Askari ajitoa uhai kwa kuupoteza msafara wa Kikwete Tarime!!!

Sajenti

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
3,651
412
Askari wa kike (WP Suzana) wa kituo cha Polisi Tarime mkoania mara amejiua kwa kujipiga risasi 4 katika upande wa kushoto wa kifua chake.

Habari zinasema askari huyo alikuwa katika zamu ya kuongoza msafara wa Rais Kikwete aliyekuwa ziarani huko Tarime kwa shughuli za ufunguzi wa bwawa la maji la manchira.

WP Suzana alipoteza muelekeo wa msafara wa Raisi Kikwete uliotakiwa kuelekezwa kwenda kwenye kanisa la hapo Tarime.

Tukio hilo lilisababisha viongozi wake kumuweka mahabusu akisubiri hatua nyingine za kinidhamu lakini jana askari huyo alijilipua kwa risasi na kupoteza uhai wake...

Source: Mwananchi newspaper

My take:

Inawezekanaje awekwe mahabusu na kuweza kupata silaha hadi kujitoa uhai? Kweli Suzana hilo tu limekufanya utoe roho yako kisa kukosea kuelekeza msafara? Kwa kweli roho imeniuma sana ingawa simfahamu huyo askari....RIP Suzzy!
 
mungu aipe nguvu familia yake... inasikisisha sana kupoteza askari

lakini lazma kuna makosa ya kiufundi hapo, kwanza kupoteza msafara, pili kuwa mahabusu akiwa na silaha, nk. nk.

RIP
 
Waungwana tuwekane sawa katika hili.
Inawezekanaje unawekwa ndani/rumande/cell ukiwa na silaha achilia mbala mkanda wa suruwali na hata viatu?

Je kuna ukweli wowote katika hili la askari aliekosea kuuelekeza msafara wa muungwana njia sahii kuwekwa rumande na kisha mwenyewe kujiua kwa risasi tena nne(4)????????????????
 
Ripoti za jeshi la polisi wa Tz zina utata mkubwa sana. Ni ripoti ambazo hazistahili kutolewa na hata mgambo ambao hawajaenda shule.

Inakuwa je aliye mahabusu awe na silaha?. Bado nchi yetu hata zama hizi za technologia tunaendesha mambo ki barbariic style. Nasema kama kuna kitengo kinachoongoza nchini kwa uhalifu ni jeshi letu la polisi.
 
My take:

Inawezekanaje awekwe mahabusu na kuweza kupata silaha hadi kujitoa uhai? Kweli Suzana hilo tu limekufanya utoe roho yako kisa kukosea kuelekeza msafara? Kwa kweli roho imeniuma sana ingawa simfahamu huyo askari....RIP Suzzy!

Labda hii itaweza kutoa mwanga zaidi

"Kitendo hicho kiliwachukiza viongozi na kuamuru kukamatwa na kuwekwa
mahabusu kwa askari huyo. Wakati akiwa mapokezi ghafla alichukua bunduki aina ya SMG na kujimiminia risasi tatu na kukata roho papo hapo," kilisema chanzo hicho.

Source: Mwananchi newspaper.

RIP Suzana
 
Mkuu Kisoda2:

Nukuu za vyombo vya habari zinasema Askari huyo alikuwa "mapokezi" na yawezekana alikuwa bado "hajarudisha" silaha - na hii silaha yawezekana ni "bastola":

Mwananchi:

Polisi ajiua kwa kuupoteza msafara wa Rais Kikwete,AJIPIGA RISASI AKIWA RUMANDE

Habari Leo:
Not Reported

Tanzania Daima:
Polisi ajipiga risasi nne kituoni

ALL-IN-ALL: uchunguzi zaidi unahitajika: Siamini kama Askari anaweza kuwekwa "chini ya Ulinzi" akabaki na silaha mkononi - hii ni kwa Tanzania pekee
 
I strongly believe there are something behind the scenes !!! shooting herself 4 times, now way plz. That is next to impossible !!!! wakuu hio issue haingiii akilini kabisa, may be if they come up with plan B to cover the story.
 
Huenda amri ya wakubwa zake ilikuwa kumdanganya Rais kama ilivyo kawaida halafu baada ya kumdanganya njia Rais wake wakubwa wakamgeukia kuwa kwanini kamudanganya Rais wa wadanganyika, hapo ndipo hasira zikampata kwanini nitimize amri halali halafu waseme nimedanganya njia?.....pwaa pwaaa pwaaa pwaaaaaaaaaa, hatuwezi jua wapelelezi ni wao wenyewe
 
Wana JF,

Kwanza Haiwezekani kabisa kwa Binadamu yeyote kujipiga Risasi zaidi hata ya mmoja tena binadamu anaye jiua ni akisha jipiga risasi mmoja basi imetoka hata kama kwa kujaribu jipige mkononi uone kama utarudia risasi ya pili na ya tatu mpaka ya nne.

Ntauhoji Usalama wa taifa pia na Jeshi la police huko mara,tarime wakuu wa vituo vyote ulisha ona wapi mtu anawekwa chini ya rumande au mahabusu ambako kuna siraha za moto au kuna kifaa chochote hatarishi??

Walio husika wanawajibu wa kuwajibishwa kwa kusababisha huyo askari kujiua na uchunguzi ufanyike,

Kuna jambo hapo lazima
 
Nina mashaka sana kwamba mtu ambaye ameamua kujimaliza kwa kulenga moyo wake halafu anafyatua risasi tatu.
Hii ripoti ni HAJUA. waje tena na uongo mwingine.

Ninaanza kutilia shaka hata kile kifo cha yule mkufunzi pale chuo cha polisi dar es salaam kwa maana mazingira ya vifo hivyi yana utata mkubwa...

Ninahisi kuna balaa kubwa linakuja mbeleni muda si mrefu maana haya matukio yanafululiza kila kukicha ilihali hakuna ufafanuzi makini wa mambo haya..

Mungu mrehemu marehemu.
 
Wana JF,

Kwanza Haiwezekani kabisa kwa Binadamu yeyote kujipiga Risasi zaidi hata ya mmoja tena binadamu anaye jiua ni akisha jipiga risasi mmoja basi imetoka hata kama kwa kujaribu jipige mkononi uone kama utarudia risasi ya pili na ya tatu mpaka ya nne.

Ntauhoji Usalama wa taifa pia na Jeshi la police huko mara,tarime wakuu wa vituo vyote ulisha ona wapi mtu anawekwa chini ya rumande au mahabusu ambako kuna siraha za moto au kuna kifaa chochote hatarishi??

Walio husika wanawajibu wa kuwajibishwa kwa kusababisha huyo askari kujiua na uchunguzi ufanyike,

Kuna jambo hapo lazima

Kaka ni SMG. hapa ndiyo mafunzo ya JKT tuliyopata yanatusaidia - SMG unaweza kuset risasi hata mia zikapiga kwa mtiririko na kasi sana ( in seconds) , kwa hiyo huyu mama aliset zote 4 zitoke kwa pamoja - alivyoachia tu zote nne zikamiminika.

Labda tuangalie upande wa pili - alipataje hiyo silaha na kuset automatic execution - ina maana alikuwa na muda na hiyo silaha.
 
UwT wanahusika big time ktk hili.
Ninahisi nchi hii hatuko pamoja
 
Tangu nilipoiona habari hii kwenye gazeti la mwananchi, conclusion yangu niliyoifanya ni kwamba huyu askari kauawa. Hakuna lingine na wala polisi wasituletee longolongo hapa na sidhani kama kuna maelezo mengine yoyote yanayoweza kutolewa yatakayotengua ukweli huu kwamba askari huyu ameuawa.
Huwezi kuniambia askari amejiua kwa kujipiga risasi ilihali alikuwa tayari ni mtuhumiwa. Aliwezaje kuwa mtuhumiwa halafu ana silaha. Na pili hivi unawezaje kujipiga kwa shortgun risasi hata mbili jamani. Maana hiyo moja tu utakapoachia ndo ushasambaratika hiyo ya pili unaianzia wapi? Hoja hii ni ya kipuuzi na kuna kila sababu ya hatua zaidi kuchukuliwa dhidi ya tukio hili. Kuna haja ya watanzania kusema sasa yatosha.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom