Elections 2010 Asiyefunzwa na mamaye atafunzwa na ulimwengu ni tusi?

utawala uliopo unapendelea upande mmoja,tusife moyo serkali mpya ya CHADEMA itakapoingia madarakan ndio ccm itakaposhkishwa adabu.tuombe Mungu tu na tukapige kura.
 
Chadema nao wana haki ya kushitaki kama wanaona wametukanwa kwani hiyo haiondoi kosa la mgombea wa chadema kumtukana wa CCM. Two wrongs don't make one right, kwa kiswahili kibovu....Makosa mawili hayafanyi kuwa kosa moja lililo sahihi. Tuhukumu kila kosa kwa hoja zake. Usije kwenda mahakamani/kizimbani ukamwambia hakimu kwamba, mheshimiwa hakimu niliamua kumwibia ng'ombe bwana X aliyenishitaki baada ya hapo awali yeye kuniibia mbuzi wawili.

Kova kasema wamemshika huyo wa CHADEMA kwa kuvunja sheria na si kwa amalalamiko ya CCM....Kamala je mbona hajamshika?
 
"Asiyefunzwa na mamamaye hufunzwa na ulimwengu" naikumbuka hii nilifundishwa shule ya msingi. Ina maana nilifundishwa tusi? basi tatizo ni mitaala na wala si mtu. HAHAHAHAHAHAHAHAHA!!!!!!
 
Mie nawashangaa sana hawa CCM, jana Mrisho J.K kawadharau wanamageuzi hajafanywa chochote, Hadija Kopa nae kamkashifu Dr. Slaa lakini Selemani Kova hajasema chochote.

Kila siku Yusuph Makamba anatoa kauli za hovyo kabisa na manager wa kampeni Abdulhaman Kinana hakemei kabisa yeye analalamika tu CCM wanaposemwa.

Mie nafikiri mkuu wa jeshi la polisi ndugu Said Mwema anatakiwa awe makini sana na mambo haya.

Hizo bold, duuuuh!!!
 
Katika suala la matusi mimi si shabiki hata siku moja, kwa yeyote alimsikia yule mgombea wa chadema live pale mwembeyanga yale ni matusi na anaweza kukiharibia chama chake kukosa kura za watanzania wapiga kura za mlengo wa upande wa ustaarabu. John Mnyika na Anna Maulida Komu wanasitahili pongezi kwa kumiliki jukwaa vizuri na kuushawishi uuma kwamba hawako kwenye siasa kwa ajili ya matusi bali kujenga hoja zenye mantiki ya kuvuta hisia ya mpiga kura.Tutakuwa tunafanya makosa makubwa kwa mustakabari wa taifa letu tukifikiri kwamba siasa ni matusi, na hii si kwa sababu alimtukana Kikwete mgombea wa CCM bali hata angaekuwa ni mgombea wa chama chochote...TLP, NCCR, CUF n.k

Kusema kikwete hakufunzwa na mama yake mzazi wakati mama wa mgombea huyo alishakufa ni suala lisilokubarika na linaweza kukumbusha kifo cha mama ya mtu si uungwana


Mimi binafsi sitashangaa sana kama huyu bwana atafunguliwa mashitaka.

Hivi Kipenzi Chetu JK kwanini meweka picha ya Mama yake kwenye kampeni zake? halafu watu wakiongea kwa kumtaja mama anaona ametukanwa? hajui shillingi ina pande mbili , kumtumia mama kuna faida yake na pia kuna hasara zake, kama vile kumtumia mkewe au watoto, au pesa
 
WanaJF tuache mambo ya ajabu,kama methali iliyotumika ni tusi basi pale wakishamhukumu jamaa uyu mbunge mi naenda mahakamani kupetite against the Republic maana kila kitabu kilicho kwenye mtaala niliposoma primary nilikutana na methali hii. Kama ni tusi serikali imeufundisha umma matusi!
 
katika suala la matusi mimi si shabiki hata siku moja, kwa yeyote alimsikia yule mgombea wa chadema live pale mwembeyanga yale ni matusi na anaweza kukiharibia chama chake kukosa kura za watanzania wapiga kura za mlengo wa upande wa ustaarabu. John mnyika na anna maulida komu wanasitahili pongezi kwa kumiliki jukwaa vizuri na kuushawishi uuma kwamba hawako kwenye siasa kwa ajili ya matusi bali kujenga hoja zenye mantiki ya kuvuta hisia ya mpiga kura.tutakuwa tunafanya makosa makubwa kwa mustakabari wa taifa letu tukifikiri kwamba siasa ni matusi, na hii si kwa sababu alimtukana kikwete mgombea wa ccm bali hata angaekuwa ni mgombea wa chama chochote...tlp, nccr, cuf n.k

kusema kikwete hakufunzwa na mama yake mzazi wakati mama wa mgombea huyo alishakufa ni suala lisilokubarika na linaweza kukumbusha kifo cha mama ya mtu si uungwana

mimi binafsi sitashangaa sana kama huyu bwana atafunguliwa mashitaka.

hivi kuna tusi hapo? Huo ni msemo wa kiswahili tangu enzi - acheni kufilisika kimawazo. Hakuna tusi hapo!
 
kuna ukweli kuhusu rais wetu kuwa ulimwengu utamfunza,kumbukeni wahisani walipotishia kuinyima pesa serikali kuhusu epa ndio jk akaamua watu wapelekwe mahakamani.niliona kuwa rais hana adabu kwa point zifuatazo;

1.Wenye ukimwi ni kiherehere chao-hajui dada na kaka zetu ambao shida ndio zinawafanya hivyo.

2.Wanafunzi kupata mimba ni kiherehere chao-hajui kuwa kipato ni kidogo na ulaghai ni mwingi hata ukiangalia ndani ya familia watoto wake wote wamezaliwa na mama wangapi ina maana wote ni wa salma(kumbuka kuna mwanasheria alitamka kuwa safari nyingi za viongozi nchi za nje ni kubadilisha damu na halijakanushwa mpaka leo.

3.Kitendo cha kwenda kuwapa pole wananchi wa kilosa baada ya mafuriko na kuwaambai kuwa wanasema watoto wengine hawapendi kucheza(wewe mtoto mbona hupendi kucheza...nukuu) ili wazazi wapate muda wa kufanya ngono maana wapo kwenye chumba kimoja.je utapata hamu vipi ya kufanya ngono mchana huku chakula chenyewe shida na nyumba hauna;

je haya yote si matusi????? Watanzania tuamke na tufanye uamuzi wa busara jumapili na hakika usemi utaendelea kusimama"asiyefunzwa na wazazi atafunzwa na ulimwengu.
 
Wana JF, hakuna mtu aliyerekodi speech ya huyu mpiganaji? Naomba aidondoshe hapa mtandaoni. Make siamini kama kweli alitamka maneno hayo ya tu 'ASIYEFUNZWA NA MAMAYE ATAFUNZWA NA ULIMWENGU' na ikachukuliwa kuwa ni TUSI bila kuongeza maneno mengine ya matusi.

Nijuavyo mimi ASIYEFUNZWA NA MAMAYE HUFUNZWA NA ULIMWENGU NI METHALI YA KISWAHILI yenye kufundisha na kuwmelekeza mtu ambaye ameikosea jamii kwa tabia zake mbaya au usimamizi mbaya wa kaya yake au jambo lolote.
Nilimwona Kova kwenye runinga akidai kuwa HAWEZI KUTAMKA HAYO MANENO YA MTUHUMIWA MAANA NI MATUSI YA NGUONI.
Je,KOVA anataka kutuambia kuwa kusema au kutamka methali hii ya Kiswahili sanifu ni matusi ya nguoni kweli??? Kama ni hivyo basi vitabu vyote vya Kiswahili mashuleni vifutwe maana vinafundisha watoto wetu MATUSI YA NGUONI.

Kama kweli alitamka hiyo methali halafu wanasema kamtukana JK basi ni uongo na unafiki wa hali ya juu.
 
kazi ipo! ila tutahinda tu wacha wawatengenezee wenzao majina kwa kuwakamata kila kukicha bila sababu!! wanaacha vibaka huko mtaani wanaangaika na wakombozi wao!! STUPID IDIOT!!
 
Ndugu zangu, nimechelwa sana kujibu tuhuma dhidi yangu kwani ni mimi Dickson Amos Ng'hily ndo nilituhumiwa kumtukana Rais Kikwete....Nway mengi yamesemwa..Ndugu zangu...ninachoseam ni kile kile nilichowaambia police....sikumtukana rais coz urais ni taasisi na kamwe siwezi kuitukana..ninaiheshimu sana...ila mimi nilimuongelea bwana mmoja anaitwa Kikwete....Na yale niliyosema siyo matusi...na ukweli sikusudii na sitarajii kuomba msamaha kwani ninaamini nilichokisema siyo tusi...Na ukweli sijutii nilichokisema na hata polisi niliwaeleza na ndio maana baada ya kuhojiwa kwa saa tano...waliniachia huru na kunipa onyo kuwa japo sio tusi ila wanaomba nisirudie kusema maneno kama hayo.....Wanaotaka maelezo zaid wanaweza kuwasiliana na mimi moja kwa moja kwa kutumia barua pepe yangu ya nghily@hotmail.com au dick333amos@yahoo.com au kwa simu ya kiganjani ya +255 71 603 0030, +255 78 803 0030 na +255 76 503 0030...Asanteni kwa michango yenu....
 
umefanya vizuri mzee,, ujue hakuna kitu kinachoweza kuthibitika kama muhusika hajatoa tamko fulani, any way ki ukweli wewe Jimbo la Temeke ulikuwa unalichukua kiukweli kabisa,, na ile kauli ndio CCM walichukulia Gape na kuweza kufumba macho ya watanzania wengi waliokupigia kura,, cha msingi naomba uungane na waliopata ubunge kama moto wa Chadema kulazimisha Katiba mpya,, lile si tusi lakini ndo ivyo tena Muheshimiwa kwenye Kampaign angalia Kauli nazo si Mzuri katika kuwabadilisha wananchi Mfano mzuri ni CUF wanaanguka kisiasa kwasababu ya Kauli zao,, ""jino kwajino,, na zinginezo"""
 
Nashukuru bwana Silva25 kwa maoni yako na ukweli nayaheshimu sana....Ila ukweli kwa kauli ile ambayo katika mikutano yangu yote 65 niliyofanya, nilikuwa nikiitumia na ilinifanya watu wakubaliane na mimi kwani nao walikuwa wanaona kile ambacho wakubwa wamewafanyia na hivyo kutafsiri kuwa 'WAMEWAKOSEA HESHIMA' ambalo ni neno lenye maana moja na kukosa adabu.Ndugu yangu Silva25 naomba pia nikujulishe kuwa Ujasiri niliokuwa nao na ambao naendelea kuwa nao, uliwafanya wakazi wa Temeke kusea naomba ninukuu...."Kama huyu bwana mdogo hajawa mbunge ameonyesha ujasiri huu na kusema hayo aliyosema, hivi akiwa mbunge itakuwaje?Maana bungeni atakuwa na kinga si huko ndo atawatetea wanachi na kuibua hoja za nguvu bila woga". Nway nakubalia nawe kuwa huu ni wakati wa kujipanga upya kwa ajili ya 2015, hata hivyo yote nawaachia wanachama wenzangu na chama kama kitanipa ridhaa 2015 basi nitasimama,tuombe uzima.Hata hivyo mimi ni mbunge wa nje so nitahakikisha naendelea kuwatetea wananchi wangu na hata kama itanigharimu maisha yangu.....Asanteni sana......
 
Nashukuru sana Muheshimiwa Ng'hili unajua uungwana huanzia kwenye kujiamini ndio umnakuwa Muungwana,, hakuna Muungwana asiyejiamini,, Mfano (W.Slaa,, Zitto, ) *Marehem A Chifupa,, Molinge Sokoine*
Kujiamini kwao ndiko kukaleta maswali mengi na hapo watanzania wakaanzakujua vitu,, wengine ni Karamagi, na Sitta Kuruhusu mijadala migumu ambayo kama si kujiamini huwezi kufanya hayo mambo"" mimi nitakuchek kwa Email tuongee vizuri na tujue tunajipanga vipi>>
 
Ndugu yangu Safari...

Nashukuru sana kwa kuamini kuwa nimetukana...Ukweli cwezi kukuondoa katika imani hiyo kama wewe mwenyewe haujakubari...Nway ninachoweza kusema ni kwamba...soma hukumu ya kesi ya Rev Mtikila utapata majibu...Au naomba uangalie kamusi ya kiswahili ili ujue hilo nililolisema ni au la kuliko kuhukumu kabla ya kupata maana. Lakini kama hukusikia na haujui nilichokisema ambacho kinatamkwa kuwa tusi...basi utakuwa haujanitendea haki....wazungu wanasema 'WITHOUT A RESEARCH NO RIGHT TO SPEAK'...Hili nawashauri wote wanaonituhumu yet hawakusikia na hawajui tusi lenyewe ni nini...nawashauri wafanye kwanza utafiti kisha ndo wazungumze....Hata hvyo ninaendelea kusema kuwa nashukuru kwa maoni yako kani una uhuru wa kutoa mawazo yako na yakasikika.....By the way nilisahau kujitambulisha...mimi ndo Ng'hily mwenyewe niliyekuwa nagombea UBUNGE huko TEMEKE kwa tiketi ya CHADEMA. Niko huru na wala hakuna kesi yeyote inayoendela dhidi yangu...Asante sana......
 
Demokrasia Afrika bado,kwani Jk alidhurika nini,angekuchapa kama aliemchampa mzee ruksa sawa,mbona kina George Bush,Clinton wanatukanwa ktk music wanatajwa majina yao lakini usikii wwalioimba wamefungwa au kuchapwa viboko soma haya mashairi ya wimbo wa Eminem unaitwa Mosh
EMINEM LYRICS - Mosh
halafu usikilize ktk video www.youtube.com/mosh
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom