo wa uvumilivu!

Poleni Familia ya WP Suzana.

Kapumzike kwa amani Suzana.

Mkuu Gembe nipo kwenye maombolezo na nimeshindwa kabisa kuandika maneno makali kukemea jambo hili na nahitaji msaada!
 
who is she??? what happened??? mkuu weka data zote ili hata tusiojua kilichotokea tujue and MAYBE tunaweza to mchango wowote
 
Ni askari Mmoja amejiuja majuzi

SAA chache tu baada ya msafara wa Rais Jakaya Kikwete, kuingia katika Kanisa a Anglikana, ili kuhudhuria sherehe za kuwekwa wakfu Askofu, askari polisi wa kike WP Suzana, amejiua kwa kujipiga risasi baada ya kuwekwa mahabusu kwa kosa la kuupoteza njia, msafara wa Rais.

Habari zilisema tukio hilo lililogeuka kuwa gumzo katika mji huo, lilitokea saa 8 mchana wa jana, katika Kituo cha Polisi Tarime, muda mfupi baada ya askari huyo kuwekwa chini ya ulinzi.


Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Tarime, Dk Charles Samson, alikiri kuupokea mwili wa askari huyo na kwamba alijipiga risasi upande wa kushoto wa kifua.


Kwa mujibu wa Mganga huyo, risasi hiyo ilipenya na kutokea nyuma ya bega.


"Ni kweli amejiua kwa kujipiga risasi ambayo imetokea nyuma ya bega. Kwa ufupi ni kwamba eneo hilo ni sehemu ya moyo, nimemfanyia uchunguzi wa awali na

kuthibitisha kuwa amekufa,"alisema.

Alisema taarifa kuhusu tukio hilo alizipata akiwa katika msafara wa Rais na kwamba alipokwenda kumfanyia uchunguzi marehemu, alibaini kuwa alikata roho muda mfupi,baada ya kujipiga risasi.


"Kitaalam kilichosabaisha kifo ni risasi maana nimefanya uchunguzi na kubaini, nasubiri uchunguzi mkubwa tukiwa na polisi ili tuwakabidhi maiti kwa ajili ya hatua nyingine,"alisema kwa masikitiko.


"Sijui nini kimempelekea kujiua maana huo ni uamuzi mzito sana aliochukua," alisisitiza Mganga mkuu.


Kwa upande wake, mhudumu wa chumba cha maiti katika hospitali hiyo, Samweli Malindi, alisema marehemu alifikishwa katika katika chumba hicho kwa kutumia gari la polisi.


"Walisema amejiua kwa sababu ya kuongoza vibaya msafara wa Rais na kuwekwa mahabusu," alisema.


Chanzo kimoja cha uhakika kutoka ndani ya jeshi hilo, kililiambia

gazeti hili kuwa kiini cha askari huyo kujiua ni kuwekwa mahabusu huku akitishiwa kuchukuliwa hatua kali zaidi.

Chanzo hicho kilisema msafara wa Rais ulitakiwa kuingia kwa mkuu wa wilaya, kabla ya kwenda kanisani, lakini yeye aliruhusu magari kwenda moja kwa moja na gari la Rais likielekea kwa mkuu wa wilaya, jambo lililosababisha safara ukagawanyika na baadaye kulazimika kurudi.


"Kitendo hicho kiliwachukiza viongozi na kuamuru kukamatwa na kuwekwa

mahabusu kwa askari huyo. Wakati akiwa mapokezi ghafla alichukua bunduki aina ya SMG na kujimiminia risasi tatu na kukata roho papo hapo," kilisema chanzo hicho.

Chanzo hicho kilidai kuwa askari huyo ni miongoni mwa askari polisi waliotoka chuoni hivi karibuni na kwa hiyo si mzoefu.


Chanzo hicho kilisema katika hali ya kawaida viongozi walipaswa kumsaidia kwa kutumia lugha ambayo vinginevyo isingemfanya ajisikie vibaya na kuchukua uamuzi huo. Baadhi ya wananchi wakizungumza na Mwananchi walisema hayo ni matatizo ya matumizi ya nguvu ndani ya jeshi.

Alipotakiwa kuzungumzia suala hilo kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi katika Kanda Maalumu ya Polisi ya Tarime/Rorya, Constantine Masawe,alisema alikuwa nje ya ofisi."Niko Dar es Salaam na wala sikuwa na taarifa, amejiua kwa nini, maana sijaambiwa,"alisema.


Rais Kikwete, alikuwa amekwenda Tarime kuhudhuria kuwekwa wakfu kwa Askofu Dk Mwita Akiri.


Polisi ajiua kwa kuupoteza msafara wa Rais Kikwete,AJIPIGA RISASI AKIWA RUMANDE
 
Ni lazima tu alipewa vitisho vikubwa maana hawa polisi kwa kupenda sifa! Eeeh Mola ilaze pahali pema pepono roho ya WP Suzan na uipe auni familia yake. Ameen!
 
Dah inasikitisha.Lakini nadhani alichukua uamuzi mzito zaidi ukilinganisha na kosa lenyewe.Na isitoshe pengine alikuwa ni mwoga kukabiliana na challenges za kikazi........
Hatupaswi kogopa kukosea kwa maana ndio kujifunza........
 
Kwa taratibu za kijeshi ni makosa kwa askari kuacha silaha au kuiweka pembeni au kumkabidhi mtu mwingine akushikie,kwanz a silaha iliyotumika ijulikane ni askari gani alikuwa anapaswa awe nayo kwa wakati huo ili achukuliwe hatua, pili kiongozi aliyempangia askari huyo kuongoza msafara wa kiongozi mkubwa kama huyo bila kuzingatia uzoefu wa askari huyo naye anatakiwa kuchukuliwa hatua, tatu mpanga ratiba kwanini hakuweka wazi kuwa kwanza msafara utaanzia kwa mkuu wa wilaya halafu kanisani achukuliwe hatua, kwa ujumla uongozi wote wa polisi wilaya na uongozi wa serikali wa wilaya unatakiwa kuwajibishwa kwa kitendo hicho cha uzembe hadi kusababisha kifo cha askari huyo. RIP WP Suzy
 
Mkuu Kisoda2:

Nukuu za vyombo vya habari zinasema Askari huyo alikuwa "mapokezi" na yawezekana alikuwa bado "hajarudisha" silaha - na hii silaha yawezekana ni "bastola":







ALL-IN-ALL: uchunguzi zaidi unahitajika: Siamini kama Askari anaweza kuwekwa "chini ya Ulinzi" akabaki na silaha mkononi - hii ni kwa Tanzania pekee
Hapa lazima mkulu atwambie kulikoni huyu afe,na tena kwa risasi nne! na pia akiwa chini ya ulinzi wa polisi?
 
Na risasi zenyewe za kwenye moyo? Nne? haya ni mashokolo mageni. Tangu niliposikia hii hadithi sikuielewa. Na may be sitapewa nafasi ya kuielewa. Eti, Binti/au mama yenu alikuwa na roho ndogo hivyo? Alikua ana panic kwa vitu kama hivyo ambavyo kwa Tanzania wala sio big deal? Yani aliogopa adhabu ambayo angeipata kwa kosa hilo au? Mi sina jibu, najua na nyiye hamna majibu. Poleni wafiwa, thats all I can say!!!!
 
maskini Dada wa watu katolewa Mhanga bila kujua.....atkuwa aliuwawa ili kuficha ukweli...manake tangu lini Mahabusu akawa na silaha nzito hivyo??au labda alipewa akalazimishwa ajiue kabla hajauwawa....ooh its so sad and unbelievable!
Kikwete ni Nuksi tu ndo maana kila akizindua kitu lazima itokee skendo...mara majina ya wilaya yamekosewa...au anazindua kitu kumbe kesi iko mahakamani au mradi kama wa Maleria kumbe umejaa dhuluma tupu na mengine meengi tu...!sijui nani alumiwe,wasaidizi wake au usalama wa Taifa?RIP Suzana.:disapointed:
Hapa jamaa inabidi aje na taarifa ilonyoooka.
 
hawezi kujiua kwa kosa kama hilo,kwa sababu Tz ni mambo madogo sana!aliyeweka chakachua kwenye gari ya Raisi alifanywa nini? na aliyesahau kufunga nati kwenye gari za Raisi!watueleze walimfanya nini huyo dada?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom