Asili ya maneno 'Shikamoo' na 'Marahaba' ni utumwa, kwanini tunaendelea kuyatumia?

SF,
Hii inatokana na kwamba - unapotanguliza shikamoo ni kama umeweka kizuizi cha heshima.Anapokataa kuitika inavyotakiwa ni kwamba alikuwa ana mpango mwingine na wewe na anashangaa barrier ya nini tena?

Ok kama hata alikuwa na mpango mwingine kwa nini asiitikie salamu yangu then akaendelea kutia hilo neno lake.Kwani akiitikia shikamoo yangu age yake itabadilika na kuwa young?.I think kuwa wazee wengine hawataki kuzeeka wanadhani bado wao ni vijana.

Kwanza how do you say shimakoo in english?labda ukisema hivyo mtu ataona humuoni yeye kama ni mzee.
 
I touch your feet hahahah
ndiyo maana nikasema lugha nyingi hata za kikabila hazina equivalent ya shikamoo maana hata kama kuna hierachy siyo za kujitweza ki ivo.
 
With time hili neno litaachwa. Wengi wetu sasa hivi, hasa mijini ambako kuna wakazi 33% ya Watanzania, watu wanakwepa kutumia shikamoo maofisini; kuitoa au kuipokea. Wale ambao wamenizidi miaka 15 hawana tabu kuipokea, ila walionizidi miaka 10 hivi, wanaitikia japo kwa haya kiaina.

Nani ofisini kwao watu wanaendekeza shikamoo?
 
sidhani kama maofisini siku hizi watu wanasalimiana shikamoo tena.

Licha ya hivyo kama ukichukulia mfano Tanzania siku hizi majority wanaongea english all the time iwe anywhere pub/jikiweni you name it. Na pia ukiangalia matumizi ya lugha za kikabila pia zinapotez taratibu maana watu hawaoani tena wenyewe kwa wenyewe na inakuwa shida sana kumfundisha mtoto kabila.mfano mchaga kwenda kumuoa mmakonde hapo utamfundisha mtoto lugha gani? zaidi ya english na kiswahili.

Hata matumizi ya lugha ya kiswahili sasa hivi yatapotea mfano kama watu walioko state kuna wengine wanaona hata aibu kutumia lugha yake mbele ya mmarekani badala ya kuwa proud anaona kama atadharaulika "Kasumba". Na pia kuna wengine wanaogopa hata kusema originality yake why? Anaona ataonekana mshamba. So stupid!. Be proud of your country/where you come from and the language you speak. Tutakiua kiswahili hivi hivi maana siku hizi kuna watu wana accent kwenye kuongea kiswahili.

I guess nimeweka point sawa.
 
shikamoo waulizeni watu wa Tanga watawaambia maana yake kwani hawa wenzetu wanalitumia sana.... eti mtu kaolewa anamwamkia mumewe shikamoo hata mara tatu kwa siku....... labda wenzetu wanaelewa maana yake zaidi kuliko tunavyoelewa sisi wengine...
 
Kwa mtizamo wangu shikamoo ni salamu inaonyesha unamuheshimu mtu aliyokuzidi umri. Lkn siku hizi haina umuhimu kama ilivyokuwa zamani. Siku hizi ukimsalimia mbaba mtu mzima anakwambia "Unanipa shikamoo unaninyima nn?" Kwa hiyo inaonekana kama heshima ya kitumwa.
 
Wachangiaji mbalimbali waliandika
"Ni kweli shikamoo lina asili ya utumwa..".

Je kuna mtu mwenye uhakika?

Kuna utafiti wa kihistoria?
Jibu "marahaba" ni umbo la salamu ya kawaida ya Kiarabu huko wanasalimiana "marhaba" na jibu ni "marhabteen" (=marhaba mara mbili).

Jinsi ilivyo "Shikamoo" ni moja kati ya salamu katika tamaduni mbalimbali zinazotambua tofauti ya cheo.

* Zamani watu wa Ulaya walipiga magoti mbele mkubwa wakimsalimu;

* watu wa Uajemi walijulikana kwa desturi ya kujitupa chini kabisa ardhini mbele ya mkubwa;

* katika sehemu ya Asia ya kusini watu husalimiana kwa kufunga mikono yote miwili (karibu kama wakatoliki wakisali) na kama ni mkubwa wanashika mikono juu ya kichwa kama ni cheo sawa mbele ya uso na kama ni mdogo chini ya kichwa kifuani.

Tamaduni zilizobadilika sana watu waliacha mara nyingi aina hizi za kusalimia angalia Marekani ambako watu hupeana tu sauti kama "hai" (Hi!) isiyo na maana ndani yake.

Ni juu ya watu kuamua. Binafsi sioni ubaya kumpa mzee maskini heshima ya kifalme kwa kumsalimia kwa "shikamoo".

Nakumbuka watoto wangu walipofika Kenya mara ya kwanza waliwasalimu watu wazima kwa "shikamoo" kote tulikoenda madukani n.k. Walilalamika saaana ya kwamba hawa Wakenya hawakujibu! Ni kweli- nje ya Mombasa hawajui kabisa.
 
Kwa kweli hili neno halifai, kwani ata kwenye lugha mbalimbali za makabila yetu mtoto ana msalimia mkubwa kwa tafsiri ya kiswahili kama ni asubuhi, wanasema habari ya asubuhi alikazalika mchana na jioni. Sasa hii habari ya kuwa chini ya miguu ya mtu inakuwaje! Hata kama limekuwa linatumika muda mrefu linatumiwa kimakosa, ni salamu za Mabwana na Watwana.
 
Habarini wana JF: Nimekuwa nikijiuliza sana tafsiri halisi ya maneno haya mawili Shikamoo na Marhaba. Na pia nataka kujua zaidi ya Tanzania ni nchi gani wanatumia aina hii ya salamu! NAWASILISHA.
 
Habarini wana JF: Nimekuwa nikijiuliza sana tafsiri halisi ya maneno haya mawili Shikamoo na Marhaba. Na pia nataka kujua zaidi ya Tanzania ni nchi gani wanatumia aina hii ya salamu! NAWASILISHA.

Shikamoo = Nashika miguu yenye maana nipo chini ya miguu yako. Hii ilikuwa enzi za kitumwa za mwarabu
 
kama hujui hata maana ya shikamoo na marahaba JF sio mahala pako. humu tunataka watu wenye uelewa na uwezo wa kupambanua mambo... hilo swali kamuulize mwalimu wako wa chekechea.....
 
kama hujui hata maana ya shikamoo na marahaba JF sio mahala pako. humu tunataka watu wenye uelewa na uwezo wa kupambanua mambo... hilo swali kamuulize mwalimu wako wa chekechea.....

wee hujui maana ya hayo maneno! bora uulize ueleweshwe kuliko kujifanya mjuaji!
 
Mkuu jamaa kauliza swali ingefaa zaidi umjibu kuliko kumzodoa kwani wewe ni sehemu ya the great thinkers
jamani..........., nimemzodoa ACTIVISTA not otherwise!!

hata wewe pia hujui na hutaki kuadmit kuwa hujui!

by the way, shikamoo ......niko chini ya miguu yako bwana wangu!
Marhaba...........inuka mtumwa wangu!
 
kama hujui hata maana ya shikamoo na marahaba JF sio mahala pako. humu tunataka watu wenye uelewa na uwezo wa kupambanua mambo... hilo swali kamuulize mwalimu wako wa chekechea.....

Kweli wewe ni Great Sinker!
 
Nijuavyo mimi neno "shikamoo" hasa limebadilishwa, lilikua "Nakushikamoo" kwa maana ya nakushika miguu au nipo chini ya miguu yako kama walivyosema waliotangulia kuchangia. "Marhaba/marahaba" ni neno la kiarabu lenye maana ya "Karibu" kama alivyochangia mkuu Mipangomingi. Pia neno "Marhaba" hutumiwa kumaanisha kua umeridhika; ni sawa na kusema "sawa sawa".
 
Kama walivyosema baadhi ya walotangulia kujibu ni kuwa Shikamoo maana yake (au asili yake) ni nakushika miguu au nipo chini ya miiguu yako, tafsiri kamili ya kiswahili safi ni "nakuangukia mkuu" Pia shikamoo yaweza kutafsiriwa kama "heshima yako mkuu"

Na anayeamkiwa atajibu marahaba, au ahsante (karibu na ahsante), na kwa wakati huohuo inamaanisha kuwa unakataa kushilkwa hiyo miguu na huyo mtoto alokuamkia. Kwa tafsiri hiyo ina maana ukimpa mtu shikamoo na akaisikia lakini akakaa kimya (akauchuna), ina maana umwangukie na umshike miguu-yaani kuna kitu ambacho hajafurahishwa nacho kwako na inabidi umwangukie ki ukweli!

Mnajua lugha ya kiswahili ni mchanganyiko wa lugha nyingi na mtazamo wangu binafsi ni katika kiswahili Shikamoo na marahaba ni kitu kikubwa sana ambacho lugha nyingi hazina, kwani shikamoo ni ya mdogo to kumwamkia mkubwa (au mzazi) kwa heshima na taadhima zote! na mkubwa akiwa anaihitajia atakuambia hujambo?, nawe yabidi uitikie, sijambo shikamoo (baba, mama, babu, kaka, dada, shangazi nk)
 
Swadakta...
Kuongezea kwenye red..wakati ule wa utumwa ilitumika khasa yule mtumwa akiwa anamuona saidina wake ndio alitakiwa kutoa salamu hiyo akijidhihirisha kuwa yeye ni dhalili mbele ya huyo bwana mkubwa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom