Asiye na dhambi awe wa kwanza kumrushia jiwe Lowassa

Picha zitasema hapa
 

Attachments

  • 1441626194262.jpg
    1441626194262.jpg
    24.7 KB · Views: 153
  • 1441626275389.jpg
    1441626275389.jpg
    6.3 KB · Views: 151
  • 1441626310489.jpg
    1441626310489.jpg
    30.7 KB · Views: 148
Wanajukwaa,
Ivi Tanzania si ina maliasi za kutosha? Madini hatuna? Mbuga za wanyama hatuna?

Hivi Bandari zetu tunafaidika na nini?

Je ni Lowassa Ndo kachukua hela zote izo?
Je ni Lowassa ndo kamaliza wanyama wetu?

so kama kuna mtu ambaye sio fisadi Ccm na awe wa kwanza kumtuhumu Lowassa.

bora ungekaa kimya kwa unahalarisha ufisad wa lowasa nyie ndio wale mlioitwa malofa na mkapa
 
Wanajukwaa,
Ivi Tanzania si ina maliasi za kutosha? Madini hatuna? Mbuga za wanyama hatuna?

Hivi Bandari zetu tunafaidika na nini?

Je ni Lowassa Ndo kachukua hela zote izo?
Je ni Lowassa ndo kamaliza wanyama wetu?

so kama kuna mtu ambaye sio fisadi Ccm na awe wa kwanza kumtuhumu Lowassa.

Bandari si wanayo marafiki wa Lowassa, Karamagi? Na kwa taarifa yako, Karamagi ni mmoja wa wafadhili wa kampeni za Lowassa kwa makubaliano ya kuongezewa muda wa kufaidi bandari. Usione hela zinamwagwa ukadhani ni 'sadaka' Watanzania watalipa kila senti inayotumika kwa huyu bwana.
 
ASIYE NADHAMBI AWE WAKWANZA KUMRUSHIA JIWE LOWASSA

Imenichukua mda kupata tafsili ya neno " kujivua gamba" kwa viongozi wetu wa CCM nimelikosa.Nimsemo unaotumika sasa na viongozi wa CCM baada ya kutoka kwenye kikao cha kukosoana baada yakugundua kuwa walikuwa hawawatendei haki watanzania kwakufuja mali za watanzania.

Leo hii imekuja sera yakuwatoa kafara watu walioitwa "hawakubariki "kwenye chama mmoja ya watu hao ni Ndugu Edward Lowassa .Kama inavyofahamika kuwa huyu alibeba zigo zima la RICHMOND mitambo ya kuzalisha umeme.Hii ilitokana kuwa yeye alikuwa mtendaji mkubwa serikalini (waziri mkuu wa Tanzania).

Sina hakika kama kuna gazeti lilishawahi kumwandika kwa mazuri zaidi yakusema kuwa ndiye chanzo kikuu cha kuingiza Taifa kwenye mgogoro wa umeme na kampuni hiyo.Lakini kwaupande wangu nasema mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.

Katika viongozi waliopo katika chama cha mapinduzi (CCM) nadhani hawazidi watano au sita ambao wanaweza kusema wao wako safi na hawajaifikisha Tanzania hapa tulipo.

Leo hii viongozi wa CCM wanaitana kuambizana achia madaraka kweli!!?? Bila hata aibu? Nikipi hasa cha kuwafukuza wengine na wengine wakabaki kama siunafiki na umbea kuchongeana mbele ya wananchi wengine waonekana hawafai wengine niwazuri.Hii nijambo la ajabu sana hata magazeti kila siku kuandika ubaya wa mtu mmoja wengine hawaguswi kama nichuki binasfi kati yenu na Lowasa nibora kusema.


Imenilazimu kuandika hivi kama mtanzani mwanachama wa CCM nisiyependa unafiki.Najuwa watasema kuna njia yakuwasilisha malalamiko na si kwanjia hii ya magazeti.Mimi nasema njia hiyo niyaviongozi na sisi wa hali yachini haituhusu maana kama ingekuwa inatuhusu maamuzi mengi yangeletwa kwetu na sisi tutoe maoni yetu. Kwa kuwa kusema ukweli daima ni moja ya imani za chama chetu

Najaribu kuweka wazi kuwa simfahamu Mheshimiwa Lowasa kwa undani kwa maana kuwa sijawahi kufanyanaye kazi au kukutana naye kwa njia yoyote ile zadi yakukutana naye kwenye utendaji wake wakazi kama Waziri mkuu na mimi kama raia.

Kinachonisikitisha zaidi nikusoma katika vyombo vya habari kuwa kunasiku aliitwa na viongozi wakuu wa CCM nakumwomba ajivue gamba kwakuwa watu wanamsema vibaya kwa kweli kwa hili walimkosea na wanatakiwa kumwomba samahani kwa kumweka kwenye kundi hili sikwamba hastahiri kuwa huko ila kwa mambo aliyoyafanya kama kiongozi wa kitaifa nimakubwa zaidi ya anayoshutumiwa.

Wapo wanaostahili kuwajibika kwa kuwa wamelitumbukiza taifa hapa lilipo kwa mfano walioleta hoja ya mrahaba kwenye migodi leo tunakula makapi ya zahabu zahabu yote wanabeba wanapeleka kwao viongozi wanapasenti zao,kuuzwa nyumba za serikali,kulipana posho zisizo stahili,posho za wabunge ambazo niubinafsi,magari yakifahari matumizi makubwa ya serikali,waliouwa viwanda,vyama vya ushirika leo viko taabani na watuhumiwa wapo wanakula raha nchi hii na vitu vingi vinavyo waumiza watanzania .

Kuna mwasisi waujamaa ambaye kwa uongozi wake enzi za baba wa taifa alitakiwa leo hii awemshauri wa viongozi lakini yeye ndiye wakwanza kulitafuna taifa kupitia familia yake kwenye ukusanyaji ushuru ubungo.Kuna aliyekuwa Rais wa nchi hii tuhuma rukuki amemwagiwa kati ya hizo asilimia sabini sizakweli lakini zilizobaki nizakweli je niatuagani watu hawa wamechukuliwa hatua?Je nawao wanatakiwa kujivua gamba ?

Hata kashfa ya mkataba wa kuzalisha umeme ya Richmond ambayo inaelekea kuweka msumari wa mwisho katika maisha ya kisiasa ya Lowassa ndani ya CCM, inaelezeka kwamba, nchi ilikuwa inaingia gizani kama ambavyo imekuwa gizani hata baada ya kashfa hiyo. Lowassa kwa nafasi na kawaida yake ya kulazimisha mambo kwa manufaa ya taifa, akafanya maamuzi yanayomgharimu mpaka leo.

Kisiasa anaweza kujitetea kuwa alikuwa anafanya hivyo ili serikali ya rafiki yake isiaibike mbele ya wapiga kura. Tamko la namna hiyo ni tusi kwa mkuu wa nchi na ndiyo maana zigo hili linamwelemea Lowassa mpaka leo. Anabeba gharama ya kutenda vema kwa njia mbaya. Na huo ndiyo ubaya wa Lowassa kwa mtu mwenye mtizamo endelevu anaweza kumwelewa.

Tujiulize kama si unafiki nini leo mitambo imewaka Rais wetu yuko mstari wa mbele kuwapokea kwa jina la Symbion hakuna gazeti linalopiga kelele wala wabunge wetu wote wako kimya ,Hata hao viongozi wa CCM hakuna anayehoji kama uhalali wa mitambo hiyo kuuzwa wakati kisheria tulitakiwa kuwanyanganya kutokana na utapeli walioufanya RICHMOND huku kesi iko mahakamani.Inatia aibu kuwa tunaviongozi makini .

Tufike sehemu viongozi wetu waache unafiki hii yote ni unafiki kama kweli wanataka kujivua gamba waanze na aliyekuwa spika wajamuhuri ya muungano Samweli sitta na mwenzake Spika msaidizi Anna Makinda, Waziri mkuu wa sasa Mizengo Pinda hawa ndiyo wanajuwa ukweli wa RICHMOND na kukatisha mjadala bungeni huku wakiweka chama mbele Taifa nyuma leo ndiyo wanaona uchungu kuwa watanzania hawatendewi haki !? ndiyo wanajivua gamba niunafiki mkubwa huu.

Hakuna hata kiongozi mmoja leo hii wa CCM ambaye anaweza kusimama na kusema yuko kwa ajili ya watanzania.Haiitaji kwenda chuo wala kumaliza elimu ya msingi ili utambue kuwa maisha nimagu kwa watanzania ambao wanakila kitu,Mito,Maji ,Madini,Aridhi na vitu vingi sana ambavyo leo hii tungekuwa na unafuu wa maisha ila tatizo kubwa niuongozi au mfumo mbovu uliopo.Sasa hawa viongozi watajitoa vipi kwamba wao sigamba na wenzao nimagamba?

Waache kuzurula na kuhubiri kwa watanzania hasa wa vijijini wasichoweza kukitekeleza kwa kuwa wao pia ni gamba gumu.Ningumu kuelewa viongozi wa CCM wanapata wapi ujasili wakuwavua magamba wengine wakati nchi iko taabani na wao ndiyo wanoongoza dola!!?Turudi nyuma tumwogope mungu tuwatendee haki watanzania tuache unafiki.

Mwisho kama mhesimiwa Edward Lowassa unasoma makala hii basi nakushauri ugombee urais wapo wananchi tunaotambua uongozi wako na nchi hii inakuitaji.Usijali magazeti yanaandika nini watu wanasema nini kama kweli dhamira yako kweli ilikuwa nikuiondoa Tanzania kwenye giza ila kunawatu waliotumia mwanya huo kukuingiza mtegoni ambao serikali iliyopo imeshindwa kuwachukulia hatua endelea kufanya mikakati yakuingia ikulu.
Behind this scene wewe ni UKAWA NA si CCM.
 
Lowassa angekuwa FIsadi sasa hivi Ungekuta amehama nchi .. CCM ni hatari sana ... Real Fisadi wamiliki wa Bank M hawaguswi ...
 
CCM kama walizoea kuhonga mwaka huu wamekwisha pesa zao zinaliwa na watu bado wanadai Lowassa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom