Asiyewahi kucheat na ataje jina kamili humu

lazydog
lazydog is thinking of change
JF Senior Expert Member Join Date: Thu Apr 2008
Posts: 642
Rep Power: 22

Thanks: 3,726
Thanked 248 Times in 184 Posts
Credits: 23,185

Re: Asiyewahi kucheat na ataje jina kamili humu

--------------------------------------------------------------------------------

Quote:
Originally Posted by MAMA MIA
Wana jf nimefurahi kuona wengi walikuwa makini kuwataja watu na kwa upande mwingine hongereni kwa kusaidia kubadilisha tabia za watu...ila nafikiri tuangalie wenyewe kwanza mwenye uhakika ajawahi kuzini yaani kutoka nje ya ndoa au nje rel ship yake
na aaanze kutaja jina lake na namba zake tuanze kupongezana humubadala ya kukaa na kuapakana huku tukiwa wachafu
nawasilisha


Mbona unatuchanganya. Ni kipi unajaribu kutueleza?


LAZYDOG NILIVYOMUELEWA ANAPONGEZA KWA KUREKEBISHA TABIA ILA ANASHAURI TUANZE KUBADILIKA KWANZA KAMA WANA JF WAAMINIFU NA SI KUKIMMBILIA NDOA ZA WATU HUKU VYUMBANI MWETU KUKIWAKA MOTO KAMA NIMEMUELEWA VYEMA:::::;
 
Ukweli halisi wangu ndio huu

naitwa rehema mwanisongole::

Kucheat sikumbuki kabisa ila nakumbuka kufall in lavu tu

tangu hapo niko innoshillings
 
LAZYDOG NILIVYOMUELEWA ANAPONGEZA KWA KUREKEBISHA TABIA ILA ANASHAURI TUANZE KUBADILIKA KWANZA KAMA WANA JF WAAMINIFU NA SI KUKIMMBILIA NDOA ZA WATU HUKU VYUMBANI MWETU KUKIWAKA MOTO KAMA NIMEMUELEWA VYEMA:::::;


Haya bwana, aendelee na survey.



.
 


Ningependa kusikia zaidi kuhusu hiyo mission japo ni ya kitambo; kama uko tayari ku-share lakini :)



.

Haya lazy dog ilikuwa hivi....Kuna kaka nilitokea kuzoeana nae sana, ikawa tunasaidiana kwa kila jambo ambalo mmoja wetu inatokea amefail.... kipindi hicho my x bf alikuwa kaanza vituko sababu hazikosekani kila cku mara hiki mara kile lazima tugombane....nikavumilia karibu kwa mwaka mzima... sasa huyo kaka mwingine akawa anaonekana kujivuta karibu yangu sana mmh nami karoho kakaanza kumdondokea.. kumbe nilifanya kosa kumwambia matatizo yangu na huyo x wangu akawa anatumia upenyo huo kujisogeza.. ikafika kipindi kaka wa watu ikabidi amwage sera zake.. nikampa ka muda ingawa nami nilivutiwa nae ( baada ya kukaa na kufikiri sana nikaona bora niwe peke yangu tu maana moyo bado ulikuwa kwa huyo mpenzi wangu mwingine) nikaona nitamuumiza tu kaka wa watu.... ikabidi nimtolee nje
 
Nilika mwaka 1 mzima huku Marekani kabla mke wangu hajaja miaka 10 ilopita lakini bado kwangu haikuwa leseni ya kula uloda nje kwa vibinti chee vya kizungu vilivyojaa kila kona.

Nina miaka 15 katika ndoa yangu na sijawahi kutongoza mwanamke yeyote katika nia ya kutaka kula uloda, hii ni kwa sababu akili yangu haiamini hivyo.

Nilijipiga kufuri mwenyewe mwaka 1991 baada ya kushuhudia marafiki zangu kadhaa wakidhoofika hadi kufa kwa gonjwa la Ukimwi, huku wakiacha fedha magari na nyumba za kifahari.

Nilijiapiza kwamba kuanzia wakati ule na kuendelea sita toka nje ya ndoa yangu kwenda kutuliza hamu kwa kunywea kata isiyo yangu.

Kufanya jambo hilo liwe kitendo cha kweli mimi na G friend wangu ambaye sasa ni mke wangu tulijipeleka wenyewe pale mikocheni tukatolewa visusio vichekiwe kama viko swanu. Majibu yalipo toka kwamba tu wazima wa afya tuliamua kupeleka mahusiano yetu katika daraja la juu kabisa mwaka uliofuata tulifunga pingu za maisha.

Pingu hizo bado zinanifungamanisha na mwenzangu hadi leo.

Ujumbe kwa wale wanao dhani ni vigumu kuwa mwaminifu kwa mwana ndoa mwenzio ni huu.

Tatizo la kutembea nje ya ndoa au kuwa na matamanio makubwa ya kimwili yasumbuwayo roho yako yamo ndani ya akili yako na si nje.
Uzuri au ubaya wa kitu si mwonekano wake tu ila ni pamoja na taswira ijengwayo na kubebwa na akili yako itumikayo katika ulinganifu.
Kitu au jambo litakuwa zuri tu kama akili yako inatoa mwanya kuruhusu mwonekano wa uzuri, kinyume chake hakuna uzuri wowote.
 
Kucheat kunaongeza mapenzi! waliojulikana wanacheat mapenzi yanaongezeka zaidi (Refer Bill Clinton Case).

Mbona msio cheat hamtaji majina kama ilivyopendekezwa na mtoa hoja? Inawezekana mtu akawa shujaa wa kutokucheat kwa sababu tu hauko katika mzingira hatarishi ya kukufanya ucheat.

Labda huna mvuto, huna mkwanja, PR mbovu na hauko maridadi. Kama vyote hivi unavyo na haukuwahi kucheat basi shujaa. kwakuongezea wanaosema hawaja cheat watoe pia na anuani za wenza ili waulizwe bibiography zao.
 
Mimi kwa upande wangu sijahawi kucheat hata siku moja.
Naitwa Tusajigwe Anyemike. bahati mbaya sina simu ningetoa namba yangu.
 
wachangiaji,
Mtoa hoja mwenyewe hakusema namba yake ya simu na nafikiri si vizuri kutaja tu jina lako na namba yako ya simu katika website kama hii maana humjui mtu humu na hujui wengine watatumiaje namba yako ya simu.

sisemi kwamba mtu atataka mapenzi maana nitamkatalia anyway lakini ni vizuri kuzuia usumbufu.

By the way hata nikisema naitwa Matiku Chambiri then una uhakika gani kama ndio mimi na suppose niseme namba yangu ya simu ni 022000000 then una uhakika gani kama ni ya kweli. nafikiri cha msingi ni kupeana ukweli wa kama umecheat au la ila sio contacts maana zaweza kukutia usumbufu mwingine.

Hongera kwa wasiocheat. mliocheat pia cha msingi ni kufanya maamuzi kwamba hamtorudia tena.
 
Haya lazy dog ilikuwa hivi....Kuna kaka nilitokea kuzoeana nae sana, ikawa tunasaidiana kwa kila jambo ambalo mmoja wetu inatokea amefail.... kipindi hicho my x bf alikuwa kaanza vituko sababu hazikosekani kila cku mara hiki mara kile lazima tugombane....nikavumilia karibu kwa mwaka mzima... sasa huyo kaka mwingine akawa anaonekana kujivuta karibu yangu sana mmh nami karoho kakaanza kumdondokea.. kumbe nilifanya kosa kumwambia matatizo yangu na huyo x wangu akawa anatumia upenyo huo kujisogeza.. ikafika kipindi kaka wa watu ikabidi amwage sera zake.. nikampa ka muda ingawa nami nilivutiwa nae ( baada ya kukaa na kufikiri sana nikaona bora niwe peke yangu tu maana moyo bado ulikuwa kwa huyo mpenzi wangu mwingine) nikaona nitamuumiza tu kaka wa watu.... ikabidi nimtolee nje

Thanks for sharing.

Kwenye bandiko lako la mwanzo ulisema ulitaka ku-cheat. Napata picha kwamba ulitaka kuanza mahusiano na huyo rafiki, wakati huo huo kuendeleza mahusiano na X bf, au sio? Sikuhukumu, najaribu tu kupata picha kamili. Natambua kwamba wasichana huwa wana "backup" hasa wakifikia umri wa kuolewa.

Kucheat kunaongeza mapenzi! waliojulikana wanacheat mapenzi yanaongezeka zaidi (Refer Bill Clinton Case).

Labda huna mvuto, huna mkwanja, PR mbovu na hauko maridadi. Kama vyote hivi unavyo na haukuwahi kucheat basi shujaa. kwakuongezea wanaosema hawaja cheat watoe pia na anuani za wenza ili waulizwe bibiography zao.


Ku-cheat kunaongeza mapenzi? Sina hakika na hilo. Ambacho nina hakika nacho ni kwamba kilichotokea kwa Richard wa BBA-II na mkewe hutokea kwa watu wa personality fulani tu, tofauti na hapo the outcome will not be similar. What you saw does not apply to every couple.

Naamini kwamba mke wa Bill Clinton kila mara kiroho juu. Pia, tofauti na Bill Clinton, she is unhappy and she will continue to be. Nenda kwa Richard na Ricki kama hukukuta a similar pattern. Baada ya hapo rejea tafsiri sahihi ya "kuongeza mapenzi"!


.
 
Mimi nime cheat na bado nitacheat sitarajii kaucha...naomba hukumu yenu

Nakutumia Namba yangu ya simu kwenye PM ila umpe wifi nataka nimpeleke kwa karumanzira ukifika uchochoroni .. network haipatikani kabisa ...ukirudi nyumbani ni full communication ... hmmm utafedheheka wewe kila kona wanawake watakukimbia

unaonaje hukumu hii
 
Mimi naitwa Nyangema Samweli, sina simu.
Asikwambie mtu kucheat ni mbaya sana na wala haiongezi mapenzi inazidi kuzorotesha mapenzi pale mmoja wenu atakapogundua kuwa mwenzake anacheat. Atakachofanya mbele ya watu ni kujikaza tu lakini kama kungekuwa na uwezo wa kufungua mioyo yao ungeona ni jinsi gani wanaumia.
 
Mhn hii mada nayo? Anyway JF ni mtandao wa wanajamii wanaokosoa na kukosoana, wanaoelimisha na kuelimishana. Mara nyingi majina na details za members ni siri ya member wenyewe, hii ni kutokana na mada zinazojadiliwa humu. Sasa hapa tunapoambiana tutoe details hizo, mbona inakuwa ngumu?

Kwa mtazamo wangu, kucheat au kutokucheat inategemea vitu vitatu;1.Muda 2.Privacy 3.Money

Sasa kwa mtazamo wangu asilimia zaidi ya 80 ya watu waliopata kuwa na mambo hayo matatu kwa pamoja, wameweza kucheat au kukaribia kucheat. Ukitaka kuthibitisha hili nenda Dodoma mkaone wabunge wetu ambao wamebarikiwa kuwa na vitu hivyo vitatu wanavyo behave.

Wagumu wanaoweza kulikabili hili (kuto kucheat)wakati wana fursa hizo zote hizo ni wachache sana!!
 
Hatuwezi kuwaamini kwamba hamja-cheat-. Roho zenu ndizo zinazojua na sio midomo yenu 'life and death are in the power of tonque'
 
mimi ktk maisha ya r/ship ya kawaida cjawahi kucheat na pia toka nimeolewa ni miaka miwili sasa sijawahi kucheat na SITARAJII
Baada ya at least miaka nane,tuombe uhai ,then njoo utupe MAENDELEO YAKO.
 
Baada ya at least miaka nane,tuombe uhai ,then njoo utupe MAENDELEO YAKO.

tuombe tu uhai kwakweli ila as far as nimeona ndugu, jamaa, marafiki, majirani nk wakihangaika na wakiteseka kutokana na kucheat kwenye mahusiano yao esp.ndoa kwa kweli SITARAJII
nitakuja hapa baradhani kuthibitisha hili usiofu
kuhusu namba cwezi kutoa kwani si wote wenye nia njema
 
Nafikiri unataka kutuaminisha kwamba ku-cheat ni kitu cha kawaida kiasi kwamba watu wengi wanafanya na hivyo si ajabu-si kweli. Inaonekana mama mia wewe ni noma kwa kuibia, sio tabia nzuri, kama umemchoka mwenzio mwambie mfuate huyo anayekuridhisha. Kuhusu kuonyana humu ni sawa kabisa maana ukweli unabaki palepale kuwa ku-cheat si kuzuri na ma-ukimwi haya.
 
Back
Top Bottom