Saint Ivuga
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 54,363
- 58,386
UMOJA wa Ulaya (EU) umeipatia serikali ya Tanzania kiasi cha euro milioni 383 (sawa na sh bilioni 750) huku ikiionya juu ya ufisadi na utendaji mbovu unaozorotesha sekta ya miundombinu.
Kwa mwenendo huo, EU inataka yawepo mageuzi ya kweli na yanayoonekana, mijadala kwenye mambo magumu yanayohitaji kushughulikiwa pamoja na ahadi ya kuiweka Tanzania kwenye mstari wa mwendokasi.
Akisaini makubaliano ya kutoa kiasi hicho mbele ya Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, Balozi wa EU nchini, Tim Clarke alisema wengi wakiwemo wabia wa maendeleo watashangazwa na hatua hiyo, kwani kwa sasa habari zilizopo Tanzania ni rushwa na upotevu wa fedha za umma.
Ndiyo, watu wengi wabia wa maendeleo wa Tanzania navyama vya kijamii wanaweza kuuliza mantiki ya kutoa misaada hii kipindi ambacho vyombo vya habari vimejaa habari za kashfa za rushwa na ufisadi na upotevu mkubwa wa fedha za umma, alisema balozi huyo.
Kwa mujibu wa Clarke, wabia wa maendeleo na serikali wamekwishafanya mapitio ya mwaka na kugundua si mazuri (moderate satisfactory) huku mageuzi katika sekta ya umma yakiwa na hali mbaya.
Clarke alionyesha kushangazwa na utendaji wa hali ya chini wa bandari na reli, miundombinu ambayo ingeweza kuifanya Tanzania na Afrika Mashariki kuonekana kuwa kinara wa maendeleo ya biashara na uchumi, lakini badala yake hali katika maeneo hayo inasikitisha.
Balozi huyo alisema uendeshaji wa sekta hizo nyeti umebaki kuwa wa mazoea huku maslahi ya baadhi ya watu, urasimu na kukosa ubunifu ni mambo ambayo yamekuwa yamechangia kutofikiwa kwa malengo.
Kutokana na matatizo hayo ya utekelezaji aliyoyaainisha, Clarke aliieleza waziwazi kuwa EU haitaruhusu malipo kupitia kwenye hazina bila ya kuhakikishiwa fedha zinazotolewa zitatumika ipasavyo, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha walimu na watumishi wa afya vijijini wanapata fedha zao bila kupunjwa.
Baada ya kusema hivyo, sisi pia tuna matatizo katika utawala, vita dhidi ya ufisadi, haki za binadamu, ujenzi wa demokrasia ya uwajibikaji na uwazi. Sisi pia hatuwezi na hatutaweza kufumbia macho haya, alisisitiza.
Alieleza fedha zilizotolewa na EU licha ya mambo yote hayo ni ubia wa umoja huo na Tanzania ambao si wa fedha tu bali uanzishaji wa misingi ya kuaminiana kati ya serikali na wabia wengine na kutambua mchango wake kwa kutoa hifadhi kwa wakimbizi pamoja na ukombozi wa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Alidokeza kuwa makubaliano ya kusaini kiasi hicho cha fedha yanakuja huku Ulaya ikibadilika, hasa baada ya kupitishwa kwa Mkataba wa Lisbon na haijulikani kitakachotokea.
Naye Waziri Mkulo baada ya kusaini mkataba huo, ambao umeifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi saba pekee kupewa fedha hizo, alisema kiasi hicho kitatoa mwongozo kwa EU katika kuisaidia Tanzania katika kupambana na umasikini katika mpango huo wa kuisaidia bajeti.
Nimeelezwa ya kwamba Tanzania ni miongoni mwa nchi saba za Kiafrika katika mpango huu wa kipekee wa misaada, alisema Mkulo.
Akieleza baadhi ya maeneo fedha hizo zitakapoelekezwa, Mkulo alisema euro milioni tano zitapelekwa Kituo cha Takwimu cha Taifa (NBS) wakati euro milioni mbili zitapelekwa katika kitengo cha sukari.
Alikiri kuwa nchi inakabiliwa na tatizo la miundombinu kiasi cha kutoweza kumudu changamoto za ukuaji wa uchumi.
Kwa mujibu wa taarifa ya EU juu ya fedha hizo, lengo lake ni kusaidia Tanzania kutimiza malengo ya milenia.
Hata hivyo, wahisani wamechangia fedha hizo licha ya kuwepo kwa tuhuma nyingi za ufisadi, huku Rais Jakaya Kikwete wakati akizindua jengo la Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini (TAKUKURU) akisema zaidi ya asilimia 30 ya bajeti inaliwa na watumishi wasio waaminifu.
Kiasi hicho kinakaribia asilimia 36 ya bajeti ambayo wahisani wanachangia, jambo lililowafanya wanasiasa kuuchachamalia utawala wa awamu hii kupambana na ufisadi.
source.tanzania daima